Weeeekeeend njeeeeeeema!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Weeeekeeend njeeeeeeema!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Jul 16, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,403
  Likes Received: 5,678
  Trophy Points: 280
  [h=3]Miezi Miwili Mara Moja![/h]

  [​IMG]
  SWALI
  Ndoa yetu ina miaka 4 na tunafanya tendo la ndoa mara moja kwa miezi mwili. Kila siku usiku mume wangu husema kwamba amechoka na hawezi tendo la ndoa kwa kuwa alikuwa na siku ngumu hata hivyo nafahamu aina ya kazi alikuwa nazo mchana kwa kuwa tunafanya kazi pamoja.
  Kinachokishangaza ni kwamba anakusisimka sana akimuona mwanamke mtaani hasa kama anavutia.
  Ninachojiuliza kwa nini mara zote anasema amechoka kwangu na je nifanyeje ili awe na hamu na avutiwe na mimi?
  Mama E
  <!--[if !supportEmptyParas]--> <!--[endif]-->
  JIBU
  Swali lako ni la msingi sana.
  Tuanze kwanza na suala la “nifanyeje ili awe na hamu au nimvutie” ingawa unapenda sana mume wako awe na hamu na wewe jambo la msingi ni wewe kukaa chini kwanza na kujichunguza vile unajiona na kujisikia wewe mwenyewe.
  Wewe mwenyewe unajionaje, unajiamini vipi na unavyovutia, unavyopendeza? kwani kama wewe mwenyewe hujioni unavutia basi inakuwa ngumu sana mume wako kuona unavutia.
  <!--[if !supportEmptyParas]--> <!--[endif]-->
  Mahusiano mazuri kimapenzi na mume wako hayaji tu kwa kuwa mnafanya business pamoja bali kwanza wewe mwenyewe unajisikiaje au unajiamini vipi kuhusiana na mwonekano wako.
  <!--[if !supportEmptyParas]--> <!--[endif]-->
  Hatua inayofuata ni wewe na yeye kuanza kuongea pamoja kuhusiana na suala la mahusiano ya kimapenzi katika ndoa yenu.
  Ni kawaida kwa wanandoa kuwa na up na downs zinazohusiana na tendo la ndoa hata hivyo kunapokuwa na ukame wa kimapenzi au ukaribu wa kimapenzi ni muhimu kwa wandnoa wenyewe kukaa chini na kuanza kujadili wapi pamepungua au kitu gani kinakosekana na si kuanza kulaumiana bali kila mmoja kuwa wazi kuelezea na kusema kile anahitaji katika mahusiano ili moto wa mapenzi urudi tena.
  <!--[if !supportEmptyParas]--> <!--[endif]-->
  Je, kama mwanamke unahitaji mume kuwa karibu na wewe kwa kukubusu mara kwa mara ua kukukumbatia mara kwa mara?
  Je, unahitaji kushikwa mikono au mwili wako na mume wako mara kwa mara?
  Je, kuna migogoro nje ya chumbani au kutokuelewana au una hasira kutokana mambo fulani fulani kitu kinachofanya mume wako kuwa mbali na wewe kihisia?
  Nk
  Ukijiuliza hayo maswali na mengine na kukaa na mume wako kujadili mnaweza kufika Mahali kila mmoja akafahamu nini wajibu wake ili kurudisha moto wa mapenzi chumbani kwenu.
  Mawasiliano yaliyo wazi na yanayomruhusu kila mmoja kusema kile anahitaji ndiyo njia sahihi ya kurudisha ukaribu wa kimapenzi upya katika ndoa.
  <!--[if !supportEmptyParas]--> <!--[endif]-->
  Baada ya kufahamu hatua tatizo lipo wapi weka plan na kuanza kufanyia kazi na hakikisha kila mmoja anakuwa positive kwa mwenzake bila kulaumiana.
   
 2. First Born

  First Born JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 5,315
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Unajua mumeo anapenda wanawake wanaovutia basi na wewe ufanye jitihada zote uvutie ali akutamani.
   
 3. sinafungu

  sinafungu JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2011
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 1,406
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  penzi la mumeo kwako limeanza kuota miguu, harakisha usijepata mshituko. kaa na mwenzi wako mjadili hali hiyo kwa kina zaidi
   
 4. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  mtege upyaaa! tatizo watu wakishaoa au kuolewa wanaona kutegana upya ni ujinga au kuna ile dhana huyu si wa kwangu tuu huyu hakuna cha ziada niweze kufanya. Lugha nzuri, sio kununa nuna tuuuuuuuuuuuu!!! kuwa msafi, idea nzuri nzuri, unyenyekevu nao unasaidia km na wewe unakuwa baba ndani ya nyumba basi jamaa alazima umkifu tuuu
   
 5. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  kwa kusema ukweli, unafiki pembeni, siku hizi Pdidy unaleta threads za ukweli kaka, kama ni kiwango basi upo form ya juu mkubwa, umeifanya wik'end yangu ipendeze!
  Kwa kumshauri huyo mwanamke inabidi afanye fasta kuweka mambo safi kuepusha yasiyoepukika huko mbeleni!
   
Loading...