Weekend story: Chura Ananesanesa! Jike Shupaza

lara 1

JF-Expert Member
Jun 10, 2012
15,700
29,161
Igweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Siku hizi nimekuwa demoted, so niko branch Kariakoo nachoma mahindi tu, jamaniiii. Sasa huku kariakoo kwenda kila siku ndo nikakutana na wanangu wenyewe wa kitambooo longtime ndo mashangingi ya kariakoo wana vitu vikali Hyundai za kufa mtu, Vogue ndo kukaa kitako sasa wakanipa Throw Back toka tulivoachana kitambo kile waliniacha niko STD 1. PATA HABARI KAMILI HUSTLES ZAO, MIZINGUO YA WANAUME, ULAJI TIGO WA MAISHA, MIHANGAIKO, MPAKA WAO KUTOKA NA KUWA WANAWAKE WENYE LIQUIDITY 50m KWENDA JUU AFU WOTE STD 7 ALIESOMA SANAAAA FORM 4. (HII NI INSPIRATION PIECE KWA WADADA KUWA UKIWAENDEKEZA WANAUME HUTOKI LEO WALA KESHO.


1997 STD 7.

Elvin nakupenda sanaa mpenzi wangu, kama vipi ukimaliza shule tu mi nikuoe tuanze maisha, sina vikubwa ila naweza kutunza mke na watoto. Kweli Freddy? Kweli niamini mimi navokwambia nakupenda kichiziiii. Nakuelewa sanaaa. Basi sawa nitawaambia wazazi wangu sitaki shule nataka kuolewa. Usifanye hivo Elvin isitoshe wewe bado mwanafunzi, cha kufanya subiri umalize shuleeee. Sawa Freddy. Sasa mi naenda. Chukua hii Elly itakusaidia. Akawa kamfinyia kwenye mkono. Kuifungua mbele kumbe 1000. Kipindi hiko chips 200 ilikuwa pesa ndefu.

Harriet we mjinga bi mkubwa kapika nini huko jikoni? Kapika Ugali na mlenda. Mmmmmmh! Sasa sikia wewe boya, mi nimetoka kwa Freddy kanigea buku hili kama vipi kanunua chips sahani 2 tuje tufanye yetu, mi mlenda haushuki kabisaaaa. Weeeeeeee! Unasema kweli Elly? Ndo manake. Poa leta.

Harriet alivoenda kwenye chipps akamuona Freddy, akaamua kumsabahi, Freddy mambo! Poa niaje? Fresh tu. Nilikuwa na Elly sasa hivi. Kanituma chips. Harrieth unapendezaaa ujue. Acha masihara yako Freddy. Mi sina churaaaa kama ya Elly si unajua mi Betinaaa. Sasa sikia Harrieth kesho fanya uje ghetto kwangu. Mmmmmmhhh! Harrieth akasita. We njooo. Freddy anamkolezaa.

Elly akijua je? Si unajua Dodoma ndogo hiii. Hawezi kujua kwani wewe ndo utamwambia? Hapanaaaa! Chukua hii akamgea 2000. Harrieth akanunua chips na mayai 2 akarudi nazo kwa Elly, wakawa chumbani ndo wanataka kuzila Hamad! Bi mkubwa kaingia. Nyie watoto malaya sijawahi kuona haya nani kawafunua na kuwanunulia chips yai? Hamna mama pua zako tu. Msinizeveze mwenyewe kijana wa jana, toeni viepe hivo tule hapa, hilo nguna takuja kula huyo mzee na wanae. Hahahaaaaaaaa! Wakacheka wote.

Tamu hizo wala si unafiki, kakwahonga nani hiziii? Yule fundi au kuna mwingine? Na mna moyo alivo mchafuuu na magrisi yake mie nisingemuwezaa. Hahahaaaaa! Wakachekaaa. Elly churaaa hio itakuponzaa, upande wa baba yako huo, shangazi zako wamefungasha vyura hatariiiiii, na vya kurithi vinazidi, binti mdogo kama wewe churaaa kubwaaa loooh! Ila mzaa chema nafaidi kama hivi. Hahahaaaaaaaaaa! Wakacheka wote tenaaa.

Kesho Harrieth akaenda kwa Freddy mchana, wakaanza uhusiano na Freddy kwa siri. Ujue nini Harieth, Elly mambo mengi sanaa hajatuliaa, ana wanaume wengi afu mi design nataka mke, so kama vipi mi nitakuoa wewe. Sawaaa! Harrieth aitikia mwanamke hana hayaa kuchukua mwanaume wa binamu yake. Ikawa ndo mahusiano kamili sasa.

We elly njoo kwanza wifi yangu. Akaenda shikamoni. Marahabaaaaaaa! Jamani maniona churaaaaa hio, mnaona msambwandaaa huooo wa wifi languu, huyu ndo Elly bwanaaa, kama mchinaaa kitu original akichamba hatakati! Hahahaaaaaaaaaa! Halooooooooooooo! Tunaona shogaa kafungasha si uongo. Sasa wifi sikia nasikia kaka yangu umalaya wake ana kimwanamke Betina bonge anakiingiza kwake we chunguza wifi yangu usiniamini mimi. Tena anakiingizaga mchanaa. Elly akachokaaaaaaa. Akayaweka akilini. Akaaga tu pale akaondoka.

Usiku akataka amwambe Harrieth akasiata akaamua mchana akachungulie ajua ataona nini. Mchana akawa kabana jirani.Akamuona Harrieth anaingia na Freddy kwake. Akachokaaa! Akakaaa pale hana nguvuuu. Masaa yakapita wakatoka, akawafata na kuwasalimu, Harrieth akakimbia anamjua Elly mgomvi sanaa. Freddy likamshuka tuuu. Elly akamwambia kuanzia leo endelea na Harrieth. Freddy anaona haya tu.

Kufika nyumbani saa 2 Harrieth hajaja anaogopa Elly atamkunguta na kumshushia kipigo heavy kwa kumchukulia bwanaa. Elly akajua alipo akamfata Harieth akakimbia tenaa. Akamkimbiza mpaka akampata, akamwambia sikia twende home, mda umeenda mdingi kastukaaa. Mi sina dhiki ya mabwanaa nina kazi mpya ya maana kuliko huyo Freddy we endelea nae tu. Mi nina HB yule mtoto wa mkuu wa kituo cha polisi ana hela chafuu Freddy pumbu tuuuu. Harrieth akawa haamini. wakarudi nyumbani kimyaaaa kama sio wao. Ikawa Harry ana deal na Freddy, Elly yuko na HB.

Ikafika mda wa mtihani wa darasa la saba, wakafanya wote mwezi wa 9 wakawa wako nyumbani. Usiku wamelala Elly akamwambia Harry mi nataka niende DSM na HB kuanza maisha mambo yangu yashaharibika mda huu tunavoongea. Yameharibika kivipi Elly. Acha tu Harry. Hivi juzi bi mkubwa alivomkimbia muha ulionaaa? Hahahaaaaaaaaa! Wakacheka wote. Nimesikia Elly ila sijaipata vizuri nisimulie. Elly akaanza kumsimulia.

Bwana hili toto la humu ndani Hamisi, bi mkubwa si alikopa vitenge vya wax kwa muha, akawa kamuona nyumba ya 2, akaja hapa kupiga biti anajificha tumsitiri. Akamchimba biti mpaka Hamisi ole wake aseme kama yupo ndani, Hamisi yupo sisemi mimi mama sisemi kweli tena.

Kweli muha kaja, akamuuliza mama, tukamjibu hayupo, hadi Hamisi yupo hayupooo mama hayupooo. Muha akasema sawa mi naenda akawa kaanza kuondoka hata hajafika mbali toto lile lisivo na akili si likaanza kupayuka.

Mama aya toka humo ndani muha kashaaondoka, tumemdangaya tiari haupooo, toka tu mama. Wote tukabakia kinywa wazi haaaaaaaaaaaa. Na uhakika muha alimsikia vizuri kabisaa sema akaamua tu kuendela na safari kumsitiri tu bi mkubwa ila alijua kama alijificha ndani kusudi. Hhahaaaaaaaaaaaaa! Wakacheka wote.

Elly mi Freddy anataka kuja kunitolea barua. Elly akastukaaa ila akajikaushaaa, hongeraa Harry hongeraaa, bora yako kimeeleweka. Asante. Elly hamu ya story ikamuisha akaamua alale jumlaaa.

Kesho yake Herry anatembea kwa kujivutaa, bi mkubwa akastukaaaa. Hakusema kitu, akamnongoneza Hamisi. Harry akawa kaaga anaenda dukani, bi mkubwa anamzuia anamwambia subiri kwanza. Kila akitaka kutoka bi mkubwa anampiga pini. Elly akamuona bibi yao anakuja akahisi tu sio dalili nzuri akakimbia. Akamuitia Hamisi kwenye kona, ulienda kumuita bibi wa nini? Mi hata sijui. Sasa sikia Hamis kanisikilizie wataongea nini, na kwanini anamzuia Happy kutoka. Hamisi akamwambia hio chips yai. Hahahaaa! Elly akamwambia poaaa.

Kutokeza tu kona, bibi akadakwa juu juu wakachonga. Kuja wakamdaka Harry. Bibi yuko huyu mbona anayo kubwaaa sanaaaa, mimba ni kubwa sanaaa. Mpaka kavimba miguuu, yaani hii haina mwezi atajifungua mtumeeeee. Mama akachoka Harry!!!!!!!!! We si yatima wewe nakulea hapa kwa msaada. Mmmmmh mbona umenivua nguo? Freddy kasema ataleta posaa. Mama akazidi kupandwa jazba, haya nenda huko kwa Freddy fanya ufanyalo hio posaa ailete leo leo, tokaaaaaaaaaaa, bila posa usirudi hapaaaaaa.

Hamisi akaenda kumpasha Elly yaliojiri, Elly akachoka mwili na roho. Akamwambia bibi akiondoka njoo uniite. Saa mbili usiku ndo mshenga kuja na hio posa, ndo Elly kurudi na yeye anakaa mita 100 na bibi. Huku na huku kwa machale, bibi akielekea mashariki, yeye mngaribiii. Ugeni kuondokaa, Elly hana hili wala lile bibi huyu hapaa. Akasikia tu na huyu tayari siku nyingi mbonaaaaaa! Mama Elly akakaa chiniii. Looooohhhh!

Baba mtu hakuongea neno akaingia ndani kimyaaa. Mama mtu akaanza kilio. Bibi akaaga akaondoka. Elly akaenda kwa HB kumwambia wamejua inakuwaje? HB akasema nitawatuma wazazi wangu waje waongee nao kesho haina shida tuko pamoja baby wangu.

ITAENDELEA KESHO SAA4
 
Lara unatuchosha, yaani page moja then mpaka kesho@ ts not fair kwakweli,huyu chura wa jangwani ni tabuuu. Ebu ongeza walau kurasa ya ziada
 
Najua tutacheza kibobmarley tu humu ndani. Natumaini akina Mangi this time utawaacha wapumuwee
 
Chaka la Kwanza

Ikawa ile posa imekubaliwa ya Harry. Mipango ya ndoa ndo ianze, huku na huku mawifi wakaweka ngumu haiwezekani akaolewa yule Harry sababu mwanaume ashatembea na dada mtu na kila mtu anajua itakuwa mambo ya aibu na kujivua nguo mtaani. Wakagoma katu katu Harry asiolewe ila azae tu na watamhudumia huko huko kwao.

Harry akajifungua mtoto wa kiume ikawa yupo yupo analea sasa, kakondaa, kapauka kaishaaaa. Elly ikawa yule baba mkwe polisi kakubali sawa mwanae kamharibia maisha Elly basi waishi wote maana mwanaume kamaliza form 4 kafeli baba yake kampa duka ndo anauza uza hilo duka. Wakalipa mahari na fine zote Elly akahamia kwa baba watoto wake. Nae akapishana mwezi tu na Harry, nae Elly akazaa mtoto wa kiume pia. Ila akawa ndo yupo kwa mumewe sasa baba Franky.

Matokeo yakatoka Harry kafaulu shule ya kata, na Elly nae kapasi. Ila Elly mume akagoma asiendelee na shule, maadam Harry yuko tu nyumbani bora aende shule mtoto mama Elly atamlelea. Akaenda kureport shule na kuanza shule rasmi. Shule nako muonja asali haonji mara moja, akaendeleza tabia yake ya mabwanaaa mwanzo mwisho, ila akawa habebi mimba ngooo. Kmaliza form 4 kaambulia 0. Akarudi maskani akawa kalost upyaaa.

Elly baba mkwe akafariki, mafao wakagawana maana alikuwa na watoto 6 huyo baba mkwe wake na mke wake. Hela kugawana gawana haikuwa nyingi. Duka likaanza kufifa kufifa na Elly baba mkwe anafariki ana mtoto mwingine wa mwaka mmoja. Duka likafa kabisaaa. Wakawa wamelost wote mama mkwe na watoto kila mtu. Wakakubaliana wauze nyumba yao Area C. wagawane kila kitu. Nyumba ikawkwa mnadani.

Harry katika kutafuta maisha akaja Dsm kwa dada yake, huko mbagara rangi3 mbele,akawa kalost. Akapata kazi duka la mama mmoja anaitwa mama Naomi, huyo mama Naomi mumewe muuza unga. Akawa anauza asipouza mshahara pale pale hela si ipo. Imejaaa ya Unga. Yule boss wake akamuonesha chochoro zote za Kariakoo, mpaka wale wanaokatia mizigo majumbani, sebuleni anajua hizo chobingooo. Akawa biashara ya nguo kaijua nje ndani.

Ikatokea matatizo, yule mumewe alirudi na Unga akafariki kwenye gari, ametoka kumpokea kamfia kwenye gari. Sasa akajua ana mzigo tumboni kwa ukauzu yule mama Naomi akaenda Dispensary kala dili na Dr. wakampasua wakatoa madawa akayauza. Akafanya kuwapa taarifa ndugu J kafariki anazikwa kesho asubuhi. Sasa mwenye unga wake kumbe mda wote anamtafuta J, hajuwi yuko wapi. Akchoma polisi. Siku ya mazishi wakaja kumshika mkewe kwa kesi ya mauaji, kukagua maiti imepasuliwa. Afu hajatoa taarifa polisi. Akawekwa ndani na Dr ndani.

Harry akawa kalost upyaaa, hana hili wala lile, duka limefungwa anakaa tu kwa dada yake na dada yake kamchoka. Siku mama wa jirani akamwambia wewe Harry si umesoma soma kidogo, mdogo wangu kaolewa na mwarabu anatafuta msichana wa dukani huko Sinza utaweza. Akasema nitaweza mama, akapelekwa kwa mwarabu wakaelewana akaambiwa aanze kazi.Akaanza kutoka mbagara mpaka Sinza anapanda gari 3. Anatoka usiku anarudi usiku.

Maneno kwa dada yakawa mengi sanaa, hela yote dada mtu anataka alishe familia yoteee asibakiwe hata na kumi. Na mtoto akawa kamleta hapo kwa dada yake, basi ndo kosaaa. Siku hio karudi jirani akamwambia usimuachie mtoto dada yako, anambabuaaa kama mtu mzimaa. Anamkungutaaaa utasema mtu mzimaa bora upange zako huyu dada yako sio mtu. Akawa roho imemuuma ila sasa tasemaje maana ndo anapotegemeaaa. Akatafuta bwana wa BOT anamuhonga 20, 30 anaziweka, akipiga dili za chajuu ofisini anaweka akiba mpaka ikatosha kodi. Akahama akawa kapanga kwake Mbagara ila ndo maisha ya kuunga unga.

Mtoto anamsomesha shule za serikali primary ila ndo akitoka shule anakuta kiporo, anakula anashinda tu na majirani mpaka yeye usiku ndo arudi, amuogeshe, apike, akague madaftari usiku huo huo basi akilala hoi bin taaban hana hamu. Siku ya kulala na BOT ndo atume hela kwa jirani elfu 10, walale na mwanae maana anaogopa kulala mwenyewe. Bila 10,000 huyo bibi jirani yake hakubali kulala na mtoto wa mtu. Maisha yakawa magumu kweli kweli.

Elly na mumewe baada ya kuuza nyumba wakahamia Magomeni, ule mgao wake aliopewa wa hela nyumba iliouzwa akawa kafungua ofisi ya kuuza matofali huko mbezi. Biashara ikawa nzuri kweli watoto akawaendelezea international maana babu yao alimuanziha yule wa kwanza english medium kabla hajafariki, alivofariki bibi mtu akapigana akamuendeleza, na walivohamia magomeni akawa kamuendelezea huko huko, yule wa pili wa kike akawa kama ana miaka 3. Sasa mwanaume mchoyooo hampi hata 10, ananunua mpaka chumvi ndani, mboga anaambiwa chukua nitalipa.

Elly akawa kapauka kweli kweli nguo za mwisho ndo alizokuwa anapewa vihelahela na baba mkwe. Ikawa akionge kidogo mwanaume anamwambia kama umechoka ndoa ondokaaa. Anavumiliaa. Ila watoto akawa anawapa matunzo yoteee na yule mdogo alivofikisha miaka mi 5, akawa kamuanzisha Dimond, ada analipa bilia kushurutishwaa. Watoto nguo mpaka wanachoka asipitishe mtu akichukua wanalipiwa, akichukua yeye atakoma kudaiwaa. Na hapa mjini mgeni hana ujanja, anashinda magomeni akakondaaa. Psii anayopata ya wauza genge na madukaa. Chura yoote ikaporomokaaa.

Siku akafatwa na Harry kuna kazi kule Sinza ya kuuza duka, kaongea na mwarabu kuhusu mtoto anateseka mwarabu kakubali Harry amlete mwenzie wawe wawili yeye Harry anaingia saa 1 anatoka saa 8, Elly anaingia saa 8 anatoka saa 4 usiku. Ikawa Harry analipwa 200,000 alafu Elly analipwa 120,000. Mume wa Elly akakubali kama asubuhi anafanya kazi zote na watoto wote wanaenda shule sio kesi akienda kazini na yeye kujitafutia chochote kitu.

Elly akaanza kazi kwa mwarabu. Mwarabu akawakabidhi fremu lina midoli kila kitu na mtaji wa million 4 ya kuzungusha, waende kariakoo kununua nguo wanaziweka Sinza wanauza, ijumaa wanapiga hesabu nguo walinunu bei gani na wameuza bei gani, faida anachukua mtaji unabakia wanazungusha.

Harry machimbo yote anayajua alioneshwa na boss wake wa kwanza aliefungwa, ila Harry ujanja hanaa wa kujumlisha na kutoa kama zoba tu. Ila Elly wiki ya kwanza tu akamwambia wapandishe bei zile nguo ya kuuzia na mwarabu wanamuandikia pungufu. Wakaanza kupiga hel nzuri tu. Wakitoka wanagawana 30, 30 mpaka 50 kila mtu. Wakaanza kufanya maisha ya maana sasa.

Jioni Harry anatoka na BOT, Elly anaenda kwa mumewe. Hela hela akapata hle ya kunyoa nyusi, kununua sabuni cream, nguo za maana, na kuridhika tu churaaaa tu huyoooo akarudi. Msambwanda ukarudi upyaaa. Watu Elly anatumia dawa za kichina anatumia dawa za Kichina. Kumbe maisha tu yaliyo mporomoa churaaa yote. Akaanza kungaaa anashonea lace wig ndo zietokaa utamjua kama anauza duka?

Siku hio kasimama bar ananunua chips, kaagiza chips yai, akasikia umelipiwa dada na Bob Mapesa yule mchaga pale nyumaaa. Akamkonyeza muuza chips nifungie na kuku mzimaaa. Muuza chipa akasema poa. Elly hajivungi michezo hio anaijua kitambo kusikia Bob Mapesaa akajua ile bahatiiii ya mtende kuota jangwani akamuuliza yuko wapi nimshukuru mimi. Akaoneshwa.

Tumeeeeeeeeee! Pipa la mtu! Bongeeeeeee, bonge haswaaaaaa! Katuna kama kimbofa kwenye hiko kiti, mishavu hiooo. Roho ikamfanya paaaaaaaaah! Akakumbuka anaitwa Bob Mapesa na bar hupewi heshima bure bure akajikaza akamfata. Mambo bobu! Anamlegezea macho, nashukuru kwa ofa. Sasa mchaga yule sound hanaa. Anacheka cheka. Elly hajalaza damu, akamwambia chukua basi namba yangu tutaongea. Mangi fasta fasta kaiandika nambaaa hio. Elly akaaga kaondoka huku nyuma chura anaensa nesa hatariiiiiiiiiii. Kumchanganya tu Bobu mapesaaa.

Karudi wakajisosmola yule kuku mzimaa na Harry, Harry anauliza huyu kuku vipi, anaambiwa we kula tu, usiulize sanaa asije kukukaba bule. Wamekula tani yako. Kila saa Elly anaangalia simu kama bob kapiga au vipi kimyaaaaa. Akaanza kuingiwa na wasi wai asije mpigia usiku akiwa na mumewe ikawa sasa dili likageuka dilisha. Mpaka saa nne anafunga Bob hajamtafuta.

CHEZA KIBOBMARLEY

ITAENDELEA SAA 4 USIKU.
 
CHEZA KIBOB MARLEY,

Akafunga duka siku hio Bob hajampigia wala nini. Akaenda kwake akili yote iko kwenye simu siku hio. Mpaka wanalala hamna simu ya bob wala bobmarley. Akasonya tu kimya kimya moyoni akasema bob mapesa hunijui wewe, kama unadhani utaniponyoka kirahisi hivo unachezaaa. Kesho nadeal na wewe kisawasawa.

Kesho kawahi kabla ya mda wake wa kazini, cha kwanza akaenda bar, kuagiza supu, hakumkuta bob mapesaa. Akamuachia ujumbe mtu wa jikoni kuwa huyo mangi akijaaa mda wowote mwambie FBI Elly msambwanda anamsaka kona zote kwa gharama zozote. Alijua kuwa akimpa huo ujumbe bar maid hautofika kabisaaa. Kuonesha yupo serious akamuchia mtu wa jikoni 10,000 kama hela ya stamp kufikisha ujumbe na kumtia mshawasha kama bado hajamtia bob mkononi anamgea hio akimuweka kwa bob je.

Kupewa mwekundu mtu wa jikoni kajimiminaaa hatariii. Pale kwa Boba mbona hujapoteaaaa. Bob ana hizi semitrela za mafuta kama 7 hiviii, bob ana helaaa, bob utamwambia nini yule mchagaaa. Yaani ana helaaa ni ana helaaaa mpaka inatia kinyaaa. Unafikiri dada wa mie hutojutia kuwa na Bob, huu ujumbe umefika Posta na Bob ataupataaa, mie tenaaaa, kila kitu niachie mieeeeeeeeeeeee. Elly akamwambia nakuaminiiii, usiniangusheee.

Bob kuja mtu wa jikoni akamuwahi Bob yule dada mwenye msambwanda kaja kukuuliziaa hapa asubuhi. Bob akastukaa akafurahiii yule churaaa! Weeee! Njoo unisimulie uje na kreti ya bia kabisaa tunakunywaa huku unanipa hio habari. Mchoma nyama akatulia na Bob akaanza kubonga nae Kimachame ngikwambia ukweli kabisaa, akachanganyia kimachame huko ndani Bob akawa na e anatia kimachame juu. Mwisho Bob akamwambia wanawake wale wana wanaume wengi churaaa zile kila mtu anazipenda afu wasumbufuu sanaa, mimi wanawake wanananinyanyasa sanaa sanaa kisa tu huu mwili. Akatia na kichaga kuonesha machungu aliyo nayo. Mchoma nyama anatia kichaga humo kumshauri huyu bwanaa yuko serious niamini kaka ako wa Machame siwezi kukuweka sehemu mbaya. Maneno mia. Akakubali.

Elly kakaa dukani simu kaitia ziwani kusudi isije kuita asisikie akamkosa Bob ikaingia sms akaifunua fastaa akakuta namba mpya. Akajua tu Bob hakukumbuka hata kuuliza nani mwenzangu akakimbilia tu kujibu poa Bob niaje. Bob akacheka tu akajua huyu tunaweza kuwezana maana ananirahisishia kazi mambo za mimi jana tulikutana bar yakawa yamerukwa. Kuchat kuchat akamuuliza umekula? Elly akajibu sijala! Bob akarusha 100,000. Elly akasema aminaaa, yaani Bob utajuta kunifahamuuuu. Sijakuonjesha churaa umechukua room nikikupa chura si ndo uta blow mapigo.

Baada ya ile laki, Elly akaanza kumchokoza Bob nina hamu kweli si unajua sina mtu mimi. Bob akadataa akamuuliza yule mchoma nyama nimjibu nini. Mchoma nyama akamwambia haya mambo ya mjini kaka mwambie umechukia chumba hapo Lion aje. Bob akatoka akenda kuchukua chumba akamwambia niko Lion kama vipi njoo.

Elly akaenda mtoto wa mjini hajivungiii kampa Bob mambo mazitooo, hakuwa na mda wa kumsimanga bob umezidi unene sijui, punguza uzito sijui nini. Elly anajituma mwanzo mwishooo Hataki utani na kazi yake ya zamani ya kudangaaa. Kampeleka peleka bob putaaa. Akaoga akamwambia mi narudi kazini, Bob akamwambia subiriii akampa laki 3. Elly moyoni akasema hapasasa tutaenda sawaaa. Akapiga goti mpaka chini kuzipokeaaa zile hela. Chezea mgogo wewe. Bob akazidi kudataa.

Elly karudi kazini kama sio yeye alietoka kuuza mechi mda si mrefu. Akaenda kuitoa na ile laki akamuonesha Harry ana 400,000 kazitoa kwa Bob mapesaa. Harry kijicho kikamuingiaa akawa anaona Elly atatoka kimaisha mda si mda. Akaenda kwake mume hakistuka wala nini.

Asubuhi kakaa dukani hana hili wala lile bob huyu hapaa, kalewa tila lilaa. Anamwambia Elly leo nina helaaa maku la maakooooo nina helaaaaa! Nimesema mimi ndo Bob bwanaaaa, Raisi wa Sinzaaa. Nina helaaaaaa. Makunina zenu wote nina helaaaa. Akachukua kirambo kwenye gari lake kimejaa wekundu wa msimbazi. Harry akasema hii kibokooo. Ni hatariiii. Akamwambia Elly umekulaaa? Elly akamwambia sijala boss wangu. Mimi sio boss wako mimi bwana wakoo, unataka shinganpi ya kula? Elly akamwambia nihukumu wewe. Bob akaingizamkono kwenye rambo akatoa kibundaa hii itakutoshaa mama, wewe ndo mke wa bobu bwanaa First lady wa Sinza. Akampa. Akazitia kwenye mkoba. Haya mi naenda garage kuna gari ina matatizooo.

Elly akamwambia subiri kwanza nikusindikize, kapanda kwenye gari anampa bobu mateee. Bob ana dataaa, akaanza kumchezea dude lake sasa. Bob akasemaje au twende hapo Lion siendi garage wala nini. Elly akamwambia ndo manake. Kwenda lion wamefanya yao, Elly akahakikisha kamchosha kweli kweli, bob kalaa foo foo Elly akachomoa million kwenye lile rambo akajua levi lile haliwezi kukumbuka hela alizipotezea wapi alivo bwaxxx. Akamuaga tu Bob mi naondokaaa. Boba akamwambi chukua nauli unayotaka kwenye rambo hio. Elly hakuchukua tenaa akamwambia za asubuhi zinatoshaa.

Akarudi kazini na janaba lake hakuna hata mteja alie ingia siku hio. Ikaingia sms ya amma yake kumlili shida, akamtumia million. Mama akamwambia nakuaminia Elly wewe kubwa lao Dar imeanza kukubali mwanangu. Nilijua tu kwa IQ yako huwezi kulost jijini hapo. Jioni akafunga akampelekea mumewe janaba la Bob.

Ikawa Bob kesho hakujua kama kaibiwa million au vipi, akawa kwa Elly hana ujanja akijitia nunda tu anaongezewa dozi ya majamboz. Na elly anajua kula na kipofuu, akiwa mbele za watu ole wako umsogelee Bob atakupasua na chupaa. Na ile chura watu wana,sifia bob huyu mwanamke umemtoa wapi? Msharii ila ana chura hatariii. Wanawake marufuku kumsogelea Bob.

Bob akafika bei bwana, akamwambia Elly nataka kukuoa. Nataka nije kwenu kutoa posa. Tobaaaaaaaaaa!
 
Back
Top Bottom