The Exit Game. Sidney, Amar, Mr. Police.
Amar.
Nilipotea mda mrefuuuu sanaaa, nilikuwa Israel huko nafanya michakato, nikaenda na Urusi kufanya michakato. Sasa kupata vibali vya kusafirisha yale mambo sio rahisi, ikabidi niende Sudan, kutafuta vibali vya kuagiza silahaaa. Yaani nimefight nimefight mpaka nikafanikisha. zitaenda Sudana na baada ya Sudan zitakuja Bongo na meli.
Nimerudi bongo nasikia tu Sidney kaolewaaa, mmmh nikashangaa kundoka kidogo tu kaolewa tena anakaribia kuzaaa. Nikapiga mahesabu yangu nikaona mara ya mwisho kulala nae mbona kama mimi ndo baba. Nikawa nikimpigia akisikia sauti yangu anakata simj. Hataki kunionaaa kabisaaa.
Nikaja kusikia kazaa mtoto, roho inaniambia bwana mtoto wako. Sasa kimbembe kamuhamishia kule quaters siwezi kabisaa kumpata. Alivokuwa Regency anakaa na mkwewe sijui mda wote. Nikaona kazi kubwaaa ila yule wangu najua jinsi ya kumpata.
Nikaenda kwa mama yake Sidney na kumwambia najua mtoto ni wangu, sasa mwiteni niongee nae, ama sivo naenda kutibuaaa kule. Mama anafadhaika na hivi alivokuwa hanipendiiiii. Akakubali kumita akampigia simu. Nasikia Sidney anasema sitaki kujaaa, sitakii aniache. Mama anamwambia ndo baba wa mtoto njoo tu tuta yamaliza.
Akaja basi eti haniangaliii usoni jamaniiii. Na mimi simuangaliii usoni Basi hasemiii. Nikamwambia mama tupishe tuongeee. Mi nikajua na ufirauni wangu wa hapo kati haitakuwa kazi rahisi, ila baada ya mtoto nilikuwa tayari kubadilika kabisaaa. Nikamchukua kwanza mtoto kweli damu yangu kananichekea, Sidney haniangalii usoni.
Nikamuomba kwanza msamaha, nikamwambia zile hela zimefika a good time, Mungu katuletea double joy. Nikaanza how i love her so much ma nataka kuondoka nao, turudi marekani. sisi bado tulikuwa na green card zetu, so haikuwa ishu kabisaaaa. Nikamwambia tunaenda Congo, tukitoka ni one way USA.
Akaanza kusita sita simsomi, nikamdaka kwanza na denda moja balaaaaa. Basi nimewakumbatia wote na mwanangu. One happy familly. Kumpa mate akakumbuka mimi nani kwake. Akaanza kuniambia Police anakusaka, anajua kila kitu we jisalimishe tu atakusaidia. Nikamwambia wa kutusaidia ni Mungu tu. we unafikiri mi na huyu mtoto naweza kufanya makosa. Niamini mimi Sidney sijawahi kushindwa.
Nikamwambia rudi ili asistuke. Tukawa tunawasiliana sanaa, naenda kumuona clinic, au njiani, nikamwambia tengeneza passport ya dogo na jina silitaki hilo. Majina mengine damu haziendani yataleta nuksiiii. koo haziingiliani. We were set to go.
Akaja kunipigia maejuakuwa tunaondokaaa, ameniuliza indirect namwambia tulia hata akijua kwa ilipofikia hawezi kufanya chochote. Tarehe 3 usiku njoo, asubuhi saa 11 tunangoa kambi. Usimuage mama yako hanipendi hatari atampigia Polisi mi nakwambia.
Nikawa nampa mahaba mazitooo, ili mradi tu kumuweka vizuri. Basi ananiambia Polisi kajua unapita Congo tarehe 8 amejiandaa. Akasema ndo maana tunapita tarehe 5. Akija tarehe nane akute manyoya tu. Hio tarehe ilivofika usiku akaja na mtoto, na kibag. I was set to gi with my family, Usiku tumelala mwanangu hata hakusumbua kama alijua yuko na baba yake kipenzi.
Usiku Sidney hatulii ananiuliza maswali mia kama vile ana mashaka kwamba tutakamatwa. Ikabidi nimtoe shaka kuwa wazitooo wote wa nchi wametoa baraka zao. Ashtukaaa. Kwa hio Police mbona anasema tofauti. Nikamuhakikishia police hajua chochote by the time tunapita boda, he will remain nothing but a joke. Mi nina vibali vyote vya kupitisha hizi silaha. Zinapita kama za UN za kusaidia kulinda amani, wanaohusika wote washapewa chao. Nisingeweza ku risk maisha yako na ya baby wetu bila kuiamini hii kazi. Akasikitika maskini polisi. Namtoa shaka he will survive usiwe na shaka.
Siku ya safari ikawa inaenda ndivo sivo kwa mambo mengi sanaa. Yaani niliboreka na vitu vingi sanaa. Ila anyway nikawa niko off mood kabisa. Siku ya mikosi ni mikosi tupu, nimefika border Polisi huyu hapa yuko na timu yake nzima.
Akaja kunikagua sina shaka nikamuonesha vibali halalk hakuamini jicho lilimtoka sio kidogo. Anakagua vile vibali mara laki 5. Baadae akashindwa kuvumilia na kusema hata pamoja na vibali ananizuia pale pale na kuita press. Nikamuita chemba akaja kwa kujiamini akijua nataka kumpa rushwa. Nikamwambia tu, mzazi mwenzangu, kwa mda ambao sikuwepo ulinisaidia majukumu yangu, iko hivi i will do you one favor to settle the score.
Inside story ma boss zako muhimu wote washapewa chao kitambo. We umetumika tu kama kutusindikiza kuhakikisha hatupati matatizo au siwazunguki. Akawa anabisha muonho wewe amar kwani sikujui, you cant fool me. Nikamuonesha chats zangu na boss kubwa akinitakia safari njema na kusistiza mizigo yote ipitishiwe nchini ikibidi. Nikamionesha chat ya boss wake akiniambia keshamshughulikia kumtoa kwenye kesi hivo hatonisumbua. Nikamuonesha mpaka chati ya waziri. Alichoka. Nikamuonesha transfer za hela ndefu zilivofanyika kwa ndugu zao. Akajua pale hana kesi wala mjukuu wa kesi. Nikamwambia unanichelewesha, mke wangu ashatangulia atakuwa ananisubiria na mwanetu. Akaanza kuulizia sidney alipo, ilihusuuuu?
Nikavuka border lile kibabe nahisi nilimuacha na homa huku nyumaa. Al
********************************
Mr Policeman!
Sikuamini kama Amar kapita katikati yangu na kwenda zake, kama Yesu alivopita kati kati ua wale wana sinagogi waliotaka kumtupa nje. Nilikasirishwa na mambo mengi sanaa. I couldnt believe i was used beyond words na ma boss zangu. Ilikuwa nikifika tu Dar naacha kazi. Roho iliniuma kwa vingi. Nikawaza i could even have made Amar my partner. I was so stupid, i was so dumb, nilijilaani sio kidogo.
Maumivu mengine nikawa nawaza Sidney kaniacha tenaaa, after everything i have done for her. Nilikuwa na maumivu mengi sanaaa. Nikawaza huu ndo ule muda wenzangu wanasafisha bunduki zao na kujielekezea kichwani. Niliwaza jinsi gani jeshi lilivooza. Nikawaza yani wanawake wengi kwanini nahangaika na yule boyaaa, niliwazaaaa sanaaaa.
Nikawaza asingeondoka i would have been the happiest man in my life ila ndo kaondoka tenaaaa. Kufika dar toka Kigoma japo nilipanda ndege ila nilichoka sanaa, kama mfu, nikasema ngoja niende nyumbani kwanza nikapate akili kwanza. Nimefika home hivi kuingia naona nyota nyota nikaamua kwenda police mess. Nikanywa, nikanywa nikanywaaa. Nilikunywa sanaa basi tu, kupata valium ya matatizo.
Jioni nikiwa nimelewa chakari nikajikokote mpaka kwangu nikaingia ndani. Nikawa namuona Sidney, namuona katoto ka Angela, yaani naona tunakaa anaisemesha vitu sielewi vitu gani ila tumeongeaa kabisaa, nikamwambia naenda kulala. Pombe sio chai.
Nimestukaa asubuhi nasikia shower inawakaaa bafuni, nikasema ulevi huu nitakuwa nilifungua usiku sikuifungaaa. Nikawza maruwe ruwe ya jana. Hamad nasikk kitoto kinalia. Nikasema akili zangu tu. kikalia tena. Nikakiona kipo kabisaa kitandani kwake.
Nikafurahiii, nikajua kumbe ndo maana hakuwa kwenye gari la Amar, alirudi kwa ajili yangu. Nikaruka kukawahi katoto. Kanichekeaaa. Nikajua Sidney yupo bafuni. Kitoto kile kikalala tena, sikukawia nikawahi huko huko bafuni, hakukuwa na mda wa kupoteza. Nimefika bafuni nikamuwahi na mate mali zangu mwenyeweeee.
Sikuuliza nini wala nini. Na yeye hakusema nini wala nini tukapena mambo moto moto mazitooo, matamu balaaaa. Kule kule bafuni. Hata sikumuuliza kama Dr alimruhusu au vipi. Baadae ndo nakuja kukumbuka kumuuliza kama Dr. alimruhusu, akasema ndio alimruhusu.
Sikwenda kazini wala nini, nilitaka kukaa, na baby wangu siku nzima tunapeana mambo. Mchana nikapigiwa simu kuna dharura niende, nikaenda ghafla, Kufika boss ananionesha habari za online
AMAR KAFARIKI HUKO CONGO, JANA HIO BAADA YA KUVUKA TU BORDER AKAPIGWA RISASI. HABARI ZIMETOKA GAZETI LA CONGO, NA PICHA YA MAITI YAKE IKIWA IMEVUJIA DAMU.
Habari zilikuwa kifaransa ila baada ya kutranslate ikaonesha imeandikwa raia wa tanzania mwenye kibali cha kuishi marekani Amar Mohamed Ali, amekutwa amekufa akiwa amepigwa risasi kadhaa mwilini. Passport yake ikawekwa pale. na green card yake.
Nikachoka mwili na roho.
INAENDELEA SAA 5 NA NUSU USIKU HUU.