THE PRESENT (Sidney)
Not that i didnt like Amar, i liked him a lot, and i could swear at one point in life i loved him to death, of course before he turned into a total jerk and a broke ass. Him i liked but i also liked finer things in life, the good life you know. Bora usiwahi kushika hela maisha yako yote kuliko ushike hela afu ije ikimbie cause you will know exactly what you are missing and it is not a feeling you will wish to entertain.
I couldnt figure out what made me despise Amar more, the fact that he was broke, or the fact that he always can do anything and everything but he couldnt save our baby. Maybe both, maybe either but i was so done with his broke ass. Now that age has gone, dating again was not a life in the park either. I could tell Amar was having the time of his life, fucking his sorry life off with loser girls.
Mnaweza kuhisi labda mimi kumuacha Amar was an easy decision like i woke up one day and i was done, hell no. How could i. It was disappointment after disappointment after disappointment. You can imagine. . There was cheating, serious cheating, different girls, different stories, then there was the lies, and there were the moods and bad temper and his lazy ass not wanting to do anything all day rather than sit on the couch.
Well i wasnt getting any younger, neither was he, i just decided maybe it was time to call it quits. Waliachana princess Diana na Price Charles itakuwa sisi. He didnt want to break up not until i lit fire crackers up his ass and he couldnt take it any more and moved out the house willingly. Hahahaaa! I would yell and nagg at him all day everyday, i would denny him sex, i wouldnt cook, wouldnt wash for him, or do anything. Nikaanza mpaka ku flirt na wanaume wengine anaona kwenye simu naongea naoo yupo hapo hapo akileta kwere namkumbushia mafumanizi niliomkuta nayo. Mwisho akaona tutakuja kuuana akaamua kuhama mwenyewe.
Baadae akaja kuniambia kanitafutia nyumba Masaki, he is changed, he wants us back together, and he has money comming in soon. Kunitafutia nyumba was so like Amar, after all i was not gonna pass that offer, nikakubali kwa masharti nitaishi peke yangu pale, mpaka nitakapo jiridhisha kabadilika ndo nimrudishe. Actually i was not taking my chances asije pata hio hela kweli afu nikawa nishajambia kwa mbele.
I wasnt seeing anybody serious, Joey wanted to come back, nilivosikia mkewe alimdevorse, na alisign prenup kwa hio hakutoka na kitu, he was lost in the bronks, doing shitty jobs. So he wanted to come back ila hakujua wapi pa kuanziaa ndo kujaribu kunitumia mimi kama laverage, thinking kwamba maybe even this time Amar yupo. Kumbe angejua huku mambo magumu hatari. Even as dumb as i was nisingeweza kuanza nae upya. If i was gonna get somebody he should be an upgrade of Amar.
I hated my job, i hated my life, i hated everything and every one. I was bored to death. Without Amar life could be really a bore. My neighbours were so boring i swear i couldnt stand 2 minutes with them. Those idiot women. Kazi kusifia wanaume zao asubuhi mpaka jioni. Life can really test you by everything happening at once or nothing happening at all. I guess my life was on the nothing happening at all phase.
One day as i was running someone tryed to mug me, you bet i shoved a knife on him, bahati alijikinga na mkono. Trust Amar nilikuwa siwezi kwenda kokote bila kisu. Utakaaje kizembe zembe mjini hapa, unaweza shangaa akaja mtoto na bis bisi na kukutemesha mpaka mkojo ukakutoka.
Then there was the day Amar was locked up, na hana mtu wa kumtoa. Kwa jinsi alivofulia isingekuwa rahisi yeye kupata mtu wa kumtoa jela. Mjini watu ndugu wa pesa. Kama kawaida anajifanya hana kosa lolote kawekwa tu ndani bila sababu. Trust Amar he can look you in the eyes and lie on your face. Nikaenda kumtoa, na kweli baada ya kufatilia he did nothing for the first time he told the truth. Nikawaza maybe he is changed
You bet tulikosa msaada pale kituoni, hela hatunaaa, kufatilia tunazungushwa tu. Kama bahati nikamuona Afande, yuleeee afande wangu wa kipindi kile, kwanza hizo nyota alizokuwa nazo sio za kitoto. Nikajisemea tu Amar humu hatoki leo wala kesho. Kama ni huyu ndo kamuweka ndani amekwishaaa. Baada ya kusota sanaa, nikajizoa zoa mpaka kwa Afande, nilikuwa naogopa sio kwa kumuacha kule jamani, nikajua he would be beyond mean. Ila tofauti na matarajio yangu akawa tu mtu anaejali like he has alaways been, akanisaidia kuchimba mkwara pale mpaka Amar akatoka.
Sikutaka kumwambia Amar kuwa afande kamtoa sababu angejirudisha ndani na kujiloki kwa jinsi alivo mkorofi yule hahaaaa. Akajua labda nimefanya fanya manuvaaa akatoka. Na sababu pekee hakulipiza kisasi kwa kuwekwa ndani ni alikuwa na dili muhimu sanaa analifanya ambalo hata mimi aligoma kabisaa kuniambia linahusu nini wala nini.
Basi usiku ulikuwa ushakuwa mkubwa, tukaenda wote masaki, kiukweli alitia huruma kuwekwa ndani bila kosa, na lile swala la Afande kuwa boss mkubwa pale lilinitetemesha sio kidogo, it made me feel pity on Amar akija kujua, na tulivomfanyia, angepanic kabisaaa. One thing led to another which led to another, tukaanza kubusianaa. Na Amar mambo anayajua sio kidogo, na nilikuwa nimemisi sio kidogooo. Ikabidi tu niji enjoy kwa usiku huo. Mambo yalikuwa matamuuu sanaa, na yalinoga balaa sasa sijui kwa sababu ilikuwa kitambo toka tupeane sijui. Ila usiku kucha ni mechi ilipigwa.
Asubuhi nikamuandalia chai kabisaa nikaenda kazini, huwezi amini nilikuwa tayari kumsamehe arudi pale tuanze upya kuishi wote na kujipanga na mashambulizi ya Afande. Siku nzima ofisini namuwaza yeye, mawazo ya upendo na furaha kubwaaa. Nawaza nirudi nimpikie chakula anachokipenda, tupeane mambo tenaaa. Kiu yangu nilio kuwa nayo haikuwa ya kukatika siku moja.
Nimerudi kwa bashasha kibao, Nimefika kwanza nampa mabusu kibaoooo, na Amar tenaa kwa kuonesha ushirikiano hana mpinzani. Nikasema niende kwanza uwani kukojoa nasikia kuna harufu ya perfume ya bei rashisi mbaya mbaya tena naijua ni Kullusumu. Nikahisi labda nanusa vibaya. Nikaenda chumbani kunusa shuka ndo lina harufu hatariiii.
Nikamfata sebuleni, hawezi kuingiza mwanamke ndani kwangu, mchana kweupee, wakati jana nimekesha namkatikia maunooo. Nilimfurumushaaa sio kidogo. Anaapa kwa Miungu ya kwao hajaingiza mwanamke mule ndani kwamba i got this all wrong. Nikamwambia sawa kama hujaingiza mwanamke umeingiza shoga, na huyo shoga anapaka perfume za bei rahsi kaicha bafuni na kwenye shula langu, mbwa mkubwa. Akaanza kumlaani tena huyo mwanamke kwamba why was she so dumb kupaka perfume wakati alimwambia wawe discreet na awe makini kutokuacha ushahidi. Ila aliondoka. Yaani alinikeraaa sio kidogo
Mara inaingia sms ya kimahaba namba mpya usiku huo. Nikajua tu Amar ananichezea picha la kihindi nikamjibu kunyaa, sio kwa umalaya huu alio uanza khaaaaa. Asubuhi naenda kazini nakuta roses nzuriii sanaaa. Hata sikujichoshaa nikajua ni Amar tu huyo. Zile sms zikaendela kila mara. Siku Amar akawa amekuja kuongea mambo ya kazi akaniuliza anaweza kufanya transactions ila akazunguka internal na external controls, yaani alitaka kufanya transactions ambazo hazitaonesha ni yeye au kumuhusisha yeye like afungue kampuni over seas, afu hio kampuni itumike kutuma hela kwingine just his usual criminal lives. Nikamwambia nitamuulizia kwa wataalamu wa Bank pale. Kabla hajaondoka nikamwambia Amar miua yako unayotuma kila jumatatu inatuletea nyuki ofisini, sikutakii, quit playing games, na kunitext na namba mpya hakutosaidia i know it is you. Na hio Janese dinner ulionishikia bango forget it
Amar akakataa sio yeye, with a lier of Amars caliber sikushangaaa. Ila kunitoa shaka akaniambia kama ingekuwa mimi Sidney siwezi kukuletea roses wakati najua for a fact unapenda Lillys na Orchids zaidi. Huyo anaekuletea roses hakujui vizuri na hawezi kuwa mimi. After all mimi najua you hate sushi you hate Japanese kwanini nikuoffe dinner ya hivo. Ingekuwa mimi nisngekualika dinner, ningekupeleka Serengeti picnic cause najua for a fact you love nature. You just have a secret admier. Nikupelelezee ni nani? Nikamwambia basi nenda, tushamaliza hapa.
Kweli kwa sababu alizotoa Amar isingeweza kuwa yeye. Na kule nisha kunyaaa hatari mda wote najua ni Amar. Ikabidi tu nibadilike na kuwa sweet ghafla. Thank you for the flowers za kutosha, chat za kutoshaaa. Still nilikuwa sijui nani ila my second guess ilikuwa atakuwa Joe keshaingia mjini. Ila Joe akanipigia na namba ya US so bado alikuwa kule. Nikakosa kabisaaa. I wasnt planning to be an easy catch.
Ila nilianza kuumwaa, najisikia hovyo hovyo, nikaanza kutapikaa, mtu ofisni akatania una mimbaaa. Nikastukaaa. Nikawahi nyumbani kupima kitu na box! Tobaaaaa. Na ni wiki 4 tu tangia nilale na Amar. Akili ikanichemkaaa sanaaa. Mwanangu anahitaji baba na Amar sio baba wa maana wala nini. Sawa kuna hela alisema atapata sipopata je? Maisha yakawa magumu ghaflaaa. Nikasema sababu soon nitazaa na kuanza kulea wacha niende nikafaidi maisha na secret admirer.
Kila siku ananiomba tukutane namzingua, siku hio nikamkubalia Japanese huko huko potelea pote. Nikawahi kufika, baadae akaja Afande. Sikushtuka sanaa wala nini, nikajua labda kataka kunichamba basi roho yake irdhike. Tofauti na matarajio yangu he was so nice, so loving, so caring, so Fatherly. Desperate times call for desperate measures. Nika bond nae fasta fasta, throwing myself at him, mda ulikuwa hamnaa kabisaa toto tayari lina wiki 4 tumboni. Wazo la kumbambika ile mimba nililipata pale pale na kulitekeleza
Afande akajiloga kunirudisha mpaka mlangoni yaani sikumkumkawiza nikaanza kumpa mate, akakolea kuingia ndani nikajua kazi imekwishaaa, hachomoki na mtoto wa buree ndo kashajipatiaaa. Nilimpa mambo usiku kuchaaa, kavu kavu, goli za kutosha, sasa angebishaje kama mtoto sio wake. Kwisha habari yake. Kuweka mazingira vizuri kesho hakunitafuta wala nini nikamtegea siku nzima kimyaaa. Namna gani tena baba kijacho huyu. Nilinunaaaa. Nikawaza kweli wanaume bila ndumba na samasoti hawaendi kabisaaa, la maana niende kwa kugwi sijui shangingi mstaafu whatever anipe mawazo, huu sio mda wa kucheka na kima. Kama ameweza kumbambika mtu mitoto mi 3 haka kamoja hakatomshinda kunisaidia mimi kumbambika yule Afande.
Nimetua kwa kungwi, sikumficha chochote nikamueleza A to Z akanisikilza, akasema sio kesi, hatushindwi. La maana muanze wewe, kumbuka wewe ndo ulie mkoseaga zamani. La maana we muanze tu kwani nani kamuanza nani umri wenu huo haina maana wala nini. We muanze tu. Nikakubali. Ila nimefika kwangu roho ikagoma kabisaa kumuanzaaa. Nikalala.
Usikuuu kabisaa saa 5 ndo anapiga Afande, wala sikumlaumu, nikashukuru hata kapiga, akaomba msamaha alikuwa kwenye mission muhimu hakuwa na simu, moyoni nikajua tu alinipa ubavu yakamshinda, ikabidi anianze. Basi namchombeza, jana usiku ilikuwa tamu sanaa, njoo tenaaa. Anaruka viuzi tu Afande yule. Nikamwambia basi nije hapo kwako mimi, bado anaruka tu viunzi, ila sikuwa na shaka sanaa mara moja ilitosha kumpa ubaba wa kumpakazia.
Nikasubiria tu 2 weeks, akajichanganya twende dinner tena, nikabeba kipimo changu it is better sooner than later. Tumekaaa tu nikamwambia kuna good news, akashangaa zipi tenaaa dear? Nikampa kipimo. Akapagawa kama dakika 2 au 3, baadae akajitia kufurahiaaa. Sasa sikujua ndo nishafanikisha kumbambikaaa au ndo ana buy time afanye upelelezi wake, ila nikajiaminisha hawezi jua maana tunaojua ukweli ni mimi na kungwi tu, na kungwi hawezi kuniuza somo wake hata iwejee atakuwa hajafundwaa.
Basi jioni hio ikaisha kwa magazijuto hivo hivo. Mda wa kuondoka akanisindikiza mpaka ndani kabisaa, nataka kumpa mambo akachomoa kabisaa, akadai kesho ana kazi inabidi awahi kuamka, na sikukubali kirahisi nikawambia na mimi najisikia vibaya siwezi kulala peke yangu, navojisikia Mungu tu anajua. Mama kijaa tenaaaa. Akapata mawazo. Akakubali kulala pale.
Ila ndo akashinda na CNN kwenye kochi, mi nimelala chumbani mpaka saa 8 naona mtu haji kabisaa, sikukubali kirahisi inaitwa Die hard nikamfata kwenye kochi nambembeleza tukalale, anadai kuna habari za muhimu anangojeaaa. Na mimi nikamlalia pale pale kwenye kochi, basi kila saa najikuna mmbu. Akaingiwa imani, akasema basi twende chumbani kwenye neti. Chezea mimi nyie. Chumbani kaingia na sarawili zake, maana sio suruali kajibanza mwisho kabisaa. Mi nikajitia kulala. Nageuka geuka mpaka nikamfikia kumlaliaa, kumpima tu. Ikabidi anikumbatie tenaaa angefanyaje sasa, na joto lilishamgusaa.
Aubuhi akaenda kwake, mi nikaenda kazini. Mchana akaniuliza unaendeleaje mama Kija. Nikamjibu sijambo, ila Kija leo hana neo katuliaaa. Jioni nilikuwa nimechoka so sikutaka kumbanaa sanaaa. Kwanza ubaba wenyewe fekerooo, nikaamua tu nitalala peke yangu nitafakari mustakabali wa hili picha nalolicheza mwisho wake utakuwa nini. Amara nilikuwa sijamwambia wala sikutaka kumwambiaaa kabisaa. Na nisngekuja kumwambi kamwe labda sijui kitokee nini apate hizo hela na ziwe nyingi sanaaa.
Saa 3 nimelala, nasikia mtu anagonga, nikajua kungwi, kufungua Afande kaja na Pajamas. Nikafungua fastaaa mlangooo, namwambia nilijua leo hujii. Afande anasema ungeumwa usiku ingekuwaje, nilienda kwa Dr akasema wiki 8 za mwanzo ni ngumu sanaa kwa baadhi ya kina mama. So nikawaza unaishi peke yako ukiumwaa nani atakusaidia. Mi wala sikujikawizaa nikaanza kumpa mate Afande, nimefanyia mautundu kwenye busu hilo mpaka nikamtia nyege ila afande mgumu yuleee sijapata ona.
Usiku nimemchokoza chokoza wapii anachomoaaa, mwisho nikamwambia tu bwana baba Kijacho mimi nina nyege, hali ya mama kijacho inaleta nyege mbaya sanaa sasa unanisaidiaje, na njia inabidi tutanue. Hahahaaa! Mimba ya wiki 6 inatanuliwa njia. Nikaendelea kumfanyia utundu pale akaingia kingi, basi usiku mzima tunapena mambo. Japo hajui mambo kama Amar ila nae ana ufundi wake na utamu wake.
Tumelala wote wiki nzimaaa. Mama kijacho tenaaa. Wiki ya 2 akaniambia hajisikii vizuriii kulala nyumba ya mwanaume mwenzie, analala kimachale machale ana hisi mda wowote Amar ataufanyia ambush, hivo kwa usalama wetu na mtoto nihamie kwake. Kwake huko ni kota za poilisi za Obay lakini, kule Amar hawezi kuja mda wowote, hatdhubutu na ujasiri wake wote. Kiukweli sikupenda kwanza hamna pool kama hapa, pia hamna AC, hapa ni pazuri hatariii. Nikamgomea. Akasema haji tena kulala pale, ila nikijitafakari nikiona vipi niende kota namba flani, akaiacha funguo.
Kungwi ndo wa kwanza kunitisha wewe cha masihara hio hali sio ya kukaa peke yako, shauri yako, na maneno kibao. Hakuja wiki nzima, ila simu anapiga, na anakuja ofisini kuniona kila siku. Mwisho nikamwambia nimekubali kuhamia kota ila itabidi uniwekee Ac kwa kweli joto la Dar baya sanaaa. Akafurahiii. Nikachukua nguo nikaenda. Kungwi akaja kunisalimia anasisitiza be nice to him. Be very nice to him, kuliko hata ulivokuwa nice kwa Amar.
Anasisitiza ishi kama mkewe, kusiwe na uwazi, mpikie, mpe mambo kila mda utao wezekana, kusiwe na ratiba, chance lolote likitokea mpe mambo tu bila kujali nini wala nini. Yaani kuwa mkewe kabisaa simamia show, kuanzia misosi, mavazi, kila kitu, aone tofauti tangu uwepo na kabla hujakuwepo. Usimuulize mambo ya kazini kwake atahisi Amar kakutuma umpeleleze. Kungwi wako nipo karibu kukushauri.
Kiukweli kota palinishinda na kunikeraa, kwanza miundo mbinu ilikuwa haifaiii kabisaa. Pili umbea wa majiranii, tatu it was so local and i liked finer things in life. Siku hio hio ya kwanza kinyume na kungwi alivoelekeza nikayatibuua kwa kumngangania turudi kule. Alikuwa mkali kama pili pili. Nilimwambia tu kwanini anakuwa mbishi tusiishi kule kwenye appertments. Akawa mkali, mimi haya ndo miasha yangu, kama unanipenda na tunazaa lazima ujue haya ndo yatakuwa maisha yetu kila siku. Kama siyawezi bora nikajitoa mapemaa, yeye sio muhalifu kama Amar na hana hela kama Amar za ku afford place like that. Mishahara ya serikali sio mikubwa wala hapkei rushwaaa. Pouvu lilimtoka ndoo nzima.
Akahama na chumba na kuniachia master. Kiukweli maisha yalikuwa magumu sanaa kwangu. Amar nae nikawa simpati kwenye simu, wala sijui alipo. Akanuna wiki nzima, sipiki sifanyi chochote, jioni na oda zangu Pizaa nakula nalala. Nae tunasalimiana tu anaingia chumbani kwake anajifungia. Kidogo nirudi kwangu Masakai. Kidogo. Nikawaza ukute AMar kafa au yuko jela itakuwaje kodi ikiisha, nikajishusha siku hio karudi kajifungia chumbani kwake, nikaenda kumgongea naomba ukae na mimi sijiskii vizuri. Kweli nilikua sijiskii vizurii
Basi akaenda kunichukulia panadol, homa ikapoa, Panadol alizifata mbaliii sanaa, karudi nimekunywa namwambia na hamu ya samaki wa kuchoma wa kawe. Akauliza mbona hukusema wakati nafata panadol. Akaamua kuniambia vaa twende, nikasema nimechoka kaniletee. Akaondoka kanunaaa sio kidogo. Kumleta yule smaki harufu tu ikanichefua, nikamambia siwezi kumla. Akafokaaa sio kidogo, nikawaza nikamla hivo hivo kibishi, kipande cha 3 nikaanza kutapika, tapika na wewe. Akajisikia vibaya. Mi nikaend akuoga kwanza, nikakuta kafuta amatapishi yote. Akakoroga na uji. Nikanywa ule uji, nikaenda kulala. Akaja kulala kule kwetu, aniangalie homa usiku kucha.
Kesho tukawa tuko poa, kungwi akaja na kunilaumu kwa kutomtiii mafunzo yake. Akanisiminga hatari. Siku hio nikapika, akaja akala, tukawa tuko poa, mpaka jioni akawa yupo kwenye Tv, mafunzo ya kungwi kichwani ya motooo. Akiwa kwenye tv we vua chupi yako huko huko kaka chumbani au jikoni utakua wewe, unaenda pale unamkalia unamgusisha mkono humu ndani kufuli hamna lazima akupe mambo. Na kweli nikamkuta kwenye tv, nikashindwa kumkalia direct, nikaa kwanza pembeni, kukusanya nguvu na kumpima temperature. Nikaona iko vizuri nikaanza kwanza kumbusu busu nikaona anaelekea, wapi nisimkalie fastaa, na kumgusisha mikono, kwenye gauni ajue duka la mzungu li wazi kabisaa leo. Kungwi hakoseiii. Akadataaa. Pale pale kwenye kiti akanipa mambo ya hatari, basi kupania nampa viuonoo, na tumbo kikishaanza kuwa gumu, anakataza utamuumiza mtoto hivi hivi tamu. Alidataaa. Usiku tena kingine kitandani, nikamwambia natka niache kazi. Ikatibua mambo yoteee.
Uache kazi mtot tutamleaje atakula nini? Mimba sio ugonjwa, Mimi sio Amar, hapa utafanya kazi mpaka utafurahi, watot wa 3 utazaa na kazi utafanya. Maisha magumu, mishahara midogo usifanye kazi vipi sasa. Akanuna akaenda chumbani kwake. Kesho sikununa na mimi, nikaamka asubuhi nikampikia chai nzito, nikampasia nguo, alivoamaka akajistukiaaa, akaanza kuongea. Kungwi huyo, mkibishana sio ndo unanunaa, wewe mwanamke unajushusha wanaume wepesi, ukishuka nae anashuka.
Kazini ananiuliza unaendeleaje. Nikamwambia naenda kwa Dr wangu leo. Akadakia nakuja kukupeleka, inatakiwa tuwe tunaenda wote. Tobaaaaaaaaaaaaa. Nikachoka mwili naroho. Nimelikoroga. Kwa Dr kule mimba ni wiki 12 huku Afande anajua mimba ina wiki 8 au 9. Mmmmmh kimbembe. Nafanyaje mie. Dr. mwenyewe muhindi yule professional huwezi hata kumpa hela kumfunga mdomo. Tobaaa.
ITAENDELEA KESHO SAA 10 JIONI