Unaweza dtae na mtu miaka 10 hata 20 ukajihakikishia unamjua nje ndani my friend you dont know shit! Mpe karatasi lile kwamba nao its official uoneshwe kazi! Ndo maana ma billionea kama Oprah hawaolewi! Wala matajiri kama Ruge hawaoi! Sababu washajua huu mchezo usiuchezeee! Anza kuishi na mtu jumla jumla ndo utaelewa kwanini wazazi na ndugu walicheza sanaaaa siku ya harusi yake! Heheheeeee!
Ukiacha mimi kumpenda nani na kutokumpenda nani, mwanamke aliekuwa ananipenda kweli kweli ni Jane! Tunarudi pale pale kwa Hans unaminya minya nyanya unaishia kuokota biringanya lako moja na kuliweka ndani! Kwa kuangalia mambo Jane ndo alinipambania mpaka mwisho! Na ingekuwa ni fair competition she deserved to be my wife and spend the rest of her life with me! She worked so hard for that position!
Umuhimu wa mtu unauona during darkest hours! Maana kesi ilikuja kukaa vibaya sanaa wakati ndugu wa marehemu ni mjomba wake kabisaa alivoteuliwa kuwa moja ya majaji wa juu kabisaa! Now it became a family affair! It became personal! No amount of money could solve the issue! Alienda mpaka kwa raisi kujilalamisha! Na unaambiwa ni swaiba wake mkubwa walisoma wote kidato kimoja!
Jane alikiqa na hela sio ya nchi hii! Tukaka na maboss wa magereza wakasema hii ishu ngumu sanaa! Ni haiwezekani tunaweza sema sio riziki! Jane akawa anapanda dau anaongea kwa herufi kubwa! Pesa ikamiminwa ya kutosha mpaka ikawa dhambi wakaamua penalty! Wakasema huyu acha ahukumiwe maisha afu Judge atapoa jazba zake afu sisi tutampiga mtungo huku ndani! Kila mtu anakula mahala pake!
Nikahukumiwa maisha! Wazazi wangu walikomaa wa appeal! Nikawaambia cheni hizo mambo! Acheni kabisaaa! Hwakukubali!! Wakaniambia appeal time ikifika lazima wa appeal! Nikiwa ndani tukaa kikao na wakubwa wakasema judge bado anahakikisha sichomolewi humo ndani! Kama chezo likichezwa lazima liwe la akili kubwa! Lazima litumie akili kubwa! Kusiwe na makosa! Lasivo judge atatumalizaaaa!
Jane akaambiwa atafute mwili fresh wa marehemu alikufa siku hio hio alingane na mimj kwa urefu na mwili! Akipata tu huo mwili aseme! Jane MAFIA akaweka oda mochwari zote ananunua mwili huo kwa bei yoyote atayoropoka mtu wa mochwari! Wakawa wanamuitia miili ila yote ina kasoro! Sometimes urefu umepungua kidogo, sometimes umezidi! Sometimes mnenen sana! Sometimes mwemvamba sanaa! Ikawa inachelewa! Ananiambia im getting impatient kama vipi nimue mtu tu nijue moja! Alitafuta snaaa mtu kama mimi wa kumpoteza ikawa kama mwili tu hakuna perfet match!
Siku ya siku mida kama saa 3 asubuhi nikaitwa na kuambiwa nikasafishe kwenye mitambo! Huo mtambo una shoti balaaa! Nikawaza au Jane kabadili mawazo anataka kuniua nini? Ukute ashapata vwana mwingine! Nikaenda kuwaambia wafungwa mbona kama wanataka kuniua jamani wazi wazi! Naambiwa nikasafishe mtambo wakati una shoti balaa! Nikagoma! Nilipigwa kipigo cha mbwa mwizi! Wale wafungwa wakasema wewe nenda tu! Kikitokea kitu hapa hapata lalika!
Nikatubu kabisaaa! Nikaenda! Nimefika kule nikapigwa pigo moja takatifu! Nakuja kuzonfuka niko hotelini! Na Jane! Akaniambia hapa ushakufa kwa shoti za umeme! Nilipata mwili ukapigigwa shoti za umeme hatariii! Umebakia mweusiiiiii and disfigured! Wadungwa walileta tifu la karne! Ikabidi mwili uzikwe jana jna kwa oda ya mkuu wa magereza! Jaji alitaka kupitisha DNA! Mkuu wa magereza akagoma japo mgao hakumfikia ila revolt ya wafungwa ndo ilimchachafya kuyamaliza mambo! Ila judge bado ana mashaka makubwa! Yule boss pale kumhadaa maana anampa pesa sio za kitoto amuibie DNA! tumekungoa jino tumempa ampelekeee! Ndo kampelekea!
Nikavushwa boda na gari za jeshi mpaka South! Nikafanyiwa Surgery ya kubadilisha sura! Nikachagua sura kali kama black Amrica! Maana uwaraza ushanianza nikasogeza ahair line yangu! Nikarudisha na njino langu! Wakanipa new passport raia wa Mozambique! Utanijua! Tukarudi mpaka Mozambique nikaitumia kuomba Visa ya UK nikapata! Kwenda kwenye maonesho ya kibiashara ya utamaduni wa Africa! Nilitengeneza karatasi zote kama mjasiria mali wa vinyago! Nikajiunga na Saccos yetu! Saccos ndo ikaomba hizo visa kwa kusaidiwa na wizara ya ujasiria mali! I got my clean entry to UK! Kilichosaidia sikuwa kutoka bongo! Hata passport sikuwa nayo! So ma finger prints yangu hayakuwepo airport za watu!
Jane akajihamishia UK chini ya jeshi vile vile! Karatasi za Jane ni strong! Anaruhusiwa kuingiza watu 7 maana ni diplomatic visa! Tukafunga ndoa kabisaa! So akanipa mimi karatasi official! Naweza kuishi na kufanya kazi! Harusi lazima iwe over the top!
Its all fun and games mnapofunga ndoa mpaka ule mda sasa waalikwa wameondoka mmebakia wenyewe sasa kuanza shida na raha! Cha motooo ndo kinaanzia hapo! Uk tulikuwa tunaishi sehemu ya matajiri! Jijini manchester! Jane alinunua nyumba ya peke yake! Akasema hapendi appartment! Yeye anaona kamamkupanga vyumba tu! Nyumba nzuri, very cozy, very expensive! Ina eneo kubwa! Afu neighbor hood ya wazungu wabaguzi! Na hapo aliuziwa sababu alikuwa highest bidder mzungu asingeweza kuacha offer yake! Ali bid mara 10 ya bei ya sokoni! Majirani woote wakawa hawatutaki ila wafanyaje sasa!
Akasema hii ndo inatakiwa hakuna mtu ataekuja kwetu na sisi hatuna pa kwenda! Nikaona kuna tatizo kubwa! Ila by that time yeye ndo anamili uhai wangu! Nafanyaje? Zaidi yakumuunga mkono!
The first week ya ndoa, akawa anaongea na mibuzi maana sio moja! Mda wowote anaotaka yeye! Nikamuuliza! Akasema unadhani to afford this expensive life style kuishi mtaa mmoja na Idris Elba ni rahisi? Ina gharama zake na gharama moja wapo ni hii! Tulia hivo hivo! Nikasema sababu papa ni lake anyways nimuache!
Nyumba kubwa kuisafisha sio mchezo na mimi mwanaume wa kiafrica sijalelewa kufanya usafi na uchafu sipendi! Nikamshauri atafute maid! Akasema usijisahaulishe kama wewe ni mkimbizi! Na uko mafichoni! Hii ni UK mfanyakazi anaweza kuwa hata mpelelezi na kuharibu multi milkion investment ya kukuweka huru! Usicheze na mzungu! Kama unahitaji vifaa kusafisha oda online hapo!
After i igored the cheatings, maisha yakasogea kawaida! Then she got bored! Aliwahi kunichoka balaaa! Maybe nachosha ndugu msomaji! Siingizi hata shingi 10! Nikamuomba mtaji! Naona nikopeshe mtaji niwe naagiza vitu vya kiafarica Tz nauza E bay na Amazon! Akasema huo ni ungese nisiotaka! Akishajua mtu mmoja uko hai siku 2 judge atajua! Huli? Hunyi? Unachohangaika ni nini? Nikanyamaza!
Tukaishi hivo nikiwa mnyonge, akaanza kusema sex life is boring! Sijitumi, sipo spontaneous! Simridhishiiii kabisaa kabisaa! Kazi alionipa ni hio mojaaa tu nayo inanishindaa! Bora pesa zake ange enda ku bet casino! Sina maana kabisaaa!
Akaanza mambo ya ajabu! Siku hio usiku kaja na barafu kwenye ki ice bucket! Nikajua anataka kunywa wine labda au pombe kali! Akaziacha! Akaniambia njoo tufanyane! Kaziweka juu ya kitanda! Sikuelewa kazi yake! Sikuwa na mood ila mood yake ndo ilikuwa mbaya zaidi! Nikajikuta sababu ya woga nakubali! Tumepiga mechi nakaribia ku piziii asiniwekee barafu kwenye kende ni nini? Aiseeee chali yangu! Kama sikufaa siku hii baso sifi tenaaa! Kumbe zile barafu ndo kazi yake!Acha tu ndugu msomaji! Nilijutia dhambi zote nilizowahi kuzitenda!
Baada ya pale nikamuuliza tu sasa kwanini kanifanyia vile! Ilibidi niende kidiplomasia! Akasema hio ndo spontaneous! Mambo ya mjini! Nilisikitika sanaa! Sasa nikajua huyu mwanamke ni kichaaa! Akaanza kunipiga! Mkumbuke huyu si mwanamke lege leg ni komandooo wa jeshi, kipigo chake kimeenda shule! Anaweza kukuminya pumbu ukabaki umeganda kama nyamafu! Ashawahi kunichoma na pasi! Kunikata na visu hio ni kawaida! Ashaninimwagia maji ya birika mgongoni! Ashawahi kunisukuma ghorofani kwenye ngazimpaka chini! Na sipelekwi hospital napona hivo hivo kimiujiza! Au naoda dawa online! Au na goigle home remedy!
Mwili wangu ukawa na makovu makovu mengi sana! Hasa mgongoni aliponimwagia maji ya moto mara kadhaa pakawa hapa aminiki! Ikawa zaidi ya utumwa! Her spontaneous ways got out of hand! Mara anifunge pingu! Mara anichape viboko! Suala sio nini alinifanyia swala ni nini hakufanya!
Nikaaa nikawazaaa nikaona huyu nikimchekea ipo siku ataniambia itabidi yeye awe ananifanya mimi! Hapana kwa kweli! Siku hio nikamwambia Sikiza Jane kwa sababu our relation is already toxic ipo siku utakuja kuniua inaweza kuwa sio leo, sio kesho, sio kesho kutwa ila ipo siku! Utapatatabu pa kuutupa mwili na hii nchi ya mzungu usicheze na mzungu atakukamata tu! Utafia jela bure! Bora uniachie niondoke nikafie mbele!
Akauliza nikikuachia utaenda wapi kwa mfano? Nikamwambia nitaenda hata kuwa homeless! Naishi barabarani humo! Akaniambia sasa huko ndo utapata nafuu? Utakuwa una bakwa na wanaume wenzio kila siku! Hata usijaribu! Huku homeless unakuta waturuki wenzio wametoka vitani huko, magaidi na nusu wana silaha za kivita si watakubaka kila siku! Dont even think kutoa mguu wako kwenye huo mlango! Badala uwaze how will you get me pregnant unawaza kuwa homeless! Jamaniii! All that money i spent to own you and you are such a bum! Mambo kama haya ndo yananitia hasiraaa! Ngumi zikaanza upyaaaaa!
Aka update security Surveilance kaleta mtaalamu toka israel! One of the best company wana cutting edge technology! Kumwambia vile kama nilimstua nitatoroka! Ikawa hata nje siwezi kutoka mpaka anipe access! Ikawa sasa kajua nia yangu ya kuondoka! Yaani hata umeme ukikatika ndani ya sekunde automatic generator imewaka! Balaaa! Nikakata tamaa ya kuondoka!
Nikaanza kuwa nashinda online najisoema vitu! Na kujifunza how to munipulate the surveilance system! Nikajua umeme ukiwepo ni impossible! Labda umeme ukikatika na huku ulaya haukatikagi ni manipulate generator! Kumanipulate generator ni rahisi sanaa! Na lina bumaa instant! Na generator lilipo siwezi kufika bila acess! Kama kulibumisha nili bumishe kabla huo umeme haujakatika Jane akinipa acess! Ukikatika nateleza!
Kikubwa kilichokuwa kinanikeraaaaa mnoo mno ni kunifosi ni smile mbele za waru tukitoka! Ambayo ni rarely! Mashetani yake yakikaa vizuri! Au siku ya birthday yake au birthday yangu! Au akiwekewa hela zake from bongo! Ni mara chache sanaa! Siku tumeenda kula katika hizp chache! Nikaenda chooni, nikawaza sasa chansi si ndo hili! Nikachomoka kama mwehu! Nikowa njiani nikawaza sina pesa, sina karatasi, sina chochote afu black mbona nakisogelea kifo! Bora nipambane nife siku ingine! Nikarudi hotelini! Sikumkuta Jane! Ni mbali na nyumbani ila nilitembea masaa 4 afu usiku! Nikakuta kajifungia ndani! Niligonga hakufungua! Mpaka asubuhi!
Akasema umewaza vizuri sana! Nilikuonea huruma! Nilijikuta nalia tu ndugu msomaji ni kweli natia huruma! Nilitegemea asiponiadhibu kwa kunikata korodani sijui! Ila hakufanya hivo kuna jambo lilikuwa linamtatiza! Akaniambia tu naenda bongo mara moja kunatatizo! Sababu uliondoka kwa kujaribu kunitoroka sikuachio sh kumi! Jibane uishi kwa vyakula hivi hivi! Sijui nitarudi lini! Akawasha surveilance! Nikamwambia naomba basi nisafishe nje maana kutakaa mda majirani watakuwa concerned! Akakubali!
Nikabeba pakti ya chumvi na kumimina yote kwenye generatorsehemu ya mafuta! Nikasafisha nikaruid ndani akawasha surveilance! Chakula aliacha kidogo kweli kweli! Kikaisha baada ya wiki! Nilikaaa siku 3 bila kula! Nikatubu Mungu baba wa mbinguni! Nisamehe kwa yote! Ila usiruhusu nife hivi kama mfungwa! Njaa ikanizidi hata toba ikashindikana! Nikazimia! Nikaja kushtuka kuna li storm kubwa! Umeme umekatika na geberator imebumaa! Baridiii ni la kufa mtu! Njaa nikatoka nje na kula majani ya miti ndo kupata nguvu!
Nikaanza kuwa naenda mbali ambapo hawanijui naokota makombo nakuja nakula zangu! Nashiba kabisaa nafurahi! Nikawaza siwezi kuishi hivi nafanyajeee! Akaja kurudi baada ya mwezi! Akashangaa generator imebumaaa na sijaondoka siku zote hizi! Alishangaa sanaa! Akaniuliza mbona hujaondoka? Nikamwambia niende wapi nikuache mke wangu? Japo wewe hunipendi mi nakupenda hivo hivo!
Akapunguza surveilance kabisaaa! Akaanza kuniruhusu niwe naenda kokote! Ila karatasi zangu hakunipa! Kuna mambo yakawa bado yanamsumbua sanaa! So mda wa kupamvana na mimi ukawa umepungua!
Katika kupita pita online nikaona export business! Watu wanalima na ku export huku nje! UK, na Uarabuni! Wanapata pesa! Nikasoma soma nikaona nikiweka one B natoa 4 B! Nikawaza napata wapi hizo pesa! Kila nikijitahidi kisahau hilo swala nashindwaaa!
Jane ana pesa cash ila sio one B mule ndani na anajua mpaka shilingi ya mwisho alioacha! Nikawaza sanaaa! Wazo likanijia! Jane ana alamasi na jewerly nyingi sana! Pesa yake anaisafirisha na kuihifadhi kwenye vito vya thamani zaidi kuliko cold cash! Ana vault kama 10 za alamasi! Anapenda mikifu, saa, bangili! Kwenye harusi yetu alinipa saa na cheni na pete zote ni ruasian diamonds! Its funny nilikula jalalanani afu leo ndo nazikumbuka!
Nikam befriend local jeweller na kumuuliza kamamnataka copy atanichongea bei gani? Akanipa bei! Nikaenda london kuuza Saa! Nikapata pesa nyingi nyingi inatosha kumpa yule m Jew anipigie copy zile diamonds zangu! Nikaanza kuvaa saa ya copy hakustukaa! Nikaanza kuvaa pete ya copy hakustukaa! Nimeuza vyote bado pesa mbuzi!
Trekta moja ya John Deeder mpya ni million 60! Zinatakiwa trekta 10 kwa mipango yangu! Sikutaka investment ndogo! Nilitaka dili moja linabadilisha maisha! Trekta tu million 600! Bado machinery zingine! Eneo na kila kitu! Ku export zinatakiwa tani na volumes! Nishampanga Kyle kakubali!
Nikajaribu password ya vault ya Jane ! Sam ilikataa! Nikajaribu Deo! Holaa! Ghost holaa! birdthday zote holaaa! Linda holaaa! Nikachanganyikiwa! Nikajaribu siku aliokufa mwanamke wangu holaa! Siku aliokufa Linda ikafungua! Jackpot!
Nikaanza kutoa napiga copy! Natoa original naweka copy! Original nazi auction online huko kwa mashekhe wa uarabuni! Unakuta original market price million 160, mi nauza million 100 tu! Warabu wanaanza ku bid! Tunaishia million 120! Wanatuma masobara wao! Wakiwahakikishia wanalipia wanachukua mizigo!
Biashara ya kilimo ni mchezo mchafu! In no time nikawa nishapiga copy vault zima la Jane! Siku tukawa tunatoka akachukua copy akavaaa! Hakustuka ni copy! Roho ikafanya paaah! Anapenda kuvaa hizi juwels tukienda dinner shemu za juu! Wazungu wanatoka mijichooo! Wengine wanakuja kuzishika kamamni za kweli! Anawaambiaga yeye ni African princess! Mara baba ake na visima vya mafuta nigeria!
Siku hio hamnaaa mzungu alieshobokea mkufu wake! Akasema Sam huu mkufu una tatizo gani? Mbona wazungu hawana shobo nao! Mi najua ni Copilaaa! Nikamwambia unajua Jane huu wa mda sanaa! Utakuwa umepitwa na wakati! Akasema hapanaaa! Alamasi hzipitwi na wakati! Kuna tatizo!
Wakati tunatoka mzungu nmmoja akasema if you have to wear fake jewels atleats wear them small! Akapaniki! Nikamtoa nje! Anadata! Anajua bei yake hiziii? Mavi yakeee! Njiani akapaki kwa sonara! Nilivoiona ile sonara roho ikafanya paaaaaah!
ITAENDELEA!