Weekend story: Bad wives

Weekend story: Bad wives

Unyunyu wa Kuruthum hahaaaaaa si kwa ile harufu yake
 
I'm waiting eagerly na nimeshaweka reminder... keep it up @Lara1. you rock it with your narration
 
aCHA BANGI NDO KWANZA SAA 5, NA NISHAMWAGA KWANZA EPISODE YA SAA 7 USIKU ULE ULE IKO HAPO JUU.

Duh kama ningekuwa navuta ningehisi zishanivodafasta tayari, maana hicho kitu cha juu hapo hata sikukiona.
 
Kupatwa kwa afande,sipat picha amar akijua kua sidney anamimba yake then analea afande
 
Long time kitambo sijapata utamu wa kubwa lao wa wkend story! Ngoja nianze sasa
 
MR. POLICE MAN.

Not that i didnt know the kid was not mine, i knew it all allong, she ws straight foward from the beginning. Ata first all i wanted were a few good moments with her, sijasahau alichonifanyia, so i wanted to use her, make her know how it feels being used and dumped. Then when she told me she had a baby i had a lot of questions in my head.

I knew i wasnt a father but why would she give the baby to me? Under logical conditions she was supposed to give the kid to Amar, because probably because she loved him most and he was once rich and could be rich again anytime if i dont catch him. Au mtoto sio wa Amar so she is looking for protection, anajua akimwambia Amar mtoto ni wangu, Amar wont reap her and the baby apart. He wouldnt dare considering nimeshamkaanga vya kutosha karibuni hatojaribu. That was logica.

Ila kama mtoto sio wa Amar ni wa NANI? By the way kwa umri wa hio mimba walishacha kuishi wote na they were not sworn enemies, hata kwenye sherehe wakikutana wako poa just not for longer than 10 minutes they start throwing daggers at each other. I was gonna play with her but not the innocent kid.

Mipango yangu ikawa ni kufanya jambo moja la kingwana kabisaa kama alilotaka kulifanya St. Joseph kwa mchumba wake Marry baada ya kugundua ana mimba. DISAPPEAR. Nilitaka nimtoke kimya kimya tu, kiutu uzima, nibadilishe namba, nisafiri kikazi mfululizo mpaka akate tamaa.

The there was the issue ya boss, nishampa mpango mzima, kuwa namzoea yule mwanamke kupata data za Amar, na akanipa go ahead kabisaa, na funds aka clear za kumuhudumia fresh ikihitajika mpaka habari zipatikane. Kila kitu kilikuwa kwenye mipango yake. Baada ya kujua mjamzito nikarudi kwa Boss kumwambia nabadilisha approach kuna ishu ya mimba imejitokeza so sitoweza kuendelea na plan.

Boss ana roho ngumu huenda ndo maana akawa boss. Boss kashikilia msimamo, for now the kid could even be yours. We si umelala nae pia. Maybe amepata mimba hajui kati yako na Amar nani baba, sasa akajua akikupa wewe mtoto wa Amar poa ila akimpa Amar mtoto wako patachimbika. You could be the father.

Na kukupa wewe mtoto tuko kwenye nafasi nzuri sanaaa, she is ready to spill the beans, only press her right buttons. Mi nakwambia we are set to go. We kubali hio mimba si kuna fungu unachukua huku la kuwa baba kwani bure sasa Be a nice father and maybe Amar may die in the process and you may get to keep the kid. Who knows, the world is full of surprises.

Sikukubaliana nae, nikamwambia najitoa kwenye hio case, na kama kazi ndo hio ya kuuza utu basi naacha. Akasema kama una la kusema kamalizane na IGP. Maana anafatilia hili swala karibuuu, ashaweka press conference pending kutangaza hili tukio the minute uki mbust Singa singa na Amar. Sasa kama unajitoa kamwambie mwenyewe. Nikasema sawa.

Nikaenda mpaka kwa IGP nimekaa nje, akaanza kuwatukana watu, anafokaa ishu za msingi kabisaa anafoka kama anamfokea mwanae wa miaka 6. Mmmmmh! Ujasiri ukaniisha. Manake mara amwambie mtu ukiongea na mimi kaza makalio mtoto wa kiume sio kulegea legea. Mmmmmmhhh! Nikanyanyuka mdogo mdogo kurudi ofisini kwangu. Boss akauliza umemwambia? Nikamwambia sijamwambia akasema good, usiache kwenda clinic.

Jioni nikampigia simu, nilitegemea nitakuta missed calls hata 50 given the situation alivokuwa desperate sijakuta hata moja wala nini. Mwanamke jeuri huyu. Nikamuanza mwenyewe. Baadala yake nikaamu kwenda huko huko. I need to figure out things first so sikutaka kulala nae tenaa mpaka niwe na uhakika.

Ukiishi na mtu bwana ndo unamjua. Mwanzoni ilikuw mtihani kweli kweli. Kwanza i dont know what i want. Ujue bora ukae na mwanamke mimba yako, mimba ya mtu afu unajua ni mtihani kweli kweli. Akianza kudeka ananikeraaa sio kidogooo. Natamani nimshushue aache mambo zake hio mimba sio yangu najikaza tu. Maybe because i am a nice person ndo maana niliweza.

Then she changed, akawa anapika, ananijali, she was trying, isingekuwa mimba maybe i could have loved her again ila sio kwa mimba ile. I must admit wanawake wajawazito bwana watamuuu, kwanza mimba ile anangaa kama papai, afu huyu hakuwa mjamzito yule mchafuu mchafuu, mjamzito huyu mda wote lipstic iko mdomoni, anangaaa, nywele zimesukwaa zinangaaa, fashionable, kucha anatengeneza, na mazoezi anafanya basi ndo anangaaa kama papai bivu.

Kiukweli sikuwa na nia ya kumla ila mitego yake ilinishinda, kila mara nasema leo namla cha mwisho, leo cha mwisho, kesho namla tenaa, na tenaaa, mpaka sasa niakzoea kumla. Ikawa lazima nifungue njia kila siku na kila mda unapopatikana.

Baada ya kuzoeana sasa akanijua mimi ni mtu wa aina gani, na mimi nikamjua ni mtu wa aina gani, tukaweza sasa kuishi kwa maelewano. Ikawa ikifika saa 10 na nusu sikai ofisini hata kwa dawa, nawahi zangu nyumbaniii. Nyumbani. Saa 12, baby mama anakuja, kwanza napewa juice, nakunywa baridiii, mi si ndo baba mwenye nyumba.

Tunaanda vitu tunapikaaa wote, mimba sio ugonjwa nimpikie nani kasema. Mi nafanya akzi ngumu kama kuosha vyombo, kudeki, yeye anakarangiza mambo, tunakula, naosha vyombo. Baada ya hapo miguu imevimbaaa, namkandaaa. Basi we started healthy conversations yani we could talk for hours bila kurushiana daggers, kukumbuka kipindi kileeee.

Jioni tunasali kabisaa, alikuwa anasali sijui alikuwa anaomba Amar asirudi sijui, au ajifungue salama sijui ila dada alikuwa anasali ni balaaa. Baadae nafungua njiaaa ndo tunalalaaa. Mpaka ikafika stage mwenyewe nikaomba Mungu Amar awe kafa huko alipo na tuishi hivi hivi asije tena. Au nikawa nawaza tu kwa mfano, yani kwa mfano hata Amar akija aamue tu hamtaki tena Amar, tubakie hivi hivi ila nilijua hamna kitu kama hicho pale upendo wote na mandingo yote just because she was out of options. Ila kujali hata kama kuigiza alikuwa anajali, i could have beend fooled ananipenda mimi ila namjua.

Hospitali nampeleka, Dr. muhuni sanaa anaongea vyote kasoro mimba ina siku ngapi. Mi nawaangali tu najifanya sijui nini wala nini. Mama yangu ane sijui alisikia wapi nakaa na mwanamke mjamzito, akaja fastaaaa kunihudumiaaaa. Jamaniiii. Mi narudi namkuta kajaa tele, yupo na mkwewe anamfumua. Sikusema kitu. Nikakaa kimya na yeye hakusema kitu. Ila ndo akaamua haondoki maana mimba ilishakaribia mwisho bado wiki kadhaa tu ajifungue. Basi anauambia ukoo mzima nakaribia kupata mtoto jamaniii. Huyo mtoto vipi. Navomkataza ndo anawaambia na kuwaambia nimemwambia asiseme jamaniii.

Sidney mkorofi, ila mama mkorofi mara 2 ila cha kushangaza wakawa mashogaaa. Labda sababu mama shangingi anapenda ujana na urembo na Sidney akawa anamjazaaa, kumnunulia migua ya botic, madhahabu, misaaa, simu, anamfundisha mambo ya Instagrama, whats up, live band. Ikawa sasa kama mama yangu ndo mama yake yeye sasa. Nikichelewa nagombezwaa utafikiri sasa yule ndo mkwe wangu. Jambo lolote yuko upande wake namuonea sijui nini. Jamaniii. Hata TV wanaungana kuchagua channel.

Mkwe wangu hakuwahi kuja tukaonaa hata siku moja, sio baba sio mama. Mama Sidney alikuwa anakuja mchana, nikiwa sipo mama aliniuliza nimemfanya nini mbona hataki tuonane, ila wakawa mashoga wa 3. Mi nilijua tu walikuwa wanajua yule mjukuu sio mwanangu hivo kuepusha aibu wakaona wawe wanakuja kama digi digi.

Ikiwa imebakia wiki ajifungue, Amar akarudi mjini baada ya kupotea mda sanaaa. Nikapata tetesi ana shehena kubwa ya silahaaa anaipitisha nchini kwenda Kongo. Kila naempepelza anajua mpaka hapo tu. Shehena inatoka wapi inaenda wapi hawajui. Na lini au wapi hawajui. I was out of time. Nikajua tu sina namna zaidi ya kumbana Sidney.

Kwanza nikamwambia Amar karudi una taarifa? Akastukaaa, akajikausha hana taarifa, kwanza yeye taarifa za nini wakati ana familia huku. Nikamchana najua hio mimba ni ya Amar, na najua kitammbooo. Akawa mdogooo. Akapanic akawa hana la kusema, zaidi ya nimejua lini. Nikamwambia toka mwanzo. Basi akauliza kwanini umenisaidia? Nikamwambia kwasabu mimi ndo nampenda ukweli na nataka kumsaidia kiukweli kweli.

Najua Amar hatokubali kuondoka mjini bila yeye wala mtoto, sasa nataka kumsaidia na Amar, sababu sitaki mtoto aje ajue mimi ndo nimefunga baba yake. Amar akija kumtafuta aniambie mimi na atukutanishe then Amar akijua tunajua kila kitu hatopeleka hizo silaha, hato dakwa, na hatoozea gwantanamo bay maana hio kesi sahivi ni ya ugaidi. Na kwa kunimbia mimi Amar akija atakuwa kajisaidia mwenyewe na kamsaidia Amar. Akikaa kimya Amar atafungwa and she would break my trust, and abuse my goodwill. Akawa na mawazo kweli.

Kesho nipo ofisini, mama ananipigia simu tayari mambo huku. Aliumwa tumempeleka hospital. Nikaenda Hospital nikakuta kajifungua katoto ka kike, kazuriii. Mama kujitia bibi ndo yeye. Nikakaangalia nikaamua yule mtoto simuachii Amar hata iweje. Kwanza mimi ndo baba yake. Yaani simpi hata iweje, yule ni mwanangu and nothing can convise me otherwise.

Wakwe wakaja ila hawaniangalii usoni wala nini, wanajikausha kausha kwa aibu. Na mimi sikusema kitu. Sidney mwenywe baada ya kumwambia najua mtoto wa Amar akawa haniamini amini kabisaa na yule mtoto sijui alijua nitamdhuru au vipi, manake nikiwa nae mimi hana amani kabisaa. Akaniambia anarudi kwao. Nikamwambia hamna kitu kama hicho. Akakubali tukarudi nyumbaniii.

Ukapita mwezi hamna habari za Amar wala nini. Speculation zinazidi tu kitaaa. Baadae ikaja kujulikana mzigo unaenda Bukavu. Baadae Sidney akaona jinsi navokapenda kale katoto akanielewa. Maana usiku kucha nahangaika nako, kinakunya kunya, mda mwingine yeye ananiambia mwanao kanya huko. Hahaaaaa! Nikamuuliza Amar hajakutafua akasema hajamtafuta wala nini. I jus believed her.

Siku hio nipo kazini ananimbia yupo clinic kadi kaisahau nimfatie nimpelekee foleni kubwa. Nikarudi nyumbani kupekua pekua kadi nikaliona. Nikaona kuna kapochi kamefichwaaa kwenye konaa kabisaa ya kabati. Nikakachukua. Nikataka kuifungua roho ikasema muamini, nikakarudisha, nikatoka mpaka kona ya 3, nikarudi nikakafungua, nikakuta kamtengenezea mtoto PASSPORT. Na mtoto mimi nilimpa jina la mama yangu, na nikamuandikisha jina langu. Ndani ya hiko kipochi nikakuta na affidavit anataka kumbadilisha mtoto jina kurudi Amar.

Nikavirudisha, nikampelekea kadi clinic kama sio mimi. Ila roho iliniuma sanaa kujua kumbe Amar kamtafutaaa, na wana mpango wa kundoka wote na mtoto. Na mpaka kapata passpot ni mda mrefu anawasiliana na Amar. Roho iliniuma sanaa, sijui kwanini manake ndo ilivotakiwa kuwa still roho iliniumaaaa. Nilichojipa moyo nitawakamata wote, na mtoto atalelewa na bibi yake nitakuwa namuonaa.

Alivorudi nikamtegaaa, kwa mfano Amar karudi kakwambia muondoke wote, utaondoka nae au utabaki na mimi? Akatoa mijichooo kama kabanwa na mlango.

ITAENDELEA SAA 4 USIKU.
 
Back
Top Bottom