Nasaha kwa web developers

Jul 21, 2022
41
60
1. Kabla bado unajifunza, pendelea kupiga codes kwa mkono, usitumie WYSIWYG apps kama DreamWeaver mapema. Zitakusababishia kutoelewa HTML, CSS codes kwa ukamilifu au kwa haraka, hivyo tumia notepads kama Notepad++, Atom, Geany na zinginezo.

2. Usitest website yako kwenye browser moja pekee kwani mtumiaji usetegemee atakuwa na browser kama ya kwako. La sivyo kama website yako ni special kwa browser maalum, weka warning kwenye website yako kum-prompt mtumiaji kwamba lazima atumie browser fulani (mf. Chrome). Hii pia inaweza kuandaliwa programmatically kwa kutumia "browser user agent" detection code (wataalam wanajua).

3. Usikimbilie kutumia API au features mpya saaana lakini hata hivyo usitumie API za zamani zilizofikia hatua ya kuwa "unsupported" au "deprecated". Tarajia kwamba watumiaji wengi wa website yako watakuwa na browsers za zamani kidogo hivyo ukitumia API mpya baadhi ya features zitakuwa hazikubali. La sivyo kama tulivyoona awali, weka prompt ya kusasisha (update) browser.

4. Watu wengi sasa wanatumia simu kufungua website mbalimbali, hakikisha website yako inakaa vizuri kwenye PC na Simu. Ifanye iwe na flexible layouts. (Wapo wataalam humu wanajua vizuri waulizieni). Hata hivyo kama website yako labda umetarget watu au office maalum ambayo unajua watu watatumia PC tu au simu tu sio mbaya kuweka layaout (view) ya aina moja.

5. Kama website yako ina matangazo, kuwa na busara, usiweke "click-jacking au fake-redirection" yaani usilazimishe watu walibonyeze tangazo bila kukusudia ilhali wanataka kufanya kitu cha maana kwenye hiyo link au button. Madhara yake ni kwamba watu wengi watakereka na website yako na kusababisha waweke AdBlocker, pia baadhi ya AntiViruses zinauwezo wa kublock websites zenye tabia kama hizi automatically.

6. Usifanye website yako iwe kama website zaidi ya moja kila page. Yaani usifanye kila page iwe na muonekano tofauti >80% kana kwamba ukifungua page nyingine ni kama umetembelea website nyingine. Kuna baadhi ya vitu havitakiwi kubadilika katika website yako, mfano "menu bar" na wakati mwingine hata background au font, isipokuwa tu kama unasababu ya kufanya hivyo... yaani kama website yako in dhima zaidi ya moja tofauti.

7. Usiiletee uzito website yako ikawa inaload picha na script nyiiingi zisizo na maana. Kwa kifupi usijaze vitu visivyohitajika.

8. Kuna mengi mno, labda siku nyingine ... ila pia unapojisikia kusinzia lala aisee! usilazimishe coding ubongo ukichoka... relax and don't forget praying ...
 
Back
Top Bottom