Wedding Anniversary

Nashukuru sana rafiki yangu kwa haya maombi yako, naamini Mungu atatujalia yote uliyotuombea.... Asante sana

Congratulations my Dearest, Mungu akutangulie kwa kila jambO wewe na familia yako, najisikia amani ninaposikia mtu anaongelea na utamu wa ndoa pia, sio kila siku majuto/manung'uniko goodluck FP.
 
pacha mimi wakati BAK anajipanga kutuwekea wimbo a shania twain na diana ross naomba mimi nitunge shairi kwa ajili ya dada yetu wa moyoni @fp
 
Last edited by a moderator:
Kumi na tatu si hoja,kweli unastahili,
Ya kuwa pamoja,ya mgosi na kamwali,
Mmevumilia shida,na iliyokuwa ngumu hali,
Unastahili hongera.

Mwaka ulioolewa,usisahau maishani,
Mwenzio alinogewa,akakuweka ndani,
Mengi ulizushiwa,kuwa si mwema mwandani,
Unastahili hongera.

Itaendelea...
 
Mungu azidi kuwabariki katika ndoa yenu ya miaka 13 mkae pamoja kama mlivyoagana mpaka mwisho............................Hongera sana dada FP ni upendo wa Mungu ndio ulifanikisha yote basi hatuna budi kumshukuru
 
Last edited by a moderator:
Nilikuita kamwali, labda ulikuwa busy. Nalisubiri kwa hamu hilo neno zuri. asante sana

Mungu mebariki ndoa ,kwa upendo uso na doa
baraka alowapatia,milele dumu ameitoa
pokeeni kwa mapana ,baraka zake Rabana
MWANZO UKAWE MILELE,TISA OKTOBA ILEILE

Mapenzi mlopeana ,yadumu bila hiyana
leo milele kama jana,mejalia Maulana
nidhamu aloiona,sipindishe akanuna
MWANZO UKAWE MILEL,TISA OCTOBA ILEILE

Kwa busara mlizopewa,mlijenge na kulinda
penzi lataka pepewa,kupendwa kwake kupenda
kulikinga nao chawa ,vya watu wenye kuwinda
MWANZO UKAWE MILELE,TISA OCTOBA ILEILE

Watoto mlojaliwa ,kwao nyie ni vinara
wapeni mahitajiwa,kwao wakawe ishara
upendo wenu wa ndowa,kwao ukawebendera
MWANZO UKAWE MILELE,TISA OCTOBA ILEILE

Rafiki wako kipenzi,hajajuta kuwa nawe
wake mkewe mpenzi,ajivuna kwa wenziwe
litunze na lenu penzi,wengine mu mfanowe
MWANZO UKAWE MILELE,TISA OCTOBA ILEILE.
 
Ni raha iliyoje kuona watu wanafikisha miaka kumi na tatu( 13) ya ndoa,naamini mmepitia mengi hadi hiyo miaka 13 hapa namshukuru Mungu kuwa na nyinyi kwani ukiona machafuko jua mmemkaribisha shetani ila yenu Bwana amewalinda mmefikia hapo nawatakia miaka mingi yenye furaha.
Mkumbukeni Bwana kwa kila mtendalo kwani He is Alpha and Omega

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
chezeya wangoni walimu wa kiswahili wewe!nimeipenda hii!
 
asante sana mlongo wangu.......... mnanipaje raha sasa! wangoni oyeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!
 
what would I have done without you mlongo wangu? usengwili sana.
naomba ni-copy hili na la kaka Mzee Tupatupa, nimpe na shemeji yenu aone watu wanavyotupenda
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…