frankgalos
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 223
- 100
- Je, unapenda kutengeza kitu chako ambacho umekitolea jasho?
- Je, unapenda kujifunza technology mbalimbali hususani za kompyuta?
- Je, unapenda kujua jinsi website zinavo fanya kazi.Basi hii thread ina kufaa?
Habari marafiki?
Katika hii course ningependa kuelekeza jinsi ya kutengenza website na iliyokua na ubora wa hali ya juu, ambayo inyoweza kuonekana na kila kifaa ikiwemo simu na Kompyuta.
BAADA YA KUJIFUNZA HII TEKNOLOGIA UTA PATA NINI.
1. Baada ya kujifunza hii lugha utakua una uwezo wa kutengeneza page yako amboya una weza kuweka taarifa zako.
2. Utaweza kuweika page au website yako online ili iweze kuonekana na kila mmoja.
3. Utaweza kupata ujuzi wakuandika html na css code.
4. Utaweza kua freelancer wa kudesign pages za aina mbalimbali.
HII COURSE IME MLENGA NANI ?
Hii course ime mlenga mtuambaye ajui chochote kuhu website wala code ila anachojua ni ana kompyuta na ana itumia kwa matumizi ya kawaida tu.
Hii course ime mlenga mtu ambaye anae itaji kujua nini maana ya html na css na nini maana ya website.
VIFAA UNAVO TAKIWA KUWA NAVYO
1. Uwezo wa kutumia kompyuta.
2. Uwe na kompyuta.
3. Uwe na notepad ya kompyuta au notepad++ kwa kudownload.
UTANGULIZI WA HTML.
Nini maana ya HTML ?
HTML ni lugha inayo eleza nyarakaka za mtandao (web documents) au kurasa zinazo patikana mtandaoni (web pages).
· HTML inasimama kama au kirefu chake ni HYPER TEXT MARKUP LANGUGE.
· Nyaraka za HTML zina vitambulisho vya HTML (html tags).
· Kila vitambulisho(tag) vinaeleza nyaraka zilizomo.
Mfano wa html.
<!DOCTYPE html>
<html>
<head>
<title>Ni website yangu ya kwanza</title>
</head>
<body>
<h1>Karibu katika page yangu</h1>
<p>katika page hii nitaeleza kuhusu jinsi ya kutengeneza website</p>
</body>
</html>
MAELEZO YA MFANO.
· !DOCTYPE inaelezea aina ya nyaraka (document) nahiyo ni html.
· Kati ya nakala <html> na </html> inaelezea nyaraka (document) za HTML.
· Kati ya nakala <head> na </head> inaeleza taharifa kuhusu nyaraka (document).
· Kati ya nakara <title> na </title> inaeleza (title) kichwa cha nyaraka(document).
· Kati ya nakala <body> na </body> inaeleza kurasa inayoonekana (visible page).
· Kati ya nakala <h1> na </h1> inaeleza viongozi (heading).
· Kati ya nakala <p> na </p> inaeleza aya (paragraph).
Kutumia maelezo haya browser inaweza kuonesha nyaraka na viongozi (heading) na aya (paragraph).
HTML Tags.
Tags ni vitambulisho.
HTML tags ni maneno (keywords) au (jina la vitambulisho ) tags name lililo zunguukwa na pembe mabano (angle brackets).
<jina la kitambulisho> yaliyomo </jina la kitambulisho>
· HTML tags kwa kawaida zina kuja kwa jozi(pairs) kama <h1> na </h1>.
· Tag ya kwanza kwenye jozi(pair) ni tag ya kuanza nay a pili ni yaku funga.
· Tag yakufunga inaandikwa kama ya kufungua ila ina wekwa alama ya / kabla ya jina la kitambulisho aut tag.
WEB BROWSERS.
Kazi ya web browsers ni kusoma kusoma nyaraka za HTML na kuzionesha.
Browser hai oneshi html tags lakini inazitumia ili kuonesha nyaraka (document).
Mfano hapo juu utaonekana kama hivi.
Karibu katika page yangu
katika page hii nitaeleza kuhusu jinsi ya kutengeneza website
Browser in onesha sehem ya <body></body> tu.
Huitwaji wa <!DOCTYPE>
Huitwaji wa <!DOCTYPE> unasaidia browser kuonesha kurasa za mtandao (Web page) kuonesha sawia.
Kunaaina ya nyaraka mbalimbali mtandaoni.
Kuonesha nyaraka sawia,browser inaitaji kujua aina na version.
Uitwaji wa doctype sio kesi nyeti (case sensitive),kesi zote zina kubalika.
Mfano.
<!DOCTYPE HTML>
<!DOCTYPE html>
<!DOCTYPE Html>
Uitwaji wa kawaida.
HTML 5
<!DOCTYPE html>
HTML 4.01
<!DOCTYPE HTML PUBLIC "-//W3C//DTD HTML 4.01 Transitional//EN" "http://www.w3.org/TR/html4/loose.dtd">
XHTML 1.0
<!DOCTYPE html PUBLIC "-//W3C//DTD XHTML 1.0 Transitional//EN" "http://www.w3.org/TR/xhtml1/DTD/xhtml1-transitional.dtd">
Kwenye course hii tutatumia HTML 5.
AINA ZA HTML | HTML VERSIONS
Version
HTML
Year
1991
Version
HTML 2.0
Year
1995
Version
HTML 3.2
Year
1997
Version
HTML 4.01
Year
1999
Version
XHTML
Year
2000
Version
HTML5
Year
2014
Itaendelea ....