WCW: Thamani na Nguvu ya Mwanamke

Hatari mno.


Mwanamke asiye na Ego, ubinafsi na tamaa, ni mwanamke anayestahili kuishi kwa raha sana hii dunia.

MUNGU awatangulie wanawake wote ambao hawana Ego dhidi ya mwanaume, sio wabinafsi na wamepungukiwa tamaa.
 
Kiumbe kinachotumia hisia mara nyingi zaidi ya logic, Sijaandika kwa nia mbaya , I a ni kuusema ukweli iliyothibitika na kuthibitika kila siku ugomvi huanza pale ambapo Tunataka kila kitu kiwe logic kwao
Kiumbe kinachotumia hisia mara nyingi zaidi ya logic, Sijaandika kwa nia mbaya , I a ni kuusema ukweli iliyothibitika na kuthibitika kila siku ugomvi huanza pale ambapo Tunataka kila kitu kiwe logic kwao
Ndo maana wa shauri hasa wa kisaikolojia hupenda kutuasa kuwe na emotional intelligence above all else.

Hisia is greater than akili. Hii iko scientific proven... Ni lazima utengeneze mazingira mazuri ya Kihisia ili uweze kufikiri vyema
 
Asante kwa andiko hili mkuu, huwa nina furaha sana kuona mwanaume ana appreciate kazi ngumu inayofanywa na mwanamke ya kumleta kiumbe mwingine duniani, hakuna kazi inayoweza kufananishwa na hiyo, haipo.
Kuhusu submission, endapo mwanamke akiwa na mwanaume anaempenda na anaesimama kwenye uanaume wake, submission inakuja automatically na inakuja na feeling fulani ya kuenjoy sanaaa tena sanaa. Vile vile kama kwenye jamii ,wanaume wangejua kwamba wao ni protectors wa wanawake na si watumie nguvu zao kuwaumiza, ingekuwa ni raha sana na hizi mada sijui za wanawake hivi au wanawake vile, zingepungua.Tatizo linakuja kwenye jamii yetu wanaume wanatumia nguvu zao kumuumiza mwanamke na si kuwasaidia.

Nitakupa mfano, mimi nimekua kwenye jamii ambayo mwanaume kumpiga mke wake mjamzito hadi mimba inaharibika ilikuwa ni kawaida, hayo nimeshuhudia sijasimuliwa. Kesho mtu aje anambie " nyenyekea mwanaume" mimi nitamjibuje ilihali nimekua nikiona wanaume wanaua watoto wao ambao hawajazaliwa kwa kuwapiga wake zao wajawazito?. Huko makazini ndo usiseme yaani kuna mabosi wanaume ambao wanaona wafanyakazi wanawake kama machangundoa, wanahisi kama wanaweza kukutongoza na haupaswi kukataa. Mimi niliwahi kugombana na mkuu wangu wa idara enzi hizo kwa sababu alitumia lugha ambayo kwangu nilitafsiri kama udhalilishaji, na nilibishan nae hadi mwisho akasema nina dharau na sikujali. Kwanini nimuheshimu mtu ambaye yeye utu wangu hauthamini? yaani niwe mnyenyekevu ilihali naona utu wangu hauthaminiwi?. NEVER EVER.
 
Sure thing, it is that masculine energy ya kumfanya a feel safe let alone kuprovide.. Ikikosekana pia huleta mpasuko
Yaani umegusa penyewe. Nyumbani kukiwa na mwanaume ambaye ni mwanaume kweli, ni raha saana jamani kwa sisi wanawake.
 
Kiumbe kinachotumia hisia mara nyingi zaidi ya logic, Sijaandika kwa nia mbaya , I a ni kuusema ukweli iliyothibitika na kuthibitika kila siku ugomvi huanza pale ambapo Tunataka kila kitu kiwe logic kwao
Sisi wanawake tumeumbwa kuwa walezi wa familia,hisia zinatusaidia kutimiza majukumu yetu vyema. Ukiwa na mtoto mdogo ambaye hawezi kuongea, hisia ndo zinakuongoza kujua mwanangu sasahivi ana shida fulani ili utoe msaada. Bila hizo hisia kutuongoza ,tusingeweza kuwa wamama. Hata uwezo wetu wa kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja ni hisia zinatuongoza, unakuwa unafanya kazi fulani baadae hisia zinakwambia kule jikoni yale maji uliyobandika yatakuwa yamechemka na ukienda kweli unakuta yamechemka.
Pia usisahau sisi mkuu tuna hormones nyingi za mfumo wa uzazi ambazo kiwango chake kinabadilika kila siku. Siku estrogen ikiwa juu, unakuwa na furaha,siku progesterone ikiwa juu, unakuwa na huzuni na hasira . Hizo hormones kuwa hivyo ndio sababu kwanini mimi na wewe tumezaliwa, ingawa ndio sababu pia kwanini tunakuwa hatueleweki mara tumenuna mara tumefurahi, lakini mwisho wa siku hiyo ndo maana ya kuwa mwanamke.
 
Umeongea vizuri sana mkuu

Ila Kama ukisha jua ins and outs za hayo yotee. Unaweza kuwa na compassion kwao kujua where they're coming from... Also not being consumed by their negativity

Pole sana kwa kukulia katika hayo mazingira. Inatia uchungu sana..

Just forgive ukitambua it's mostly not them but societal and egoic conditions zinawasumbua
 
Notes taken.. 📝
 
Hawa v
Do you know how tough that is?
iumbe wanakula raha sana kwenye haya maisha

Wepesi na ugumu wa maisha wanachagua mwenza, mapato na mali zote wao ndio warithi wasiotengeneza hizo mali, kila anachopata baba kinaenda kwa mwanamke, yeye hutumia kujilemba, kujivalisha, kunenepa na bado hana sympathy kwa maumivu y mume. Ni mchoyo wa mali zake.

Men have the sacrificial role and toughest life lisilo na faida kwake baali kwa mke na watoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…