We Waziri Ambulance 50 tu nchi nzima?

mie nasema hawa viongozi wetu wanahitaji kupimwa akili zao,tusije tukawa tunalalamika kila siku kumbe tunaongozwa na mapunguani.mtu na akili zako timamu huwezi kutoa jibu kama hilo au hajui nchi ni nini? au hajui tanzania ina watu wangapi? yani nchi hiwe na bajeti ya ambulance 50 na bunge ina bajeti ya "mashangingi" 300? hama kweli chizi sio lazima aokote makopo.
 
Nashangaa wabunge nao wameridhika kupewa Ambulance 50 nchi nzima sijui wanatetea masrahi ya nani bungeni.
 
Hawa viongozi wetu sasa wanatuchezea akili inabidi watu tuanze kuandamana na sisi maana tutalalamika tuu hadi lini? na wao wanazidi kufaidika.Hapa nafikiria maisha ya mapacha wangu na hali inavyozidi kuwa mbaya wengine wanakula kuku kwa mrija.
 
Nimeskia leo asubuhi vifo vya mama wajawazito na watoto vinazidi kuongeza.
 
Jamani kutokana na hasira niliipasua TV yangu pale pale huu ni upuuzi sasa kodi tunalipa za nini? .
Kaka punguza hasira vinginevyo utamaliza vitu ndani maana hii nchi inamambo ya #@^***&..Mfano Ambulance kuikuta imepark baa dereva na Daktari wanapata moja baridi moja moja moto au kufanya shughuli zingine za hosp wakati tunajua Ambulance ni kwa ajiri ya shunguli zipi nini, lkn hii inasababishwa na nini? ...hii ndiyo Bongo
 
Hii serikali inatia kichefuchefu kabisa mwenyekuchukia na achukie baut hii ni kweli tupu. Kila muhula wa uchaguzi wananunu mashangingi, kila waziri anagari la wizara na mengine yamepaki tu yanakwenda sokoni kufanya shopping za nyumbani. halafu bado wanalalamika mshahara mdogo huu ni ujinga kabisa
 
Mkuu hapa panatakiwa mabadiliko ya kifikra. Kujua vipaumbele ni vipi. Mfano kununua magari ya wagonjwa na kujenga minara pacha. Au haya mashirika badala ya kuinvest kwenye kujenga majengo mijini pekee kwanini wasiwekeze na kwenye hospitali maana hao wanaowachangia ndiyo wanakotoka. Unaweza kuona kuwa viongozi wetu wako pale bora tu si kuwa pale kuongoza kwa kutoa muongozo ulio bora. Ndiyo maana irrespective ya khali mbaya wanataka marupurupu yao yaongezwe lakini wanasahau kuwa wale walio wapigia kura kila kitu ni cha kubahatisha kuanzia chakula, afya, elimu etc. TUNA VIHIYO WA UONGOZI.
 
Kwa ujumla majibu ya mawaziri Bungeni yanachefua. Ni kweli wana majibu ya hovyo hovyo. Kuna Mbunge mwingine leo aliuliza kwa nini, OC za vyuo vidogo (akatolea mfano chuo cha maji) ni nyingi kuliko za chuo kikubwa kama Udom. Akaomba serikali ifikirie kugawa fedha za OC kwenye vyuo kulingana na ukubwa wa shughuli za cghuo. Waziri Maghembe katika majibu yake ya hovyo hovyo wala hata hakugusia iwapo hilo litafikiriwa, alisema tu kuwa hali ni mbaya sana kwenye vyuo hivyo vidogo wakati inajulikana kuwa hakuna chuo chenye hali nzuri kifedha.
Kuna Mbunge mwingine alilalamikia fedha kidogo zinazotengwa kwa UDSM and Mzumbe. Pia akasema hata hizo chache zinazotengwa, hazipelekwi zote. katika majibu yake ya hivyo hovyo, maghembe anasema serikali itajitahidi kuhakikisha vyuo vyote vinapatiwa fedha za kutosha, Alisema hivyo baada ya kulieleza Bunge kuwa hali ya kifedha serikali ni mbaya sana na ndio maana fedha zinatengwa kidogo.
yaani ni vigumu sana kulewa wanachojibu mawaziri kwenye maswali ya wangune.
lakini wanaoshangaza zaidi ni wabunge ambao wanakubaliana na majibu hayo.
Lakini hata Sitta si aliwahi kuahidi kuwu hatovulimia majibu ya hovyo hovyo kutoka kwa mawaziri?
 
Nashangaa wabunge nao wameridhika kupewa Ambulance 50 nchi nzima sijui wanatetea masrahi ya nani bungeni.
Chukua Chako Mapema...naukionekana utetea wanainchi sana wana kuingiza kwenye system(utaongea nini na wewe uko kwenye system) au wanakuchafulia na hutaupata tena ubunge hivyo wengi wao hutulia imradi anapata chake na anauhakika kuendelea kuwa mbunge..lkn kwa kasi hii hawana muda mwingi tumeanza kuwashitukia, tutaondoa mmoja baada ya mwingine....
 
Nashangaa wabunge nao wameridhika kupewa Ambulance 50 nchi nzima sijui wanatetea masrahi ya nani bungeni.
Spika....Katibu soma kifungu

Katibu....Kifungu 6004 kitabu cha nne Tsh 2,564,000,000,00 bra bra...

Spika..... Kifungu hicho kinapitika?

Wabungu....pwaah......pwaah....pwaaaaaa
 
Spika..... Kifungu hicho kinapitika?

Wabungu....pwaah......pwaah....pwaaaaaa

Ndo hapo napo choka yaani nao wamekubali wananchi tuteseke kwa kupewa Ambulance 50 nchi nzima na kupitisha mashangingi 1000 kwa ajili ya vibopa.
 
kuwa hali ya kifedha serikali ni mbaya sana na ndio maana fedha zinatengwa kidogo.
Wamekamliwa vya kutosha na mafisadi au wametumia pesa nyingi sana kulinda mafisadi..kama serikali haina pesa mbona mashangingi wanayaagiza kama kawa na mishahara ya wabunge juu....
 
Alisema hivyo baada ya kulieleza Bunge kuwa hali ya kifedha serikali ni mbaya sana na ndio maana fedha zinatengwa kidogo.

Kama hali ya pesa serikalini ni mbaya kwa nini wasipunguze matumizi kwa watendaji wa serikali mfano kutembelea magari ya bei nafuu kama Escudo,Starlet, hata Bajaj mbona wenzetu Kenya wameweza! Si tunashindwa nini? Tunaendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu mpaka lini ndugu zangu?
 
Ndo hapo napo choka yaani nao wamekubali wananchi tuteseke kwa kupewa Ambulance 50 nchi nzima na kupitisha mashangingi 1000 kwa ajili ya vibopa.
duuuh kumbe ni 1000x100,000,000(ni wastani )...vipi bei ya Ambulance (50 x ......?)..
 
hata Bajaj
patakuwa patamu mtukama RA atembele Bajaji si mtampiga mawe...Kuna waziri alipendekeza wanunue yenye thamani ya mil 80 badala ya 100 kama sikosei kwamba watakuwa wameokoa mil 20@ na kupitisha msako kwa magari yaliyokuwa wameyafanya yao wakati ya serikali walimnunia ikawa bifu mpaka leo..sasa ukiwaambia watembelee bajaj si watakuua hata maiti yako isioneka
 
Back
Top Bottom