WCB wabadilike uimbaji

Mapensho star

JF-Expert Member
Jun 30, 2016
3,052
4,067
Nashangaa kuona wasanii wote wanaimba key moja mwisho wa siku haitambuliki huyu ni nani sababu wanaigana kama wataendelea hivi watachokwa hakuna anayetaka kubadika.

Baada yakuja huyo Lava Lava nikazani anakuja na key tofauti kumbe yale yale leo katoa nyimbo mpya inaitwa teja anaimba kama Diamond au harmonize
game ya mziki kwa sasa imepoa sana wasanii wajaribu kuja na style mpya kila siku kuimba kwa mazoea ni kero tu kwa wasikilizaji.
 
nashangaa kuona wasanii wote wanaimba key moja mwisho wa siku haitambuliki huyu ni nani sababu wanaigana kama wataendelea hivi watachokwa hakuna anayetaka kubadika
baada yakuja huyo lavalava nikazani anakuja na key tofauti kumbe yale yale leo katoa nyimbo mpya inaitwa teja anaimba kama diamond au harmonize
game ya mziki kwa sasa imepoa sana wasanii wajaribu kuja na style mpya kula siku kuimba kwa mazoea ni kero tu kwa wasikilizaji
Hawawezi kubadilika kwa producer mmoja huyo huyo walionae, wabadilishe maproducer ili biti zibadilike ndo wanataweza kubadilika.

Nataka nikwambie producer wao anayo biti moja tu alishaitengeneza siku nyingi anachofanya anaediti tu, halafu wanasema wanaproducer.
 
Kwani si usikilize wasanii wengine wenye melody tofauti?
Au Tanzania nzima wasanii wapo wcb tu?
Nyinyi ndio hamuwasapoti hao wasanii wengine halafu kila kukicha kuwasema hao wasafi!
Tubadilike tuwasikilize hao wenye melody tofauti kama wapo
 
Shida moja wanamtegemea huyo producer wao tu...hawataki kusikia producer mwingine...Kwa hiyo midundo na mirindimo ni ileile
 
kila mtu anataka kumuiga diamond matokeo yake tunashindwa kutofautisha yupi diamond original yupi fake. bongo flavour inaelekea kuwa bongo muvi ubunifu zero!!
 
Ni kweli jaribu uimbe ww ili ulete ladha tofauti sio kuongea tyuu,af hao wasafi wanaimba ivo mbna ndo wanaongoza kwa kusikilizwa si muwape masikio watu wengine nilitegemea ungeandika kuhusu msanii kama FOBY AU IBRA NATION
 
toka waanze kuimba naona bado hawajachokwa inaonekana watu wanawakubali, ukitaka ladha tofauti kuna wasanii wengine pia
 
Imefika wakati sasa Diamond afanye kazi na maproducer tofauti barani Afrika.
Dj Maphorisa ni mkali sana wangefanyakazi
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom