ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,141
- 950
Siku moja wakati naingie "filling station" pale Kimara Resort ORYX, yapata saa saba na madakika fulani mchana, mara ikaja gari ndogo, jamaa nae alikuwa anataka kuweka mafuta, akasimamisha karibu na mashine ya mafuta, akashuka akaelekea upande wa pili, akafungua mlango wa abiria. Ghafla tukashtukia anamchapa makofi dada aliyekaa upande wa abiria kumbe ni mkewe ..."waaap, wap,wap' kisha akasonya.."swiiiiiiiii, pumbavu" ..Mama akawa bado amekaa kimya, akafunika sura na mikono akaanza kulia...
Binafsi na watu tuliokuwepo hapo hatukupendezwa na ile tabia. Lakini mama hakushuka kwenye gari na jamaa akaiingia akaomba awekewe mafuta, alipomaliza wakaondoka haooooooooo....
Baadae nikajiuliza sana, sikujua kisa lakini nikakumbuka wakati fulani nilisikia visa vya kina mama wa kingoni wakati huo nasome sekondari kule Songea (Peramiho) wakipigwa na waume zao hawataki kutoka nje wala kuruhusu mtu aingile ugomvi ..wanasema kwa kingoni "KOMAI TU BABA,...KWANI NDOA YA NANI, SI NDOA YAKO HII??" ...yaaaani "WE UA TU BABA ..KWANI NDOA YA NANI, SI NDOA YAKO HII??"!! (samahani wangoni kama nimekosea mnaweza kusahihisha lugha hapo). Tafsiri yake ni kuwa Mke alikuwa akitetea mdoa yake, atajitahidi kuvumilia hata kwa kipigo cha namna gani. Wakati ule, hata mke akiumizwa namna gani, atamfichia mumewe siri, hakuna atakae jua na hata wakijua, ukipeleka shauri kwa "Mjumbe", mwanamke hawezi kwenda kutoa ushahidi.
Najiuliza tena na tena kwa nini, baadhi ya wanaume katika jamii zetu (Ukiondoa kule kenya ambapo kuna wanawake wanapiga waume zao) ni wepesi sana wa kupiga wake zao.??
Nini tafsiri yake kumpiga mwenzio? Unamfundisha, unamwadhibu au unamdhalilisha??, Je, unapompiga unamfananisha na mtoto kuwa hasitaili kufanya vile alivyofanya??...Wapo wengine ambao hawana staa, wanaweza kupiga mke hata mbele za watu, wakubwa waliowazidi umri nk..hii inatokana na nini? ni hasira, mfumo Dume, AU ??
Tujadili..
Mwanamke wa kikenya akimpa kichapo mumewe,utamaduni huu umechukua sura mpya kwa sasa nchini KENYA

"
Jamaa aliefahamika kwa jina la Kwingwa Mhina wa Kigogo Luhanga akimpiga mkewe mara baada ya kuhitilafiana"
Najiuliza tena na tena kwa nini, baadhi ya wanaume katika jamii zetu (Ukiondoa kule kenya ambapo kuna wanawake wanapiga waume zao) ni wepesi sana wa kupiga wake zao.??
Nini tafsiri yake kumpiga mwenzio? Unamfundisha, unamwadhibu au unamdhalilisha??, Je, unapompiga unamfananisha na mtoto kuwa hasitaili kufanya vile alivyofanya??...Wapo wengine ambao hawana staa, wanaweza kupiga mke hata mbele za watu, wakubwa waliowazidi umri nk..hii inatokana na nini? ni hasira, mfumo Dume, AU ??
Tujadili..
Mwanamke wa kikenya akimpa kichapo mumewe,utamaduni huu umechukua sura mpya kwa sasa nchini KENYA
Last edited by a moderator: