Wazungu wameichoka CCM, Wasituletee ya Libya

Wazungu wameichoka CCM, Wasituletee ya Libya

Na kwa akili za Nyumbu tulio nao hilo wao watalichukulia mkumbo
Hapa wanapaswa kuangalia madhala yapo zaidi kwa kinanani haswa,
Wengine kwa akili zao wanafurahia kuwa ndio nafasi yao kuingia madalakani
Tutavuka tu
 
Kwani primary goal ya TISS ni nini ?? Ukishanijibu hilo ndio uangalie kama wameshindwa au wamefanikiwa
Kama lilivyo jina lao, ni usalama wa taifa.
Kumbuka Rais anakua briefed kuhusu mambo ya kiusalama na yeye ndie anatoa order kwa wahusika kuchukua hatua.
Kama taasisi kunaweza kuwa na mapungufu ya hapa na pale lakini kiujumla taarifa nyingi wanazo lakini hawana mamlaka ya kuchukua hatua.
 
Kinachotakiwa ni UZALENDO kwa sisi kana Watanzania hii tabia ya kuwakumbatia Wazungu ndio inayosababisha ukosefu wa amani Duniani nchi nyingi ziliambiwa akitoka fulani maisha yao yatakuwa mazuri lakini mpaka leo ni maskini wa ajabu. Toka lini Mzungu akawa na huruma na mtu Mweusi? Kwa nini walilie CCM itoke? Hii nchi itaendelea kuwa chini ya mikono salama ya CCM mpaka pale kitakapopatikana chama mbadala cha Wazalendo na wafia nchi wengine kama CCM ndio tutairuhusu CCM ikajiunge na Malaika wengine Mbinguni.
Ivyo vyama vyenu vya kupiga dili na ukibaraka kwa wazungu vitaongoza baada ya sisi wazalendo wa nchi hii kufa kikabaki kizazi chenu cha mtoto wa kiume unapiga picha huku umebana ulimi.

wapumbavu wakubwa nyie mikono salama albino wanakufa,mikono salama wakati chama linafuga majangili na mafisadi wewe hospital ya srikali haina panadol alafu watu hawa fiki hata 30 wanagawana mabilioni ya escrow mabehe fake,uda,eti hadi leo madini yanayo chimbwa mwekezaji ana miaka zaidi ya 20 lakini anakwambia anapata hasara kisa anagawana na majinga mapumbavu ya ccm....mue mnaona haya kusifia uhayawani wenu hapa
 
Na kwa akili za Nyumbu tulio nao hilo wao watalichukulia mkumbo
Hapa wanapaswa kuangalia madhala yapo zaidi kwa kinanani haswa,
Wengine kwa akili zao wanafurahia kuwa ndio nafasi yao kuingia madalakani
Tutavuka tu
mnakuwa waoga nini sasa subirini mbele kwa mbele yenu serikali iliyopita siillikuwa inajinasibu kuwa mnakubalika kwa mabwana wakubwa??jipambanueni na demokrasia yenu yauongo,kama ccm mngekuwa wazalendo basi mngekataa kata kata mwaka 1992 kuingizwa kwa vyama vingi katika katiba.!sababu ya unafiki wenu mkajua mtaendelea kutawala kinafiki hivyo hivyo waume zenu sasa wanawananga hata mkivuka jueni kunamengi yatalicost taifa sababu yadhalimu wa chama cha mapinduzi
 
....................................................................kama siri aliyoitoboa Mugabe kuhusu CCM ni kweli, ..............TISS fanyeni kazi yenu............................................
Sidhani kama TISS wana deal na mambo mazito kiasi hicho... naamini wakiwezacho TISS ni kutoa maagizo yanayoitwayo 'maelekezo kutoka juu' naamini Lubuva na Jecha anawafaham vizuri sana TISS na kazi za.... Mungu atunusuru tu Zanzibar isije kumbwa na magaidi tu at the expence of CCM kuendelea kuwa mshindi wa uchaguzi Zanzibar
 
Kama lilivyo jina lao, ni usalama wa taifa.
Kumbuka Rais anakua briefed kuhusu mambo ya kiusalama na yeye ndie anatoa order kwa wahusika kuchukua hatua.
Kama taasisi kunaweza kuwa na mapungufu ya hapa na pale lakini kiujumla taarifa nyingi wanazo lakini hawana mamlaka ya kuchukua hatua.
Kwa maana hiyo utendaji wa TISS unapimwa kwa utashi wa Rais ?? Kwamba Rais aamue ni Taarifa gani ifanyiwe kazi na ipi isifanyiwe kazi ?? Siku tukipata Rais Mwendawazimu asiyefanyia kazi taarifa za msingi mathalani tishio la ugaidi likitokea la kutokea TISS watakua upande gani wa waliofanikiwa au walioshindwa ???
Basi hakuna sababu ya idara hiyo kutumia jina la usalama wa taifa ,wangejiita washauri wa raisi
 
Washindwe na walegee kwa jina la mngu, hiyo fujo itatoka wap kama wazee wa maandamano hawajaianzisha
 
Y
mkuu don't underestimate the power of intelligence, tatizo amani tuliyonayo imetufanya tumekuwa complacent sana.
So ni muhimu taasisi yetu ya usalama kukusanya some covert intelligence and use them to predetermine the situation, then take preventive measures, kimsingi hatuwezi kuvamiwa kivita, so kuzuia propaganda encroachment ni muhimu sana na hii huwezi kuifanya bila kujiandaa kiintelligensia
TISS itawezaje kuzuia propaganda,huku vyombo vyote vya uhakika kwa habari vina milikiwa na western?? ingekuwa TBC ndo wanasambaza propaganda ingekuwa rahisi
 
Duh, elimu elimu elimu, hivi unategemea itapigwa ccm pekee? Nilidhan walio jf wako vizuri upstairs kumbeee sivyo
watapigwa wananchi wote kiuchumi lakini kila moja atajua CCM ndo imesababisha
 
Mkuu hilo swali unaweza ukaona ni la kitoto lakini ,fikiria tena ?? Unazijua Western propaganda vizuri hivi unategemea nini kama kweli wametuchoka watanzania ? TISS watafanya nini ,?? Hapo kuna CIA,MI6,MOSAD nk wote kwa pamoja hao wanaungana
Nani atakayewaunga mkono? Mbona hawakuyasema hayo wazi wazi wamwambie kikwete tu? Wewe kama unadhani cia, m16, na mossad ni Mungu endelea kuwasubiri.
 
nimetafakari sana hotuba ya MUGABE, yule dictator wa Africa hasa pale aliposema eti KIKWETE alimtonya kuwa dunia ya kwanza wamemwambia CCM imekaa madarakani muda mrefu sana na wakashauri wawapishe na wengine. tafakari yangu imenikumbusha kuwa kauli hizi si mara ya kwanza kusikika katika nchi tofauti na baada ya kauli hizi mambo huwa si mazuri,
Wazungu wakikuchoka, na wakaamua kukupa live basi ujue kweli wanamaanisha, waulize Libya, Tunisia, Misri, sudan, afaghanstan, Osama, n.k

hawa watu ni mabingwa wa kutumia kosa dogo sana kupenyeza fujo kubwa ili kumuondoa yoyote waliyemchoka, yaani they take advantage of a very small internal mistake or cleavage and escalate it to unimaginable conflict combo.
Sasa haka ka mgogoro ka zanzbar tusipokuwa makini ndo katatumika, nimewaskia wakianza kutoa warning kalikali, na za kuogofya, huku wakisema eti wasijelaumiwa kuwa hawakutuonya. Hapa kuna kitu kinanukia hapa. kama siri aliyoitoboa Mugabe kuhusu CCM ni kweli, TISS fanyeni kazi yenu, nna wasiwasi Zanzbar inaweza kutumika kama njia ya hawa wenzetu kupenyeza propaganda za kuwaharibia waliochokwa

CCM imechokwa na ndugu zao wazungu, alafu wanalea mgogoro ambao ni potential threat kwa amani ya Tanzania nzima, Tusishangae rocket launchers zikianza kupatikana mitaani, alafu tukaanza kujiuliza eti zimetoka wapi, wakati wameshasema wamewachoka CCM

Msijesema sikusema
Wadhungu was*ng*
 
Swala la Zanzibar hizo nchi wahisani wakiamua kulitumia kama kigezo cha ku impose strict economic sanctions haturudi Zimbabwe ilipo sasa

Wanatakiwa wasome katiba ya jamhuri ya muungano na ile ya Zanzibar kablla ya kuchukua maamuzi yoyote.Huwezi kuiwekea sanctions Tanzania kwa sababu ya yanayoendelea ndani burundi!!

Zanzibar ni nchi huru yenye Raisi na sheria zake.Mambo ya uchaguzi wa Zanzibar si swala la Muungano.Wakicheza vibaya hapo hatima ya vitega uchumi vyao vilivyopo na wanavyotarajia kuwekeza vitaathirika.Mfano wakiweka vikwazo vya biashara kwa Tanzania mfano vya utalii.Watakao umia kwanza ni ndege zao zinazoleta mamilioni ya watalii wanaotembelea mbuga za ARUSHA,MANYARA,Mlima KILIMANJARO na Zanzibar,Halafu pia watakaoumia sana ni makampuni yanayoleta hao watalii ambayo yako nchini kwao,na watakaoumia zaidi ni wawekezaji wa kutoka nchi zao wenye mahoteli ya kitalii Arusha na Zanzibar.Kwa sekta hiyo tu wao ndio watakuwa waumiaji wakubwa.

Na Kwa Tanzania vikwazo hivyo vya biashara vya utalii vikiwekwa watu wa kwanza kuumia ni wa UKAWA wale wa KASKAZINI NA ZANZIBAR sababu wanategemea sana utalii kutoka kwa hao wazungu waweka vikwazo.

Usidhani vikwazo vinawekwa tu kwa sababu tu SEIF hamad KAWAOMBA wanaangalia Faida na hasara kwao za hivyo vikwazo.Wakiona watafaidika vikiwekwa wanaweka wakiona watapata hasara wakiweka hawaweki.Wanaangalia upande wao tu hawaangalii upande wa UKAWA au nani.
 
Ccm inaweza kuongoza nchi kupitia chama kingine ambacho baada ya uchaguzi wanachama wao wote watahamia kwa wingi kwenye chama chao hicho. Ccm kwa siasa za kitaalam ni ma-genius.
 
Acha kiherehere subiri tarehe 20 utarudi hapa !
 
Kwani mkuu kwenye uchaguzi ni sawa na kupokea threat kutoka kwenye mataifa makubwa ambayo ndio ma bwana zetu ???
Wao hutumia busara kubwa kuliko viongozi wa Africa au umesikia ulaya uchaguzi kufutwa or uchaguzi usio kuwa huru? Lazima muongozwe waafrica
 
Osama nayo ni nchi! Nchi zote ulizotaja zina shahabiana mambo fulani na ndio yaliyopelekea machafuko unlike Tz ambako kuna Amani, democracy, tolerance na upendo. Mtu mzima usitishiwe nyau
Mkuu wengine wanakuaga kama nyau kumbe no chui
 
Tatizo sisi hatuna tatizo na nchi yoyote ya mzungu kisiasa.Waafrika hawajawahi ingilia siasa za nchi za wazungu.Wala hawajawahi hoji kwa nini malkia wa uingereza au mfalme wa norway kwa nini awe yeye tu asiwe anachaguliwa kidemokrasia kwa sanduku la kura? Lakini wao kiguu na njia kutwa kuingilia siasa za Afrika.Mwenye adabu ni china tu.

Kuhusu Zimbabwe uchumi wake umevurugwa na wazungu.Wazungu walikuwa wameshilia ardhi kubwa yenye rutuba Zimbabwe kwa miaka mingi Kila wazungu wakiambiwa wagawieni mashamba waafrika wakawa wanagoma.Waafrika wanaendelea kuteseka.Mugabe akachukua mashamba yao akawagawia waswahili.Alipowapa waswahili wakawa wanalima mazao yale yale waliyokuwa wakilima wazungu kwa ubora ule ule bila kupunguza kitu.Walipotaka kuuza kwenye masoko ya wazungu,wazungu wakagoma kununua wakasema hatutaki kununua kutoka kwa ngozi nyeusi mumefukuza wazungu wenzetu kuleni mazao yenu wenyewe.Ndio mwanzo wa kuporomoka uchumi wa Zimbabwe.

Kaongeze elimu
 
Wazungu bana!Tanzania tumepata boyfriend mpya(China).anatutreat vizuri na anatuheshimu.pia anatusaidia kwenye kuleta maendeleo..tofauti na wazungu(USA,UK and the co)ambao wamekuwa wanatugegeda tu without any help..Halafu mbona wana mademu wengi tuu,Rwanda,Uganda and many more ila bado wanatungangania?wakatishe tu misaada yao ila bf wetu China atatusaidia.
 
Uhuru wa kujiamulia mambo yetu, bado sana hatujaupata, tutaupata tu, pale tutakapokua na uwezo wa kiuchumi na rasilimali watu, bila hivyo nchi za afrika tutaendelea kunyanyaswa miaka mingi ijayo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom