...we acha tu!

Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,745
7,773
Wapenda ligi watatu walibishana kuwa nani amekubuhu kwa ubishi kati yao . Wakaamua kila mmoja ahadithie ubishi wa haja alomfanyia mkewe ili wapime nani kubobea zaidi kwenye hiyo fani.

Mbishi 1 akasema:
Mi siku moja nilivyokuwa nje ya nchi nilimpigia mke wangu simu usiku kafungua simu hakusema haloo...kulaleki! na mimi nikakaa kimya sikuongea mpaka alfajiri wakati simu ilikuwa wazi.

Mbishi 2 akatia:
Mbona hiyo cha mtoto, mi siku moja nimerudi home nikagonga mlango mke wangu akaufungua lkn hakusema karibu mume wangu...aliniangalia tu...nikaona analeta madharau! sikuingia ndani nikasimama hapo hapo mlangoni mpaka asubuhi...huyoo nikatimua zangu job.

Mbishi 3 akaunganisha:
Hiyo nayo mbona cha mtoto tu, mi mke wangu tulipooana alikuwa anaona haya kunigusa...ananidengulia eti! na mimi sikumgusa na mpaka leo hatugusani.

Mbishi 1 na 2:
Aaaaaaaah faza! acha usanii, nyie si mna watoto wawili lkn?

Mbishi 3:
Na hao watoto sijamuuliza kawaokota wapi... kwani mi nataka mchezo!.
 
LOL!!!...Bingwa ni huyo mwenye watoto wawili wa 'kuokota'
 
mamamaaaaaahha, mbavu sina!.
nlikua na hasira tangu asubuhi, baada ya kusoma hapa kwakweli hasira zote zimekwisha, niko fresh!, kweli JF is evrything duh.
 
duh huyu wa tatu kanivunja mbavu kwa kicheko.! huyu ndio bingwa.
 
oh my god i am rolling on the floor kwa kucheka maana nilivyokuwa namsoma huyo mchizi wa pili nilianza kucheka sana,hapo sijui kamkomoa nani eti kasimama mlangoni hadi hasubuhi,ila kuja kumsoma wa tatu huyo ndiyo alinimaliza mbavu zangu jamani tsk tsk tsk tsk mahoka hahahahahahaha.duh duniani humu kuna watu machizi sana si bure,
 
mamamaaaaaahha, mbavu sina!.
nlikua na hasira tangu asubuhi, baada ya kusoma hapa kwakweli hasira zote zimekwisha, niko fresh!, kweli JF is evrything duh.

shemu vipi tena hasira za nini asubuhi yote au kuna nini ten kinaendelea?
bado dada anakusumbua tu nikija dar nitakutafuta niwape kitchen party ya ndoa
 
Duuuh, matundiko ya weekend ni raha tupu, hakuna cha ufisadi wala politiki, ni kicheko tu!!
 
Mbona hicho cha mtoto,kuna jamaa mitaa fulani kule mbagala mkewe amezaa na mpangaji wake na jamaa amewapongeza bila hata kuonyesha hasira,hadi leo wote wapo pamoja.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom