Vizuri. Sasa nakushauri hata hiyo googlechrome na firefox pia na hiyo word 2010 navyo uvi-code usitumie software/program za wengine yaani googlechrome ui-code iwe imetengenezwa na wewe mwenyewe kadharika kwa firefox na word maana huko mbeleni utapata taabu sana KAMA UTAENDELEA NA HII TABIA YAKO YA KUTUMIA SOFTWARE ZA WENGINE WAKATI KU-CODE UNAJUWA.
Just because you can't code and just because you chose to take a shortcut and design using some software which still sucks (yeah because i have seen your work) don't just give people some sarcastic answers. Let this guy learn to create his own stuff, it will do him good. He chose to be different and do the right thing, let him be. Inakera sana unapomwambia eti na chrome, firefox, word atengeneze zake just because you don't want him to learn? C'mon dude show some class, there's a reason he chose to learn otherwise he could've just googled "software to create websites for me" and i am sure he would get a lot of answers from google.
If you can't contribute to his learning experience, just take some prozac and chill, you don't have to open your mouth and speak every time a post shows up on your screen, take a backseat old man and let the guy improve his craft.
huwa nashangaa kuona web designers/developers wengi wa hapa Tanzania wanavyofanya kazi zilizo na very low quality.
I think its about time na mimi nichangie kwenye hiii topic.
Avoid kutumia code generation tools,hizi tools zinazokuambia zinasimplify na kugenerate codes zina disadvantages nyingi utaishia kutengeneza websites zenye very poor code and very hard to maintain or modify.
for a basic website utahitaji kujua Heading (h1,h2,h3...),paragraphs (p),anchor (a),images(img),lists, muhimu sana, ukiona umefika pazuri jitahidi kutumia photoshop kidogo kuongeza uzuri wa website yako(<ul>) n.k.
Ukiwa na interest zaidi unaweza kutumia server side scripting languages
Kutengeneza website sio kazi ya kuchukua code generation tool au drag and drop kama unataka kufanya kazi professional ni lazima usome kwa bidii, unless kama unataka kutengeneza blog na website za mtaani zisizokuwa na maana kwa clients ambao wanajua wanachotaka kuna vitu vingi sana wanavyoangalia, search engine optimization,validation ya markup language unazotumia,cross browser compatibility(Internet explorer inahusika kwa sana),security (XSS,Sql Injection blah blah...).
Kazi yangu sio web designer wala developer lakini haya mambo nayafahamu kiundani sana na huwa nashangaa kuona web designers/developers wengi wa hapa Tanzania wanavyofanya kazi zilizo na very low quality.
Mkuu,
Nimeona nikuulize maswali kulingana na ulichoandika hapa, maana kama ndiyo huu ni muda mzuri kwako Kuchangia topic hii basi kwa hakika tutajifunza mengi kwani muda wote ulikuwa hapa na huchangii wakati kumbe una mengi tu ya kuchangia.
Mkuu hii topic niliiona asubuhi ila nikashindwa kujibu kwa maana nilikuwa natumia simu ya mkononi, napata wakati mgumu kuandika maneno mengi kupitia simu. Nitajaribu kujibu maswali yako kwa lugha itakayoeleweka vizuri kwa kila mtu kwa manufaa ya wote.
1.Websites zenye poor code na hard to maintain/or modify-hapa ninamaanisha hizi (nyenzo)tools zinazofanya code generation hutengeneza kitu chenye muonekana unaoutaka lakini nyuma ya pazia [namaanisha kwenye hizo code zinazofanya hiyo tovuti yako ionekane unavyotaka huwa ni matatizo na haziweizi kusomwa na binadamu kirahisi]
Je kuna umuhimu wa Code kusomeka kwa binadamu?
Ndio umuhimu upo, pale utakapotaka kuongeza features na kukutana na hizi code zilizongumu kusomeka utapata shida sana na kama hauna uzoefu kabisa na kuandika ama kusoma codes unaweza kujaribu kufuta mstari ama neno moja na kuangusha kazi yako yote.
-Mara nyingi Hizi code zinazokuwa generated kuna neno wanaloita 'Bloated' yani zinakuwa na vitu vingi sana na kuongeza ukubwa wa tovuti yako, Kwa mfano kuna hatua ya kuhakiki kama taarifa zilizoingizwa na mtumiaji wa tovuti ni sahihi kwa mfano barua pepe,jina nk kwa kutumia code generation ya Adobe Dreamweaver unaweza ukapata mistari 15-20 wakati unaweza ukaandika mistari miwili ama mitatu na kupunguza vile vitu ambavyo havihitajiki.
-Kwa anayefahamu hizo code nini kimeandikwa anaweza kufuta vile visivyohitajika na kuongeza vile anavyotaka na kuwa huru katika kazi yake, kwa yule atakayetegemea code kuwa generated anaweza kujifunga na kupata shida sana hivyo ndio maana nilishauri mtu aanze kujifunza jinsi ya kuandika code na kuachana na njia za mkato.
2.Katika swali la pili-Nilipotaja h1,h2,p,a,images...
-Webpage yani Ukurasa wa Tovuti unaundwa na Elements (Vipengele) ambavyo ni muunganiko wa tags (vitambulisho) vinavyoelezea Web Browser (Kiperuzi cha Tovuti kama opera mini,Internet Explorer n.k) jinsi ya kuonyesha ukurasa kwa mpangilio sahihi...Kiperuzi (Web Browser) husoma hivyo vipengele na kuweza kurudisha muonekano uliosahihi (interpret/tafsiri code).
-Kuna vipengele vingi sana na Lugha inayotumika (Markup Language) ni HTML katika kuunda kurasa za tovuti. Ukurasa wa tovuti ni kama ukurasa wa kitabu ama daftari lako na umegawanyika katika sehemu kama Kichwa (head) na mwili(body).
Kichwa huwa na taarifa muhimu kuhusu ukurasa huo kwa mfano Jina La ukurasa wako na vielelezo vya taarifa za tovuti yako. Mwili (Body) huu ndio hubeba maelezo yote kama maneno picha unazotaka zisomwe na mtembeleaji wa tovuti yako.
Mfano vitambulisho hufunguliwa na kufungwa, vitambulisho vya kufungua (opening tags) huanza na namna hii <herufi moja ama zaidi> na vitambulisho vya kufungwa huadikwa kwa namna hii </herufi moja ama zaidi >
-Kwa mfano < h1 > </ h1>Ukiandika neno lolote katikati ya vitambulisho vilivyofunguliwa na kufungwa utapata kichwa cha habari kikubwa mfano < h1 >TAARIFA YA HABARI < / h1> Hiki huonekana kama maneno yaliyokolozewa kwenye kiperuzi cha tovuti. Muunganiko wa vitambulisho vya kufungua na kufunga na hilo neno huunda kipengele kimoja.
Ukitumia vitambulisho kama < h2 >,< h3 >< h4 > unamaanisha vichwa vidogo vya habari, namba inavyozidi kuongezeka ndio udogo wa kichwa cha habari (katika muonekano na hata cheo katika ukurasa)
Ningependa kuoongelea sana HTML lakini itachukua sehemu kubwa sana na ninahisi kuna tutorial zimeshawekwa humu Jamiiforums kwa mfano https://www.jamiiforums.com/tech-gadgets-and-science-forum/429224-html-tutorial-3.html
- Vitambulisho vingine kama < p > Hiki ni kwa ajili ya kuandika aya (paragraph)
- < img >-Hiki hutumika kuweka picha.
- lists hutumika kuweka orodha ya vitu katika ukurasa (kama huu unaouona hapa kwenye ukurasa wangu)
Ninaamini zipo nyingi sana na hata kwa kutafuta google waweza kupata maelezo zaidi.
Mfano wa HTML code ni kama hiyo hapo chini.
View attachment 108529
Kama nilivyosema vitambulisho vipo vingi sana ila si vyote utakavyohitaji kuvitumia katika kuunda tovuti yako,jaribu kuangailwa vitambulisho vilivyopo katika tovuti nyingi utakuta ni aina chache zinazotumia,
Kuviona vitambulisho na vipengele
View attachment 108533
- tumia kiperuzi chako kufungua tovuti yoyote
- Bofya right click(kiswahili chake sikifahamu)
- Chagua sehemu imeandikwa view source code ama view page source (hutofautiana na viperuzi)
kwa njia hii ukiwa makini utaweza kujua ni vitambulisho vipi hutumika sana na jinsi ya kupangilia ukurasa wako.
3. Server Side Scripting Languages-hizi ni lugha (Programming Languages) zinazotumika kufanya manipulation (kucheza) na data katika upande wa server na kutuma majibu kwenye kiperuzi.
Hayo maelezo hapo juu yaweza kuchanganya kwa mtu asiye na ujuzi wa mambo ya computer.
Tuchukue mfano huu (nimejaribu kuelezea kwa njia rahisi sana na kuondoa baadhi ya maelezo ili kueleweka kiurahisi)
-Unapofungua tovuti kama Jamiiforums unatuma ombi lako kwenye kompyuta (Server) iliyobeba taarifa za Jamiiforums.
-Computer hiyo yani (Server) itatuma jibu kutokana na ombi ulilofanya kama ni kujibu topic ama kuanzisha topic mpya yenyewe itaangalia ni nini cha kukujibu, hiii yote huandikwa na wataalamu kwa kuiambia computer nini cha kufanya ombi linapotumwa.
-Lugha zinazotumika kuieeleza computer nini cha kufanya/kujibu pale ombi linapotumwa huitwa server side scripting language (Hutumika kutoa maelezo kwa upange wa computer iliyobeba taarifa za jamiiforums)
-Lugha hizi zipo nyingi sana kwa mfano PHP,ASP,JAVA-JSP,Python,Ruby, Sitoweza kuzitaja zote.
4. Adobe Photoshop-ni programu/software inayotumika kufanya mabadiliko ya muonekano wa picha/michoro.
Hii ni nyenzo muhimu sana kwa wasanifu wa website (Web Designers) kwa maana tovuti yenye muonekano mzuri huundwa na picha zenye mvuto mzuri na maumbo yanayoweza kumvutia mtembeleaji wako, kuna tools nyingine kama Gimp nayo ina uwezo mkubwa. Uwezo wa photoshop ni mkubwa sana unaweza kutengeneza picha na michoro mizuri sana wataalamu kama C6,Leh wameshaweka tutorial nyingi sana hapo nyuma kama
https://www.jamiiforums.com/tech-ga...8-tujifunze-photoshop-tembocard-mockup-2.html
https://www.jamiiforums.com/tech-gadgets-and-science-forum/317396-another-photoshop-tutorial.html
ambapo hata mimi niliweza kujifunza mengi kupitia kwao.
5.Search Engine Optimization-ni kufanya tovuti yako ipatikane kiurahisi katika search engine (hii ni mitandao kama Google.com/bing.com)
Jaribu kuingia Google andika neno kama Tanzania Forums, ya kwanza kutokea ni JF, hiii ina umuhimu gani?...Tovuti yako inapotokea mwanzo mwa matokeo inaongeza watembeleaji wapya wa tovuti yako, kama mimi ni mgeni katika forums na nilikuwa natafuta forum ya Tanzania kupitia google kwa namna moja ama nyingine ningejikuta nipo JF Hivyo Search engine optimization ni muhimu katika kuongeza watembeleaji katika tovuti yako.
6-Cross Browser Compatibility-Hii ni kuhakikisha tovuti yako inaonekana sawa kupitia viperuzi mbali mbali kwa mfano Internet explorer,Google chrome,Mozila etc. Usitengeneze tovuti inayoonekana kwa kiperuzi cha aina moja kwani hujui mtembeleaji wako atatumia kiperuzi gani, pale itakapotokea kiperuzi kimoja kinashindwa kuionyesha tovuti yako vizuri basi unaweza kuwa umejipotezea watembeleaji.
-Viperuzi vinavyosumbua sana ni Kama internet explorer 6-7 [hizi huwa na tabia ya kuonyesha muonekano tofauti wa tovuti ukilinganisha na viperuzi vingine vipya ila ni jukumu lako wewe designer kuhakikisha tovuti yako inaonekana vizuri]
7-Validation ya Markup-Hii ni kuhakiki kuwa HTML code zinazounda tovuti yako zipo sahihi na zinaendana na sheria zilizowekwa na mamlaka inayotoa sheria za tovuti W3C. Unashauriwa kufuatwa sheria zilizowekwa ili kuepuka matatizo kama muonekano tofauti wa tovuti kwenye kiperuzi kimoja na kingine (angalia namba 6)
8.Je nikitumia code generation tools nitaweza kufanya Search Engine Optimization,Cross Browser Compatibility na Validation Markup?
Hii inategemea na uzoefu wako na codes, kwa wale wajuzi hata akitumia code generation tool anaweza kurekebisha matatizo kama Cross Browser Compatibility na kuondoa Invalid Markup iliyotengenezwa na hizo tools bila kuharibu tovuti yake na hata kuweka Search Engine Optimization. Kama huna ujuzi na hizo code basi kufanya mambo haya itakuwa ni vigumu sana na hata kupelekea kuachana nayo kwa maana tovuti si inaonekana vizuri?, na Huu ndio mwanzo wa kazi zenye low quality.
-Utakapokuwa na ujuzi na code zako ndio utaweza kuwa na uhuru zaidi wa kufanya yote yaliyotajwa hapo juu kwenye swali.
Kwa kumaliza Mkuu japokuwa kazi yangu si web designer/web developer nina ujuzi wa kutosha kwa maana katika taaluma yangu nimeshayasomea haya mambo na kupitia juhudi zangu binafsi nikaweza kuendeleza ujuzi kwenye haya mambo, kwa sasa ninafanya kazi katika mambo tofauti lakini ninafahamu jinsi ya kutengeneza tovuti, ipi ni njia sahihi na nyenzo zipi zinafaa hasa kwa mtu anayeanza kujifunza.
Nikipata muda ninaweza kuweka tutorial hapa kuonyesha jinsi ya kutengeneza a simple attractive home page from scratch kwa kutumia HTML na CSS peke yake na kuonyesha jinsi hizo code zilivyorahisi kuziandika.
Nitakapokuwa nimekosea naomba nirekebishwe, Let us work together to Improve our society.🙂

Kama umeshajaribu dreamweaver nakushauri ujaribu pia software nyingine inaitwa ARTISTEER utakuwa na uwezo wa kudesign sites katika:
WEB DESIGN TEMPLATES/HTML
JOOMLA TEMPLATES
WORDPRESS TEMPLATES
DRUPAL THEMES
DOTNETNUKE SKINS na
BLOGGER TEMPLATES
Vyote hivyo kwa kutumia software 1.
CODE IS POETRY.
Kimsingi mimi sipo upande wako Fadhili Paulo
maana naona kama unamkatisha tamaa mshikaji.
unaonekana kama hutaki ajifunze.
Kama ungekuwa unatoa ushirikiano na msaada usingeweza kumwambia a code FireFox au google crome.
Kwenye IT hasa Software Development tunajifunza ku appreciate kazi za watu
ku-encourage new Developers siyo kama unavyojaribu kufanya wewe.
Kuhusu kazi mlizofanya wewe na Zech hapa siyo sehemu ya Mashindano lakini hata mimi nimevutiwa kutaka kujua kazi ulizofanya na nilichogundua ni alichogundua Zech. moja ya kazi yako amabayo nadhani utakuwa unaikubali zaidi amabyo hadi umeamua kuifanya sehemu ya Signature yako hapa JF ni http://maajabuyamaji.net/
Kazi nyingine ninayoijua ambayo kimsingi ilikuwa niifanye mimi ya website ya Hotel moja inaitwa nellyzinn. Hii ni Hotel amabyo ipo Mbezi na inamilikiwa na Prof.wa sheria kutoka OPEN UNIV Home | Nelly's InnNelly's Inn. Hii nayo ni moja kati ya website mbaya(Sorry for Discouragement)
... Una discourage watu usidhani hakuna watu wasiokujua kijana...we una copy templates(Siyo kitu kibaya kama we ni mtaalamu) na mwenzio anapiga from scratch acha kufanya hivyo kaka
yani hapo ujagusa php,java,jquery ila ukweli ni huu kuna software nyingi zinazolahisisha kazi kama dreamweaver,joomla,microsoft frontpage so tafuta
Asante sana mkuu naifanyia kazi hiyo naona hyo itansadia xana ngoja niitafute!