We Waziri Ambulance 50 tu nchi nzima? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

We Waziri Ambulance 50 tu nchi nzima?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fidel80, Jul 30, 2009.

 1. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Jana niliwahi kurudi home nikawa na angalia kipindi cha Bunge kupitia TBC kuna mbunge mmoja wa Ludewa nafikiri Mh. Mwalyosi alitaka apewe Ambulance katika jimbo lako kwani ipo moja kwa jimbo zima.
  Kuna waziri mmoja wa TAMISEMI alinichefua wakati anajibu swali hilo la mbunge Mwalyosi eti serikali imetenga fedha kwa ajili ya AMBULANCE 50 nchi nzima. Duh jamani hii inaonyesha jinsi gani serikali isivyo jali afya zetu yaani nchi nzima serikali imetenga ambulance 50 tu? Huu ni utani tena na dharau kwa wananchi na walipa kodi wao wanatembelea magari ya kifahari wanashindwa hata kuwathamini wananchi kwa angalau kuwapa AMbulance za kutosha kwenye mahospital akina mama wajawazito wanakufa kwa kukosa huduma za haraka.
  Jamani kutokana na hasira niliipasua TV yangu pale pale huu ni upuuzi sasa kodi tunalipa za nini? Kama huduma ndo kama hivyo tunapewa kwa kusua sua kuna hospital kubwa hata Ambulance hakuna wao wanabadilisha magari kila baada ya miaka 2 na wanajiuzia wenyewe kwa bei za kutupwa kwani mnafikiri hatujui haya! Si hata nyumba za serikali mmejiuzia wenyewe kwa bei za kutupwa sasa serikali inazidi kuingia hasara kwa kuwapangia nyumba.
  Kuna watu hawana uchungu na nchi hii yaani machungu mpaka yananipitiliza.
   
 2. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Inatia uchungu Aisee!
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Yaani mzee watu wote hapa tuna ndugu vijijini huko wanateseka huduma za afya zinasua sua yaani mpaka Ambulance nazo tunabaniwa hii too much. Wao wanakula bei gani mpaka washindwe kununua Land cruiser Hard top kupeleka kwenye mahospital nchi nzima?
   
 4. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #4
  Jul 30, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mkuu sasa inabidi ukanunue nyingine, manake walisema "hasira, hasara". Jamaa wakiugua wanaenda nje kutibiwa. Kama wako mahututi inakuja "Air ambulance" toka South Africa kuwabeba, unadhani wanawaza Mwananchi anayebebwa na toroli, mkokoteni, baiskeli nk kuwahishwa hospitali pale anapougua ama kushikwa na uchungu. Kweli inaudhi.
   
 5. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #5
  Jul 30, 2009
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Mie nilishangazwa waziri wa Afya pale aliposema kuwa eti mwaka huu wa fedha wamepanga kununua pikipiki za matairi matatu mia nne kwa ajili ya vituo vya Afya, Nikarudisha akili yangu miaka ya 80, enzi za mwalimu ambapo kila Health centre Tanzania ilikuwa na Ambulance tayari kupeleka mgonjwa wakati wowote, leo kila kituo cha Afya kinatakiwa kiwe na angalau daktari mmoja anayeweza kuhudumia emergency cases hasa za akina mama, lakini hawana vifaa na cha ajabu badala ya kununua vitendea kazi na kuwapa motisha hao madaktari ili waweze kukaa huko vijijini basi wao bado wanajikita kwenye vipikipiki, mungu awe nasi!
   
 6. Sura-ya-Kwanza

  Sura-ya-Kwanza JF-Expert Member

  #6
  Jul 30, 2009
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 561
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Yaani misuli ya mbavu! Sina.:D

  Pole! duh, hasira ndugu yangu...

  ...haya sasa 'Ambulance' ungetoa wapi kama ndio ungeumia na gilasi za luninga?

  Ndungu yangu chagua jimbo mapema kati ya hayo hamsini!

  hivi ule mradi wa bajaji umefikia wapi ;)
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Jul 30, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Jamani inatia simanzi sana hawa watendaji wa serikali mpaka najiskia kichefu chefu.
   
 8. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #8
  Jul 30, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  Hivi serikali ina mashangingi mangapi jumla kulinganisha na ambulance zilisopo nchi nzima?
   
 9. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #9
  Jul 30, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Hawa naomba walaaniwe kwa Mungu kwa nini wanatufanya hivyo sisi maskini?
  Wanataka twendelee kutumia local ambulance kama hii? Ndo fraha yao wanatuona sisi wajinga sana.
  Hii local Ambulance
  ambulance.JPG
  Sasa mpaka ufike Bugando mgonjwa si atakuwa amesha kata roho njiani.
   
 10. araway

  araway JF-Expert Member

  #10
  Jul 30, 2009
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 498
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45

  usiendeleee mkuu INAUMAAA!!
   
 11. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #11
  Jul 30, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Mkuu nimepoteza network hivi hivi kila siku wanahubiri Utawala bora nikimpiga vibao huyo waziri nitakuwa nimekosea??
   
 12. Komamanga

  Komamanga JF-Expert Member

  #12
  Jul 30, 2009
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 221
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi kuingiza Ambulance Tanzania kuna ushuru wowote maana naona sasa wnazidi kuleta utani na nchi
   
 13. Kilbark

  Kilbark JF-Expert Member

  #13
  Jul 30, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Nilitaka kuuliza swali kama hilo , wanakomalia mashangingi na kujenga barabara nzuri kwa ajili ya kujipigia kampeni. Wakiumwa wanakodisha charter plane kuwatoa hapo walipo Mtanzania wa kawaida hata hiyo Ambulance yenyewe anafanya kuiona kwa macho.Ni Machela, Baiskeli, Punda au Toroli . Hizo ndizo Ambulance
   
 14. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #14
  Jul 30, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Hakuna cha ushuru bana zile wakiagiza zinapita free si za serikali!
  Sema kuna mijitu michache ndio inayo tukwamisha si walalahoi na walaaniwe.
   
 15. M

  Msindima JF-Expert Member

  #15
  Jul 30, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Pole Fidel80 kwa machungu uliyopata,lakini TV ilikukosea nini mpaka uivunje huoni sasa umepata hasara ya kwenda kununua nyingine?
  Jamani hii nchi sijui inaelekea wapi mimi mambo mengine huwa hata staki kuyasikia maana yanakera sana,Ambulance 50 nchi nzima? hivi hawa watu wanatutakia mema kweli? Kuna hospital ngapi nchi hii ambazo zinahitaji ambulance?
   
 16. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #16
  Jul 30, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Hebu angalia msafara wa Mjomba na Mishangingi iliyopo. Nimeshindwa hata kuhesabu. Sasa ambulance itoke wapi? Ukiongeza huku inabidi upunguze kule.

  [ame="http://www.youtube.com/watch?v=3XYDM_KtEjY"]YouTube - Broadcast Yourself.[/ame]
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Jul 30, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Halafu lispika la bunge linanunuliwa gari la dola laki tatu....hapo bado hatujui gari la li raisi kikwete limegharimu kiasi gani, waziri mkuu, makamu wa raisi....yaani everything bs to the max...so stupid!

  Miafrika hiyo.....
   
 18. B

  Boney E.M. JF-Expert Member

  #18
  Jul 30, 2009
  Joined: Jan 22, 2007
  Messages: 425
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Fidel 80 nadhani wewe ndio una matatizo kibao. Kwa kuvunja TV yako una-solve nini? Sidhani kama ulifanya uamuzi wa busara na ndio maana hujapewa na hutapewa uongozi kwani maamuzi yako yanaweza kuwa madhara kwa wale unaowaongoza. Topic ilikuwa nzuri ila kwa kasoro hiyo hata kuijadili naona haina maana.
   
 19. F

  Froida JF-Expert Member

  #19
  Jul 30, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Yaani waziri kabore kweli yaani ambulance hamsini kwa watu milioni arobaini mchezo wa ajabu kabisa nchi hii ,halafu jana alikuwa na kisirani alikuwa anajibu wabunge kwa mkato sana
   
 20. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #20
  Jul 30, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Mkuu laiti kama ungekuwa na uchungu na nchi hii inavyo tafunwa na watu wachache najua ungechukua uamuzi kama wangu yaani kuna vijitu vichache vinajifanya Miungu watu ndo venyewe vina haki ya kutembelea Benz,BMW,Vogue,n.k huku vikitudharau sisi tulio viweka madarakani. Nasema na walaaniwe kwa Mungu malipo ni hapa hapa duniani.
  N.B Naombeni mchango jamani nitakuwa sipati news tena TV ndo hivyo nimeivunja.
   
Loading...