Wee mchungaji acha kutukera wenzio

Mpo wanaJF.

Leo nina kero kubwa sana kutoka kwa mama mchungaji yule.

Tuna kikundi cha wanawake mtaani kwetu cha kusaidiana katika mazuri na mabaya na pia tunakopeshana japo hatuna kibali rasmi kutoka kwenye mamlaka za serikali zinazoruhusu kukopeshana.

Mama mchungaji huyu ni mwanachama mwenzetu. Anachokera huyu dada yaani analazimisha members wote tumumchukulie kama "mama mchunguji" wanavyomchukulia kule kanisani kwake SDA.

Mama mchungaji hatoi michango yake ya ada ya michango mingine ya lazima kwa wakati, akikumbushwa anaanza kufoka na kutushangaa kuwa yaani hatuoni aibu kumdai tumeshindwa nini kumlipia hadi asomeke ana deni!!! (sijui nani amlipie kwa usawa huu wa JPM).

Mama mchungaji sie wengine tukiwa na sherehe siku za Jumamosi kwa imani yake hawezi kuhudhuria lakini yeye akiwa na sherehe yake siku ya Jumapili wanachama wanaposhindwa kuhudhuria kwa kubanwa na shughuli za kanisani ananuna na kutishia kusitisha uanachama kwa madai kwamba watu hawapendani na hawashirikiani kwa dhati wameshindwa kwenda kwake siku ya Jumapili na hali ni siku ya mapumziko!

Mama mchungaji akiomba mkopo kama akiambiwa asubiri pesa ziko kwenye mikono ya wanachama wengine hawajarejesha bado, anasema, "hivi mmeshindwa kunitafutia kwa namna yoyote ile hiyo pesa ninayoitaka nikamalize shida yangu".

Pale kwenye kikundi tuna wanachama ambao wana abudu pamoja na mama mchungaji, wakiona ana mapengo kwenye ada yake wakimlipia siku wakimdai, anawashangaa utasikia kwa mfano "hata wewe Miss Natafuta unadiriki kunidai?!!

Nyie wa mama mchungaji na wa mama askofu, jirekebisheni kama mmeamua kuingia kwenye hivi vikundi vyetu vya "kimataifa" basi mhakikishe mko tayari kutimiza na kufuata sheria, kanuni, sera, taratibu na masharti yote ya kikundi husika, kama hamuwezi undeni vikundi vyenu msitukere sie.

Mbaya zaidi tukimaliza vikao akiona sie wengine tunaagiza "kahenken" ana maindi.
Atakutana na Mwenye maradhi amshughulikie...
 
hahahaahah ya kaisari mpe kaisari [HASHTAG]#mama[/HASHTAG] mchungaji! na usiwaonee wivu wa "mataifa" wakiagiza [HASHTAG]#desperado[/HASHTAG] zao !
 
hahahaahah ya kaisari mpe kaisari [HASHTAG]#mama[/HASHTAG] mchungaji! na usiwaonee wivu wa "mataifa" wakiagiza [HASHTAG]#desperado[/HASHTAG] zao !
hahahaahahah, upo rafiki yangu? nakwambia kuna watu wanapenda kuudhi wenzao!! eti tuishi kama wote ni SDA wakati wengine tumebatizwa kwenye vimaji vya kumiminiwa kichwani kidogo tu
 
hahahaahahah, upo rafiki yangu? nakwambia kuna watu wanapenda kuudhi wenzao!! eti tuishi kama wote ni SDA wakati wengine tumebatizwa kwenye vimaji vya kumiminiwa kichwani kidogo tu

hahahahah nipo shost !aisee naielewa sana hyo situation !siku nyingine mpeni makavu !na wana madeko hao wamama wachungaji !uwii wananyenyekewa mnooooo !mama angu anapelekaga had sukari [HASHTAG]#kwamchungaji[/HASHTAG] wao!
usishangae anavyolalamika hvyo ndo wamelelewa namna hyo km wafalme fulan !

mie siwez jaman !anywys mama mwana kondoo wa Mungu atoe marejesho fresh aache kuremba !siku mnywee hata ka "k vant" mbwatukie
 
hahahahahahah
 
Huku kwetu kuna Mama mchungaji wa kanisa la Efatha yeye anataka ata deki kufuliwa nguo zoote anataka wamfanyie inakeraje akina mama mchungaji
 
Ndege wanaofanana huruka pamoja.. nyie hamfanani kwa hiyo lazma msiendane tu...
Yeye sasa kwa kuwa ameamua kuwa na sisi afanye yetu, asilazimishe kufanya mazingira ya kule kanisani wanapomnyenyekea!!! sisi huku ni kufuata taratibu za kikundi tu, hakuna cha zaidi
 
Huku kwetu kuna Mama mchungaji wa kanisa la Efatha yeye anataka ata deki kufuliwa nguo zoote anataka wamfanyie inakeraje akina mama mchungaji
Basi itakuwa ndio tabia yao, maana hata huyu naona kama ikiwa kuna msabato mwenzio labda alimlipia ada akimdai utamsikia "yaani hata wewe Yukina unanidai?!" hahahahahah
 
hahahahah nipo shost !aisee naielewa sana hyo situation !siku nyingine mpeni makavu !na wana madeko hao wamama wachungaji !uwii wananyenyekewa mnooooo !mama angu anapelekaga had sukari [HASHTAG]#kwamchungaji[/HASHTAG] wao!
usishangae anavyolalamika hvyo ndo wamelelewa namna hyo km wafalme fulan !

mie siwez jaman !anywys mama mwana kondoo wa Mungu atoe marejesho fresh aache kuremba !siku mnywee hata ka "k vant" mbwatukie
Yaani kama mie ndio ananionaga "shetwani" kweli maana nikianza kunywa akianzisha maneno yake, na mjibu kwa ufupi kuwa "imani yangu ya kanisa katoliki inaruhusu kunywa dada"
 
Yeye sasa kwa kuwa ameamua kuwa na sisi afanye yetu, asilazimishe kufanya mazingira ya kule kanisani wanapomnyenyekea!!! sisi huku ni kufuata taratibu za kikundi tu, hakuna cha zaidi
Sasa inakuwaje mnashindwa kumuweka kwenye mstari? hamna uongozi wa kikundi? mambo kama hayo ndo kiongozi anachukua nafasi yake kuwaweka members wote kwenye mstari mmoja.. na ndiyo maana miongozo na taratibu zimewekwa.. vikundi vinatakiwa kuwa vyombo vya kutatua kero mbalimbali, siyo kuleteana makwazo.. tatizo ni kuwa huyo mama mchungaji keshazoea hayo maisha.. na kama kawa mama mchungaji kwa miaka mingi tayari anaona kila mahali anatakiwa kuchukuliwa hivyo hivyo.. na wale wamezoea kupewa siyo kutoa.. sasa kazi kwenu
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom