Weekend story: Chura Ananesanesa! Jike Shupaza

Weekend story: Chura Ananesanesa! Jike Shupaza

Igweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Siku hizi nimekuwa demoted, so niko branch Kariakoo nachoma mahindi tu, jamaniiii. Sasa huku kariakoo kwenda kila siku ndo nikakutana na wanangu wenyewe wa kitambooo longtime ndo mashangingi ya kariakoo wana vitu vikali Hyundai za kufa mtu, Vogue ndo kukaa kitako sasa wakanipa Throw Back toka tulivoachana kitambo kile waliniacha niko STD 1. PATA HABARI KAMILI HUSTLES ZAO, MIZINGUO YA WANAUME, ULAJI TIGO WA MAISHA, MIHANGAIKO, MPAKA WAO KUTOKA NA KUWA WANAWAKE WENYE LIQUIDITY 50m KWENDA JUU AFU WOTE STD 7 ALIESOMA SANAAAA FORM 4. (HII NI INSPIRATION PIECE KWA WADADA KUWA UKIWAENDEKEZA WANAUME HUTOKI LEO WALA KESHO.


1997 STD 7.

Elvin nakupenda sanaa mpenzi wangu, kama vipi ukimaliza shule tu mi nikuoe tuanze maisha, sina vikubwa ila naweza kutunza mke na watoto. Kweli Freddy? Kweli niamini mimi navokwambia nakupenda kichiziiii. Nakuelewa sanaaa. Basi sawa nitawaambia wazazi wangu sitaki shule nataka kuolewa. Usifanye hivo Elvin isitoshe wewe bado mwanafunzi, cha kufanya subiri umalize shuleeee. Sawa Freddy. Sasa mi naenda. Chukua hii Elly itakusaidia. Akawa kamfinyia kwenye mkono. Kuifungua mbele kumbe 1000. Kipindi hiko chips 200 ilikuwa pesa ndefu.

Harriet we mjinga bi mkubwa kapika nini huko jikoni? Kapika Ugali na mlenda. Mmmmmmh! Sasa sikia wewe boya, mi nimetoka kwa Freddy kanigea buku hili kama vipi kanunua chips sahani 2 tuje tufanye yetu, mi mlenda haushuki kabisaaaa. Weeeeeeee! Unasema kweli Elly? Ndo manake. Poa leta.

Harriet alivoenda kwenye chipps akamuona Freddy, akaamua kumsabahi, Freddy mambo! Poa niaje? Fresh tu. Nilikuwa na Elly sasa hivi. Kanituma chips. Harrieth unapendezaaa ujue. Acha masihara yako Freddy. Mi sina churaaaa kama ya Elly si unajua mi Betinaaa. Sasa sikia Harrieth kesho fanya uje ghetto kwangu. Mmmmmmhhh! Harrieth akasita. We njooo. Freddy anamkolezaa.

Elly akijua je? Si unajua Dodoma ndogo hiii. Hawezi kujua kwani wewe ndo utamwambia? Hapanaaaa! Chukua hii akamgea 2000. Harrieth akanunua chips na mayai 2 akarudi nazo kwa Elly, wakawa chumbani ndo wanataka kuzila Hamad! Bi mkubwa kaingia. Nyie watoto malaya sijawahi kuona haya nani kawafunua na kuwanunulia chips yai? Hamna mama pua zako tu. Msinizeveze mwenyewe kijana wa jana, toeni viepe hivo tule hapa, hilo nguna takuja kula huyo mzee na wanae. Hahahaaaaaaaa! Wakacheka wote.

Tamu hizo wala si unafiki, kakwahonga nani hiziii? Yule fundi au kuna mwingine? Na mna moyo alivo mchafuuu na magrisi yake mie nisingemuwezaa. Hahahaaaaa! Wakachekaaa. Elly churaaa hio itakuponzaa, upande wa baba yako huo, shangazi zako wamefungasha vyura hatariiiiii, na vya kurithi vinazidi, binti mdogo kama wewe churaaa kubwaaa loooh! Ila mzaa chema nafaidi kama hivi. Hahahaaaaaaaaaa! Wakacheka wote tenaaa.

Kesho Harrieth akaenda kwa Freddy mchana, wakaanza uhusiano na Freddy kwa siri. Ujue nini Harieth, Elly mambo mengi sanaa hajatuliaa, ana wanaume wengi afu mi design nataka mke, so kama vipi mi nitakuoa wewe. Sawaaa! Harrieth aitikia mwanamke hana hayaa kuchukua mwanaume wa binamu yake. Ikawa ndo mahusiano kamili sasa.

We elly njoo kwanza wifi yangu. Akaenda shikamoni. Marahabaaaaaaa! Jamani maniona churaaaaa hio, mnaona msambwandaaa huooo wa wifi languu, huyu ndo Elly bwanaaa, kama mchinaaa kitu original akichamba hatakati! Hahahaaaaaaaaaa! Halooooooooooooo! Tunaona shogaa kafungasha si uongo. Sasa wifi sikia nasikia kaka yangu umalaya wake ana kimwanamke Betina bonge anakiingiza kwake we chunguza wifi yangu usiniamini mimi. Tena anakiingizaga mchanaa. Elly akachokaaaaaaa. Akayaweka akilini. Akaaga tu pale akaondoka.

Usiku akataka amwambe Harrieth akasiata akaamua mchana akachungulie ajua ataona nini. Mchana akawa kabana jirani.Akamuona Harrieth anaingia na Freddy kwake. Akachokaaa! Akakaaa pale hana nguvuuu. Masaa yakapita wakatoka, akawafata na kuwasalimu, Harrieth akakimbia anamjua Elly mgomvi sanaa. Freddy likamshuka tuuu. Elly akamwambia kuanzia leo endelea na Harrieth. Freddy anaona haya tu.

Kufika nyumbani saa 2 Harrieth hajaja anaogopa Elly atamkunguta na kumshushia kipigo heavy kwa kumchukulia bwanaa. Elly akajua alipo akamfata Harieth akakimbia tenaa. Akamkimbiza mpaka akampata, akamwambia sikia twende home, mda umeenda mdingi kastukaaa. Mi sina dhiki ya mabwanaa nina kazi mpya ya maana kuliko huyo Freddy we endelea nae tu. Mi nina HB yule mtoto wa mkuu wa kituo cha polisi ana hela chafuu Freddy pumbu tuuuu. Harrieth akawa haamini. wakarudi nyumbani kimyaaaa kama sio wao. Ikawa Harry ana deal na Freddy, Elly yuko na HB.

Ikafika mda wa mtihani wa darasa la saba, wakafanya wote mwezi wa 9 wakawa wako nyumbani. Usiku wamelala Elly akamwambia Harry mi nataka niende DSM na HB kuanza maisha mambo yangu yashaharibika mda huu tunavoongea. Yameharibika kivipi Elly. Acha tu Harry. Hivi juzi bi mkubwa alivomkimbia muha ulionaaa? Hahahaaaaaaaaa! Wakacheka wote. Nimesikia Elly ila sijaipata vizuri nisimulie. Elly akaanza kumsimulia.

Bwana hili toto la humu ndani Hamisi, bi mkubwa si alikopa vitenge vya wax kwa muha, akawa kamuona nyumba ya 2, akaja hapa kupiga biti anajificha tumsitiri. Akamchimba biti mpaka Hamisi ole wake aseme kama yupo ndani, Hamisi yupo sisemi mimi mama sisemi kweli tena.

Kweli muha kaja, akamuuliza mama, tukamjibu hayupo, hadi Hamisi yupo hayupooo mama hayupooo. Muha akasema sawa mi naenda akawa kaanza kuondoka hata hajafika mbali toto lile lisivo na akili si likaanza kupayuka.

Mama aya toka humo ndani muha kashaaondoka, tumemdangaya tiari haupooo, toka tu mama. Wote tukabakia kinywa wazi haaaaaaaaaaaa. Na uhakika muha alimsikia vizuri kabisaa sema akaamua tu kuendela na safari kumsitiri tu bi mkubwa ila alijua kama alijificha ndani kusudi. Hhahaaaaaaaaaaaaa! Wakacheka wote.

Elly mi Freddy anataka kuja kunitolea barua. Elly akastukaaa ila akajikaushaaa, hongeraa Harry hongeraaa, bora yako kimeeleweka. Asante. Elly hamu ya story ikamuisha akaamua alale jumlaaa.

Kesho yake Herry anatembea kwa kujivutaa, bi mkubwa akastukaaaa. Hakusema kitu, akamnongoneza Hamisi. Harry akawa kaaga anaenda dukani, bi mkubwa anamzuia anamwambia subiri kwanza. Kila akitaka kutoka bi mkubwa anampiga pini. Elly akamuona bibi yao anakuja akahisi tu sio dalili nzuri akakimbia. Akamuitia Hamisi kwenye kona, ulienda kumuita bibi wa nini? Mi hata sijui. Sasa sikia Hamis kanisikilizie wataongea nini, na kwanini anamzuia Happy kutoka. Hamisi akamwambia hio chips yai. Hahahaaa! Elly akamwambia poaaa.

Kutokeza tu kona, bibi akadakwa juu juu wakachonga. Kuja wakamdaka Harry. Bibi yuko huyu mbona anayo kubwaaa sanaaaa, mimba ni kubwa sanaaa. Mpaka kavimba miguuu, yaani hii haina mwezi atajifungua mtumeeeee. Mama akachoka Harry!!!!!!!!! We si yatima wewe nakulea hapa kwa msaada. Mmmmmh mbona umenivua nguo? Freddy kasema ataleta posaa. Mama akazidi kupandwa jazba, haya nenda huko kwa Freddy fanya ufanyalo hio posaa ailete leo leo, tokaaaaaaaaaaa, bila posa usirudi hapaaaaaa.

Hamisi akaenda kumpasha Elly yaliojiri, Elly akachoka mwili na roho. Akamwambia bibi akiondoka njoo uniite. Saa mbili usiku ndo mshenga kuja na hio posa, ndo Elly kurudi na yeye anakaa mita 100 na bibi. Huku na huku kwa machale, bibi akielekea mashariki, yeye mngaribiii. Ugeni kuondokaa, Elly hana hili wala lile bibi huyu hapaa. Akasikia tu na huyu tayari siku nyingi mbonaaaaaa! Mama Elly akakaa chiniii. Looooohhhh!

Baba mtu hakuongea neno akaingia ndani kimyaaa. Mama mtu akaanza kilio. Bibi akaaga akaondoka. Elly akaenda kwa HB kumwambia wamejua inakuwaje? HB akasema nitawatuma wazazi wangu waje waongee nao kesho haina shida tuko pamoja baby wangu.

ITAENDELEA KESHO SAA4
 
great story lara1
yani usipopost jukwaa linapoaa
Big up for this special talent you have
 
Afadhali utusaidie kumpa vyake aisee... Na wengine wenye tabia za kishamba kama hizo waachage bhana...
 
laraaaaaa.....dahhh nataman ningekuwa karibu uwe unanihadithia tu.....aisee haya mafunzo tunayoyapata kibokoo asante sana
 
Hv mtu anavyo quote story nzima anataka mwandsh ajue na ww alimquote au? Lara anajua jinsi tunavyokunwa na uandishi wake hakuna haja ya kumuonyesha umemquote comment inatosha..mnakeraaaaa
 
Akazinduka wamemwagia maji ya baridi kibongo bongo akakaa kwanza watu wanaongea hawasikii wanaongea nini wala nini. Baadae akaingia kwenye nyumba tupu akatandika kitenge saa 11 hio akalala fofooo mpaka kesho yake saa 5 asubuhi. Akaamka anaharishaa. Akawa kachoka mwili na roho. Kila analoliwaza haliendi wala halirudi. Akiba aliyo nayo ni ndogo juzi juiz tu katoka kumtumia mama mtu hela. Akiwaza wanae ndo anachoka kabisaaa.

Akajizoa zoa akaenda Dimond, akangoja wakatoka. Akamuona mwanae wa kike Jacky anatoka. Akamuita Jacky! Jacky akafurahi mamaaaa! Akamuwaoh! Akaanza kulia mama umetuacha tunateseka. Mama mwingine anatupigaa anatufanyisha kazi zote, naosha vyombo, nadeki asubuhi kabla sijaja shule, napika, napigwaaa. Baba hatupendi. Asubuhi hamna schoolbus napanda daladala. Kaka Frank alivokuwa likizo alikuwa ananisindikiza ila sahivi nakuja mwenyewe. Akamuona kakonda na alivo mwembamba kazidi kukauka kau kau. Akamuuliza mnakaa wapi akamuelekeza, aksema sawa. Akamuuliza huyo mama anakuwepo saa ngapi, akasema jioni anafanya kazi wizara ya ujenzi.

Akamwambia jikaze mwanangu nitakuja kukufata ila sio leo wala kesho wewe jitahidi tu. Mtoto kalilia hataki kurudi kwa mama wa kambo anajigalagaza ikabidi tu amfanyie ukali sasa japo roho inamuuma mtoto wa darasa la 2 kufanyishwa mikazi yote ile. Roho ilimuuma na huyo Jacky akili za drasani hanaga, alikuwa anakuwa wa mwisho kila siku, kujitahidi tution nyingi na kumfatilia ndo kama kuna watoto 50 atakuwa wa 30 hivi. Sasa na hii mikazi si atakuwa wa mwisho tenaa. Bora kaka mtu kichwaa, mpaka walimu wanamsifia hatariii. Alivomaliza STD 7 akafaulu Ilbour boarding. Sasa huyu aliechukua akili za baba yake si balaaa.

Akarudi kwenye jumba lake tupu, anatandika sakafuni analala. Akili inamzunguka mwanae anadaiwa ada pale, Dimond na yule baba anavomjua yeye anaweza asimlipie wala nini. Na hiko kiakiba akimlipia si ndo ataadhirika sasa. Afanye nini kimlipe mjini hapa kazi hana, bwana hana, mume hana. Akawaza sijui akabebe unga tu au afanyaje. Akaenda magomeni hapo wanapobebesha watu unga. Kafika pale kaambiwa passport unayo? Akasema ndio maana alitengenezewa na bwana wake Dubai na kama bahati alienda nayo moshi akitegemea angerudi na ndege labda.

Akaangaliwa chura kubwaa, kajaa jaa akaonekana Afya ya kazi anayo. Akaulizwa kwenu wapi? Akasema Dodoma mjini. Akaulizwa umeelekezwa na nani? Akasema na Miriam aliefungwa china, sasa nilimtumia barua nataka kazi hii ndo akanielekeza kwa codes. Akaulizwa barua iko wapi? Akasema barua sina mume wangu kahamisha nyumba nzima nikiwa safarini na barua imo kabatini kaenda kuoa mke mwingine. Akaulizwa unakaa Magomeni ipi, nyumba ya nani? Akataja pale. Wakapiga simu, akasikia wanauliza eti hapo mtaani kwenu kuna mama ana churaa kubwa hivi, mumewe kahamisha nyumba akiwa safarini mmesikia kitu kama hiko au tego la polisi. Akamwambia alikuwa anakaa wapi? Akataja akasema ngoja nikapeleleze kwanza. Baadae huyo mpelelezi akapiga eeeh kweli kabisaa ndio, limetokea tukio hilo majuzi tuu hapa. Mwanamke mwenyewe anaitwa Elly msambwanda, imesikitisha. Akamjibu sawaa. Kaporowa hadi watoto 2, kaachwa na chupi aliovaa tu, sisi wanaume nyokooo. Hahahaaaaa! Wakacheka

Basi akamwambia mama habari yako ya kweli, hapa kazi umepata sasa bado jambo moja tu, kapime Alcers napata sanaa hasara ya unga wangu kuwapasukiawatu tumboni sababu ya alcers, kugharamia misiba, na unga kukamatwa nimeona kabla sijasajili punda lazima apime alcers. Ukikutwa na alcers usirudi mama hii kazi itakuwa ishakukataa, tafuta kazi ingine halali kama kufagia bara bara ama kuuza mama ntilie Maulana ni mwemaa tu atkutilia kheri huko utafanikiwa. Na kupima nenda hospital flani huyo Dr. wetu tunamuamini hawezi kutuchakachua. Akaenda kesho asubuhi kupima akakuta watu wengi tu wako foleni kupima hio Alcers akawa haelewi kama nao wako nae njia moja au wagonjwa wa kawaida maana hio hospital kubwa tu.

Akaingia kanywa jiuji lile. akapimwa Dr. akamwambia bibie mambo si mazuri una Alcers tena Peptic. Akamuandikia dawa na vipimo zaidi. Akamuuliza ulikuwa unakunywa pombe? Akasema sanaa, akamwambia acha mara moja utakufa vibaya sanaa. Maharage acha, vitu vya acid acha. Na ile kazi usijaribu, hata ukikataliwa Magomeni usije enda Kinondoni maana wale wana tamaa hawajali afya watakubebesha ila hutofika kokote. Hali yako ukicheza utakatwa utumbo na ukibeba yale mambo utawasili mzoga huko unakoenda. Dili ndo likawa lishakuwa dirisha.

Akarudi mtaana sasa akawa ana hustle ana hustle haviendi kodi inaisha mwezi huo hana pa kuishi wala pa kulala. Mwanae ndo haouse girl huko aliko akachokaa Akawa yupo yupo tu mjini anasaka kazi ya kufanya anapiga deiwaka kwa mama lishe, viwandani yeye kokote mradi apate riziki. Siku hio anatoka kupiza deiwaka ya ukibarua kwenye kiwanda cha sabuni huko anamkuta Jack nje na mabegi yake! Tobaaaaaaaa! Vipi baba kanileta kaniambia mjeuri mama wa kambo hanitaki ndo kanirudisha kwako. Akasikitika tu. Akafungua wakaingia ndani. Akamuuliza shule vipi akasema shule niliacha ada hamna baba akasema nikae nyumbani. Looooh!

Akaona sasa hili balaa peke yake anaweza kujihifadhi hata kwa bwana na mtoto tena mbona bwawa limeingia ruba na kodi inaisha, akiba alio nayo ndogo. Yeye kulala chini na mbu sio kesi ila kumlaza mtoto mdogo vile kwenye mimmbu ataathirika kisaikolojia. Akamuombea kwa jirani. Ila akakata shauri atafute chumba na kitanda, ndoo, jiko hivo yaani waishi maisha ya kueleweka maana mtoto yule inabidi aende shule, ale hawezi kuishi na kisela.

AKatafuta chumba hapo hapo magomeni, akanunua kitanda, godoro, neti kochi moja, jiko kabati kidogo kukawa nyumbani. Mwanae akampleka shule za kawaida hizi akamtafutia na tution za kutosha awe busy mpaka arudi usiku. Kazi za viwandani zikamshinda kutongozwa sanaa na kuombwa kipapa na ma foreman afu yeye ndo kabakia baba ndo mama kwa wanae na viwandani ukimwi mwingi sanaaa. Akaona atakuja kufa siku sio zake.

Akatafuta kazi ya kuuza duka tenaa kwa mdada, mshahara uleule 200,000 ila na comission afu hachoki anakaa tu ndo ikawa kazi yake. Hakosi kodi na kula. Mwanae wa kiume yuko form 1 shule ya serikali anatoa ada 70,000 hio haimshindi huyu wa kike mdogo darasa la 2 bado ana miaka kama 4 ya kujipanga kabla hajaingia sekondari. Akaja kujua kumbe yule mwanamke alieolewa na mumewe ana mitoto mi 3 aliozaa huko peke yake ndo mumewe anailea hio afu damu yake kaitelekeza shubhamit shenzy wahid. Akamlilia Mungu akasema Mungu mimi ni mkosefu maisha yangu yote nimekuwa mkosefu wala sikukutafuta ila wewe ni Mungu mwenye huruma huyu mwanaume na mwanamke kwa walichonifanyia na wanangu hawa malaika nakuja mbele zako naomba UMFILISIIIIIIII MPAKA ATEMBEE PEKU PEKU MJINI HAPA, AVAE NGUO ZENYE VIRAKA, SH 200 HII 200 IMPIGE CHENGA, AWE ANAKUNYWA MAJI BOMBANI KILA ATAKACHO GUSA KIGEUKE MAVI. Mimi sina hela ya kumwendea kwa mganga, maishani mwangu nimeloga sanaa, ila leo hii sina hata 100 ya kumpa mganga nimekuja kwao unitete. Kama Mungu kweli upo na umetuumba mi siombi utajiri, siombi makubwa hilo dogo tu ukinitendea nitakushukuru milele.

Siku anatoka dukani hana hili wala lile akaona gari imesimama akasema danga si ndo hili, kushushwa kioo mumewe yupo kwenye ki Rav 4. Hapo hapo akaanza kubleed ile chuki ya moyoniii. Akamsalimia Elly za siku kama hamna kilichotokea baina yao. Akataka asimjibu ila akaona asimpe faraja yule shubhamit kuona kamfira maisha sanaaaa. Akamjibu salama za kwako. Upo mwanaume anauliza. Akamwmabia nipo nanenepa tu ulijua nimekufaaa? Hamnaaa, watoto wanaendeleaje? Akamjibu wamekufa wote nimeshawazi una jingine? Sinanaaa. Wasalalimie waambie baba yao nawakumbuka sanaa. Elly akamjibu hawana baba wale, baba yao kesha kufa siku nzyingi wangekuwa na baba wasingeishi kwa kuhangaika kiasi hiko wanachohangaika sahivi. Mxiuuuuuuuuuuuuu! Akamuacha pale.

Moyoni akasema Mungu sijakata tamaa kabisaa, najua huyu shubhamit una mmudu vizuri tu. Sijakata tamaa. Mwenyewe ulisema Jeremia 32:27 Je wewe si Mungu wa wote wenye mwili, kuna jambo lolote usilo liweza? Mungu sijakata tamaa nataka huyu mtu umshughulikie kikamilifu kwa niaba yangu. Akawa siku yake isha haribika kabisaaa. Akarudi nyumbani mzitoo mzitooo.

Akaendelea na kazi ya duka huku na huku akapata buzi mume wa mtu. Mume wa mtu mwenyewe FREE P tu sanaa sanaa atakugea 20000 ukimkabaa korodani ukimkaba kweli kweli atakugea 50,000. Ikawa asha lost kabisaa yaani anaishi mla kala leo mla kesho kala nini hajui. Umeonaaa balaa hilo. Kesho yake haijui kabisaaaa. watoto wakawa wanaenda vizuri kimbembe kikafika Jacky alivofika la saba, anamjua hana akili ya kwenda special sansanaaa atapangwa za kata, na yeye hataki aende kata maana akili zake ndogo sanaa. Ada ya private hanaaa. Kichwa ikawa inamchemkaaa. Yule wa kiume akapasi kwenda Mzumbe 5 na 6. Na alikuwa akifunga shule anaenda Dodoma kwa bibi yake si alijenga nyumba kubwa tu kule. Maisha yalivobana wakapangisha kama vyumba vitatu ndo ada na amtumizi yake ya shule zingine zinamsaidia bibi.

Akiwa hana hili wala lile akapigiwa simu Baba Jacky kalost kabisaaa, yaani anatembelea Yebo yebo. Akasema Thanks God! Kweli Mungu hawai wala hachelewi. Hakuamini kirahisi sio kwa Rav 4 ile. Akajisemea mpaka nijionee kwa macho yangu. Maisha yakaendelea ikapita kama miezi mi 3. Akasikia kwa mtu mwingine Baba Jacky maisha yamempigaaa ni balaaa, ukimuona huwezi kumjuaaa. Kaishaaa, kachakaaa anapanga vitu chini kariakooo sokoni. Akajisema ngoja niende.

Akamuibukia huko huko. Kweli mara ya kwanza hakumjua kabisaaa, kamtafuta hajamuonaaa, akajua uongo akasema apange gari za ubungo aondoke, akasikia mtu anamuita Elly akageuka haraka maana ile sauti anaijua ndo kumuona mzazi mwenzie kachokaaa kweli kweli kapanga ndimu, pili pili viazi vile vitu vya kuokota okota. Akamsalimia za siku, baba Jacky hamuangalii usoni, salama watoto wanaendeleaje? Akamjibu wapo Mungu ndo baba yao mzazi siku hizi hajapungukiwa. Anajisemesha nilisikia Fredy yuko Mzumbe, asijenisahau mimi baba yake. Elly akasonya tu kimya kimya kwa hali alomkuta nayo hata kumchamba akaona huruma. Akamuuliza kwa hio siku hizi vipi Rav 4 umepaki wapi unigee lift jua kali. Akaona machozi yanamlenga mlenga akasema na badooo huo mwanzo tu moyoni tu lakini. Akamwambia haya mi naenda. Bila haya Baba Jacky akaita Elly kama una 2000 nisaidie nikale sijakula tangia jana tafadhali. Elly akasema moyoni na bado utaomba mpaka 200. Akamgea 500 mi na hio tu si unajua mi ndo baba ndo mama wa wale watoto. Akaondoka. Alitegemea atafurahi ila hata hakufurahi alisikitika tu kwa kweli.

Harry akawa karudi Bongo Daresalaam mazimaa akafungua maduka 2 moja Mbagara jingine Tandiaka. Nyumba yake ikawa imeisha kabisaaaa, na mwanae yupo A level kama Freddy ila anamsomesha St. Anthony. Maisha yamemkubali hela sh 2, 3 hazimpigi chenga. Lengo haswaa awe na maduka hata 4 Kariakoo, aende China million 100 zake yeye kufata mzigo. Hakutaka kurithika na vichenchi. Akataka awe level za Kebby Hotel. Akafight huku na huku Akaongeza duka Gongo la Mboto. Akawa kaaminika anapewa hata mizigo ya million 15 kariakoo na watu hata wa 5 tofauti auze alete hela, mali kauli.

Baadae akaanza kwenda China mwenyewe, akakata ile faida wanayogawana na Kariakoo. Hela ikamkubali hatariii. Akafungua duka kariakoo na yeye. Akawa anasafiri na kama million 40, akanunu na magari ma 2 moja kamnunulia mwanae yule wa A level, Benz akajinunulia mwenyewe. Akabadili jina maana alibatiziwa akajiita Happy sababu kawa mwenye furahaaa. Akawa na kazi ya kumpigia Elly kelel kuliko kuajiriwa bora hata achukue chupi za 300,000 apange chini apate hata 30,000 kwa siku, kwa mwezi ni 900,000. Elly akawa bado anajamba jamba. Akamwambia nitakukopesha hata million 5. Elly anamjua Happy vizri sanaa sio kwa ubaya ule, akajua akimzidi tu Happy ana roho ya kwanini sasa ataanza kumuhujumu mwenyewe.

Akiwa hana hili wala lile siku hio kavaa baibui na shungi basi tu alimua kutoka hivo, churaaa kubwaa inanensanesa akaona gari imemsimamia kuna kikaa kibayaaaa humo ndani. Mmmmmh! Akamsikiliza. Akamuomba namba akampa. Sasa siku hizi hanywi toka aambiwe ana peptic alcers. Wakakutana bar, ndo kumuona vizuri kumbe Fupi bwanaa. Fupi mweusiii, kijebaaa. Afu Elly mrefu ana churaa na miguu ya bia. Akasema kwa njaa nilionayo siangalii sura, mwanaume mzuri nataka kumnywa supu mie? La hashaaa! Akawa anamchekea akawa mkarimu wakaongea. Alivoondoka akamgea 100,000 ya tax mmmh! Akasema mbona kama namulewa.

Akambadilishia gia, akamuwekea gia no 5 sio kwa kilo ile. Baby bay hata kipapa hajampa akamuomba kodi, akaulizwa kwani bei gani? Akasema 600,000 wakati 360,000 akapewa yote. Mmmmmhhh! Akasema ina maana Mungu kaniona tena kwa mara ya pili nini. Akajisemea Bob nilifanya makosa kutokumzalia huyu nitamzalia mapacha akiendelea hivi sifanyi mistake. Huku na huku akampa kipapa sasa. Alidataa yule kaka. Sema wakiongozana ndo kituko kituko. Akamwambia ana watoto wa 2, yule kaka akamwambia ana mtoto 1. Kuna dada alitaka kumuoa akamshiti akaolewa na mtu mwingine, yeye anataka kumuoa. Atamsaidia wale watoto watakuwa wake. Mmmmmhhhh! Akasema kweli Mungu umeniona tena mja wako.

Kumbe yule kaka contractor na hela anayo ya kutosha sanaa, ana ghorofa lake huko Mbezi ana project kibao Mtwara. Akamkaribisha na wanae huko Mbezi Beach. Akaambiwa waje na nguo zao tu walizovaa hataki uchafu ndani kwakwe takataka zao zote za magomeni wagawe. Elly alishangatwa na nyoka sanaa akaona wanaume sio watu wa kuwaamini wala nini, hakugawa akampa dada mmoja alikuwa anakaa na dada yake humo humo akamwambia nilindie vikibuma narudi na kodi naendelea kutoa kama kawaida.

Akawa anaishi ghorofani dada anaona kama anaota mda mwingine ataamka ajikute magomeni. Ilimchukua mda kulizoea jumba lake. Na yule mtoto wa kule ana adabu vizuri tu anamuita mama, anamsikiliza. Hela zipo tu ndani anachukua. Na Fupi akampeleka Jacky Essacs anakosoma mwanae. Akawa anawaza hapa huyu fupi dawa kumzalia tu nisipozaa ya Mungu Mengi akifa tutatolewa baruu na wanangu kwenye ghorofa la watu. Akafanya mpango mpaka akanasa kibendi. Basi ndo akamvuruga fupi kabisaaa kabisaa. Aapewa na Prado awe anaendesha, na Bob alimfundisha ku drive. Akawa Elly, Elly kwelii anashinda Paradis Saloon. Ngozi lainiiiii. Kucha lacewig, nguo za 150,000 huwezi kumjua shogaa. Akawa kajibwetekaa anangoja kuzaa.

Siku Happy akaja akamchamba wima wima, Elly maisha ulioishi hapo kati hujakoma tuuu? Vitu vya watu sio riziki tafuta chako. Kwanini unakuwa mngese baridi? Sawa bwana anakuhudumia sanasana utakula utakunya baas. Kumzalia bwana sio suluhisho hata yule mgese mwingine moto shubhamiti si ulimzalia mitoto 2 ilikufikisha wapi hio mi trip 2 ya labor? Fanya akuwekezee uwe na vyako. Mwambie akutafutie fremu Kariakoo, na kukupa mtaji mi nitakuonesha machimbo ya China yote. Mi naenda ila ukiendkeza boloyanki kumbuka harusi nae huna umekaa suria kama mara ya kwanza umekaa suria mika 10 na zaidi akaja kuolewa mwenzio. Ujue huna akili wewe. Mi naenda ila kama umesahau ulipotoka unjifananisha na visichana vya mbezi vimetoka kwenye maghorofa vimeolewa kwenye maghorofa haya.

Maneno ya Happy yakawa yamemchoma sanaa, sanaa. Yule bwana kurudi tu Mtwara akamjambia shuzi la duka akitegemea upinzani mkali. Tofauti na alivowaza akasema sawa ni wazo zuri kuna leo na kesho na wewe japo hujasoma ni mwanamke mwenye akili sanaa tofauti na wanawake wengine ambao wangeridhika na kujibweteka pesa ipo ila wewe umewaza mbali na kutaka ujitahidi kwa upande wako twende mbali zaidii, au hata ikitokea sipo wanetu wasipate tabu. Utafaa kuwa mke wangu, nataka kutoa mahari kabisaa nikuoe kanisani. Harusi ikafungwa kanisani, na mtaji akapewa wa kutosha na ujanja ujanja wake mbona yupo mbali. Yani sahivi yeye na mumewe wanachuana kwa pesa. Siku ya harusi alilia machozi, na aliolewa baada tu ya kuzaa ile mimba. Na kaongeza wengine 2 so kwa mumewe ana wa 3.

Mpaka story hii inatoka Elly ametoka kimaisha, vibaya mnoo na Happy ane ametoka kimaisha vibaya mnoo. Wote anasomesha wale watoto wao wa kiume UK na Russia wanalipa CASH. Magari wanabadili kwa hamu tu, akiitamani anaagiza kwa hamu tu. Million 50 hizi kwao ni hela za kawaida sanaa. Beef lao wamelizika, wamesameheana kabisaa, na mume wa Elly aliwasisitiza wasome maana watoto watawaaibisha na China walikuwa wanapata tabu, wamesoma QT mpaka form 6. Wakajiunga na degree CBE, wakamaliza. Sasa hivi wanakula bata tu.

Wakaniambia tu DOGO hata usipotoka leo utatoka kesho Mungu yupo mradi tu usikate tamaa na usichoke kufight.


THE END.
 
Back
Top Bottom