RUKA KICHURA CHURA.
Elly akawa anamzevezaaa, wakipanga tarehe ya kwenda Dodoma kutoa posa ikikaribia anazusha msiba, anachukua hela kwa Bobu anajificha hapa hapa mjini anazila tu. Akishamwambia ana msiba anamwambia fundi viatu ukiona gari ya yule mangi nipigie fastaa. Basi anampigia fasta anaingia stoo, Bob anaongea na Harry hajarudi huyu msibani, anamwambia hajarudiii. Kukwepa wambea anakuwa anakuja na kuondoka na baibui kanyonga Ninja.
Huku mumewe nae akawa kapata mchepuko akaona sawa tu sababu yeye ndo anazidi kuwa free. Hata akirudi saa 8 hamuulizi kitu kabisaa wakati zamani thubutu yakeee, kuna siku alirudi saa 8 akawa anamtengea chakula kuwaza na kuwazua kwanini anafanyiwa vile akaitia mboga sukari, mboga yenyewe kisamvu. Hahahahaaaa! Yani alikuwa mbabeee, akichelewa kurudi asubuhi anamuwekea chumvi kwenye chai ya maziwa yaani hapatoshi. Ila baada ya kukolezwa na Bobu atajijua mwenyewee.
Basi mumewe anamuuliza mbona siku hizi huna cheche, anamwambia uzee huu, nishastaafu wewe hangaika ila jua mafao ya malaya ukimwi. Akifikiriwa sanaaa zaidi atapata kiinua mgongo cha Kisonono na NSSF ya Kaswende. Hahahaaaa! Mmmmmmh mumewe akaona du bora alivochoka akamuchia uhuru wa kijiachia anavotaka yeye. Ikawa mume anarudi saa 8 saa 9 yeye akichelewa sanaa saa 4 usiku. Ila majukumu yake kama mama aliyakava kama kawaida.
Lazima akagua home work japo haelewi manake yeye darasa la 7 ila lazima kagua anaangali pata na kosa, akikuta kosa kunachimbika. Au ngapi juu ya ngapi, au anachimba mkwara mbona hamna eksellent humu unacheza sanaaa wewe. Asubuhi ahakikiseh nguo zime nyooshwa, wamekunywa chai ya maziwa fresh na kitafuno heavy. Na wana lunch box za maana za kwenda nazo. Msichana wa kazi anakula nae sahani moja kuhakikisha hazingui kwenye malezi.
Mume akaanza kupunguza hela kidogo kidogo, sasa yeye si ana hela akawa hapigizani nae kelele kama zamani, mtoto akirudishwa ada anamuuliza kwani sh ngapi kalipe ya mwaka mzima. Mwenye nyumba akiuliza kodi anamuuliza kwani sh ngapi anamgea yote. Kidogo kidogo hela ya matumizi akawa haweki anakuta vyuku vimekolea nazi. Na anakwambia sitaki kujibana, sitaki wanangu washindwe kula vizuri kwa ungese wa baba yao, chakula nazi 3, vyuku, nyama , samaki kama kawaida, nguo wanae waliweka heshima mtaani. Zamani kuna siku mume hakuacha hela ya chakula akapika na wanae wakala hotpot akalijaza mchanga, akaliweka mezani, akalala. Asubuhi akakuta 10,000 akasema shenzy wahid we kumbe una akili he leo ningekujazia kokoto. Hahhaaaaa! Ikawa inapita hata wiki 2 hajapewa hela.
Akawa anakula sahani moja na Bob hatriii, bobu hatikisikii kamuweka kiganjani. Harry akaanza kuona wivu manake yeye BOT hampi hela yoyote ya maana zadi ya kumpiga boloyanki basi, cha zaidi atamgea elfu kumi au ishirini. Akimlilia kodi sound tupu. Akimlilia ada anapewa maneno tu. Akimuangalia Elly anakoga mapesa kwa Bob Mapesaa. Akikaa asubuhi jana katumikaaa kaambulia elfu 20, anakuja Bob Mapesa kalewaa ana aanza leo nina helaaaa, makunina zenu wooote, Elly leo nina helaaaa, mimi nani nakuuliza, mimi nani? Elly anamwambia bwana wangu. Anamrushia kibundaa kimetunaaa, kama si laki 5 ujue millioni. Anatukanaaa anaondoka. Harry roho yamtokaa kwani Elly ana K gani na yeye ana K gani mpaka apauke namna hio.
Kile kijicho anachomuonea Harry akawaza mpaka nae atumie dawa za kichina nini kuongeza churaa. Maana Elly alichomzidi cha maana sana sana ni hio churaa basi. Akawa roho inamuuma zile hela wanazo mchakachua mwarabu wakigawana pasu kwa pasu wakati Bob ashamgea zigine, akatamani Elly aingiwe utu amwambie yeye achukue zote. Na kibaya Elly ana mume juu. Wanae wanasoma International School wote. Yeye mwanae anasoma Kayumba, mtoto akitoka asubuhi akirudi anawaachia watu tu hajui anaishi vipi vipi mpaka hio jioni akirudi yeye. Anakula viporo. Hela hapati roho ikawa inamuuma sanaa. Maana watoto wa Elly wanarudi saa 11 jioni atleast wake saa 7 anashinda uswahilini hajui hata anakutwa na yapi.
Akaanza kuwa ananuna tu kazini bila sababu, Bob akileta vyuku haliii roho mbaya vyuku hata vishukiii. Anajinunisha kila mda. Baadae kijiba kilivo zidi akamfata mwarabu akwambia mimi naomba nibaki peke yangu dukani muachishe Elly nitakaa mwenyewe kama zamani. Mwarabau akamwambia Harry utanidanganya wewe unakaa mbagara rangi 3, una mtoto, hili duka linatakiwa kufungulliwa saa 2 na kufungwa saa 4 usiku, kukaa mda wote huo dukani utanidanganya. Huwezi. Tutamtoa Elly afu wewe utaanza kunipa visingizo na sababu kwanini duka halifunguliwi na kufungwa mda naotaka. Wote si nawalipa mimi mshahara tatizo lako nini? Elly simuondoi itabdi tu mkae woteee.
Harry akawa kakubali kishingo upande, sasa mwarabu muislamu safi hataki unafiki akamuita Elly akamwambia yote na kumwambia kama mme hitilafiana mahali muyasawazishe sie wote bin adam, asije tangulia mmoja wenu mbele za haki bila kuyasawazisha baina yenu isitoshe nyie ndugu. Elly akamwambia sawa mkuu nitayasawazisha. Ikawa Harry bado ananuna nuna kama kawaida yake. akifikiria Elly kajenga nyumba kubwa tu nzuri huko Dodoma roho inazid kumtokaaa.
Akaanz akumwambia Elly nataka kuacha kazi mwenzio. Elly anamuuliza kwanini anajibu basi tu nimeamua mazingira ya kazi magumu kama anamfumba fumba flani Elly. Elly akakumbuka wema wake wa mwanzo alivokuwa kalost akamuonea imani na kumleta hapo dukani, akawaza itakuwa si vizuri aache kazi umri huo arudi kwa dada yake. Akaamua bora aache yeye maadam kamchoka na yeye mambo yake sio mabaya sana sio kesi na si yupo na Bob. Akawa kaongea na Bob kwa kina kachoka kazi Bob amfungulie duka afu ndo waoane kama vipi baada ya hilo duka. Jinsi Bob alivokuwa anamuhitaji kwa ndoa akakubali, siku hio hio dalali akapewa hio kazi na Bob.
Duka likapatikana magomeni, kwa 400,000 kwa mwezi kddi. Bobu akalipia mwaka mzima, akamjazia na mzigooo wa nguo mpaka juu. Likawa duka la maana. Elly akaacha kazi kwa mwarabu ikawa ana duka lake na kudeal na Bob tu. Simu anayo wasiliana na bob inalala chumba cha HG. Mchana ndo wana malizana akamdanganya Bob anaishi na mjomba wake mlokoleee wa kwa kakobe. Bob hata asisogee jirani na hapo kwao itakuwa ishu. Wao wameokokaaa. Jumapili akiwa na mumewe anamwambia Bob nipo kanisani. Na usiku anamtafuta yeye Elly kutegemeana na mazingira yalivokaa ulokole huooo. Bob akawa ashazoea anamtani wewe geti kali sanaa, maadamu umaluuni wanamaliza mchana sio kesi sanaa.
Harry dukani baada ya Elly kuacha akaletewa mtu ndugu yake mwarabu hapati hata 100. Huyo dada anamwita Mwarabu Ammy yake, sh 10 hapati. Maisha yakawa magumu si kitoto. Akiangalia Elly ana mduka wake roho inamtokaa kweli kweli. Akaamua kumsaka Bob akamuuzia CD yote kuwa Elly ana mume, na watoto wa 2, mda wote wako wote kaolewaa. Akamwambia mpaka anapoishi. Bob akadataaaaaa. Hakumuuliza Elly.
Siku hio kapita dukani wakaongea akaaga kama sio yeye. Akawasha gari kaondoka. Kumbe kabana mbele. Akamuona Elly anatoka anachukua bajaji kafunga duka vizuri akaifata bajaji mpaka magomeni anakoaa Elly na mumewe. Akapaki gari sehemu hamna hata ulinzi akaanga kutembea kumfata Elly ana hema na ubonge wake kama nyumbaaa. Alivokaribia kwake wanae wakaja kumu waoh! Mamamaaaaaaaa! Yule wa kiume akampokea mfuko. Bob anachungulia hapo.
Yakamshinda akaita Ellly! Kumbe umeolewaaa na una watoto? Kumbe una bwanaaa? Kwaini umenidanganya mda wote huu? Bob anafoka mpaka kichaga humo ndani, anamvutaa kabisaa. Elly akawaambia wanae nendeni kwa mpemba mkale chips nakuja huko kulipa. Walivoondoka anamtuliza bob maana watu washaanza kujaa s uswahilini. Akajikuta tu anamkaribisha ndnai ili afunge mlango hahaahaaaaaaaa! Chezea kufumaniwa unamkaribisha hawara ndani. Bob akagoma. Pale pale nje Bob akawa anataka kulianzisha. Watu wakawa wanamshangaa Bob alivo bonge kuliko hata ya anacokisema. Ikawa tukio kubwaaa.
ITAENDELEA.