Wazungu wameichoka CCM, Wasituletee ya Libya

wazungu wakiamua kuitoa ccm hawataitoa kwa sababu ya kukusaidia wewe bali kwa ajili ya maslahi yao kijana inabidi ujifunze uzalendo wa kuipenda nchi yako hata kama matendo ya viongozi walioko madarakani hawafanyi mambo unayotaka dhambi ya usaliti ni kubwa hata kwenye vitabu vya dini wameandika
 
Ni watu makapuku tu ambao hawajaichoka ccm, ila wenye ufahamu tumeichoka mno mno ccm
Si bure ubini wako ni kichaa. Naona kimeanza kulipuka. Wakati watanzania wanarudisha mapenzi kwa ccm baada ya kujivua magamba wewe unaikumbatia cdm/ukawa, waliovua magwanda na kuvaa magamba ya ccm. Duhh!! aisee!! Nani makapuku sasa?
 
Ni vema tukumbuke kuwa, kwa lolote unaloombea like ni kwamba likiwa nawe utakuwemo ndani yake iwe ni mema au mabaya. Ikiwa neema kila aliyepo ndani ya nchi ataitumia. Ikiwa machafuko wote waliomo ndiyo yatawapata. Hakuna atakaye kuwa pembeni a naangalia kama anaagalia Movie kwenye TV. Chamsingi tumuombe Mungu aturekebishe.
 
Back ground ya Noth Korea huwezi kuifananisha na Tanzania hata kidogo wakati wa economic criss ya 1990 waliopitia North Korea baada ya USSR kusambaratika ilibidi watafute alternative ways ya kupata pesa kwa ajili ya kuendesha nchi yao na pesa wanazopata ni nyingi zinatokana na illegal means kama producing and smuggling drugs, smuggling Elephant ivory, selling weapons and nuclear tech middle east ,operating casinos in China unofficial nakadhalik

Korea kaskazini wewe huijui.Hayo uliyoandika ni propaganda za magharibi.

Korea ni nchi pekee duniani ambako ni marufuku mwananchi kulipa kodi.Njia zote za uchumi na biashara zote kubwa ziko mikononi mwa serikali

Korea ni taifa ambalo linategemea mapato toka kwenye mashirika ya umma.Korea mashirika ya umma hufanya vizuri mno na faida zake ndizo hutumika kuendesha serikali.Korea ukiendesha shirika la umma kwa hasara au kulisababishia hasara wanakuua.Mashirika ya umma ndio engine ya uchumi wa korea.Sisi watanzania yalitushinda lakini tungekuwa tuliweza leo hii tungekuwa hatupigi goti kwa mtu wala kulalamika ajira hazipo.
 
Nashukuru sana siijui Korea kaskazini ,hizo biashara wanafanya na nchi gani ??? Hayo mashirika ya umma yanajiendesha vipi ??
 
Ni ujumbe mzito sana mkuu, majuto ni mjukuu na ninge huja baadaye sana. Mungu ibariki Tanzania
Vijana wa siku hizi akili zao zipo kule wanapotolea kinyesi ndio maana wana mawazo ya kishetani na kifedhuli.....akilini mwao wanalinganisha vita au machafuko sawa na yale wanayoyatazama kwenye mikanda ya filamu za kivita.....wao wanadhani vita ni rahisi kama kupiga mswaki na kutema mate chini.....kwa fikra zao fupi wao wanadhani kuwa wale wanaovuka bahari na kukimbilia ulaya kwenda kuishi ukimbizini ni kama wanaigiza na sio matukio halisi.....
 
nimetafakari sana hotuba ya MUGABE, yule dictator wa Africa hasa pale aliposema eti KIKWETE alimtonya kuwa dunia ya kwanza wamemwambia CCM imekaa madarakani muda mrefu sana na wakashauri wawapishe na wengine. tafakari yangu imenikumbusha kuwa kauli hizi si mara ya kwanza kusikika katika nchi tofauti na baada ya kauli hizi mambo huwa si mazuri,
Wazungu wakikuchoka, na wakaamua kukupa live basi ujue kweli wanamaanisha, waulize Libya, Tunisia, Misri, sudan, afaghanstan, Osama, n.k

hawa watu ni mabingwa wa kutumia kosa dogo sana kupenyeza fujo kubwa ili kumuondoa yoyote waliyemchoka, yaani they take advantage of a very small internal mistake or cleavage and escalate it to unimaginable conflict combo.
Sasa haka ka mgogoro ka zanzbar tusipokuwa makini ndo katatumika, nimewaskia wakianza kutoa warning kalikali, na za kuogofya, huku wakisema eti wasijelaumiwa kuwa hawakutuonya. Hapa kuna kitu kinanukia hapa. kama siri aliyoitoboa Mugabe kuhusu CCM ni kweli, TISS fanyeni kazi yenu, nna wasiwasi Zanzbar inaweza kutumika kama njia ya hawa wenzetu kupenyeza propaganda za kuwaharibia waliochokwa

CCM imechokwa na ndugu zao wazungu, alafu wanalea mgogoro ambao ni potential threat kwa amani ya Tanzania nzima, Tusishangae rocket launchers zikianza kupatikana mitaani, alafu tukaanza kujiuliza eti zimetoka wapi, wakati wameshasema wamewachoka CCM

Msijesema sikusema
Siyo wazungu tu walioichoka CCM wote tu tumeichoka itoke kwa namna yoyote inayowezekana
 
Nashukuru sana siijui Korea kaskazini ,hizo biashara wanafanya na nchi gani ??? Hayo mashirika ya umma yanajiendesha vipi ??

Wana mashirika YA UMMA kama ya UMEME,MAJI,MASHAMBA MAKUBWA,MA-SUPERMARKET,MASHIRIKA YA UTALII,MAHOTEL,VIWANDA,YA Utangazaji.mabasi,malori,makampuni ya simu nk ni ya serikali.Kila kampuni kubwa Korea ni ya serikali

Korea kaskazini inafanya biashara na nchi nyingi tu hasa kuwauzia zana za kivita.Sio nchi zote duniani zimeiwekea vikwazo korea kaskazini kibiashara.Tanzania pia hatujawawekea vikwazo.Kwa hiyo wanafanya biashara na nchi nyingi tu.Lakini China ndio partner mkubwa wa kibiashara wa korea na nchi nyingi tu hasa zile zilizokuwa za kijamaa kama za America kusini,cuba,venenzuela ,nk

Nchi za magharibi ndizo zina roho mbaya na korea kaskazini
 
Sasa turudi kwenye swali la msingi la Mkuu aliyesema mbona Korea kaskazini wameweza sisi Tanzania tutashindwa vipi ?? Tuna mashirika mangapi ya umma yanayofanya kazi ?? Usije ukaniambia Tanesco na TTCL ,VIWANDA ,kuna sababu gani ya kutengeneza tension na haya mataifa ya magharibi ilhali hakuna lolote tunaloweza kulifanya na pia North Korea inafanya biashara na European union ,ubishi wa viongozi wetu utatumbukiza kwenye shida tu kama Zimbabwe ,kwa nchi kama Tanzania tutatumbukizwa kwenye vita vya uchumi na sio vita vya wenyewe kwa wenyewe kama mleta mada alivyo tahadharisha
 
nimetafakari sana hotuba ya MUGABE, yule dictator wa Africa hasa pale aliposema eti KIKWETE alimtonya kuwa dunia ya kwanza wamemwambia CCM imekaa madarakani muda mrefu sana na wakashauri wawapishe na wengine. tafakari yangu imenikumbusha kuwa kauli hizi si mara ya kwanza kusikika katika nchi tofauti na baada ya kauli hizi mambo huwa si mazuri,
Wazungu wakikuchoka, na wakaamua kukupa live basi ujue kweli wanamaanisha, waulize Libya, Tunisia, Misri, sudan, afaghanstan, Osama, n.k

hawa watu ni mabingwa wa kutumia kosa dogo sana kupenyeza fujo kubwa ili kumuondoa yoyote waliyemchoka, yaani they take advantage of a very small internal mistake or cleavage and escalate it to unimaginable conflict combo.
Sasa haka ka mgogoro ka zanzbar tusipokuwa makini ndo katatumika, nimewaskia wakianza kutoa warning kalikali, na za kuogofya, huku wakisema eti wasijelaumiwa kuwa hawakutuonya. Hapa kuna kitu kinanukia hapa. kama siri aliyoitoboa Mugabe kuhusu CCM ni kweli, TISS fanyeni kazi yenu, nna wasiwasi Zanzbar inaweza kutumika kama njia ya hawa wenzetu kupenyeza propaganda za kuwaharibia waliochokwa

CCM imechokwa na ndugu zao wazungu, alafu wanalea mgogoro ambao ni potential threat kwa amani ya Tanzania nzima, Tusishangae rocket launchers zikianza kupatikana mitaani, alafu tukaanza kujiuliza eti zimetoka wapi, wakati wameshasema wamewachoka CCM

Msijesema sikusema

Wala usiogope hata Seif anayetia ndimu anakuwa ametoka kunywa gahawa na Shein, ndio akiwa anaelekea kwake anatafuta media ziko wapi na kuwapasha kuwa kuna mgogoro. Akivuka bara ndio acha akikutana na UKAWA ndio na wenyewe anawajambisha kuwa Zenji ni mshike mshike kumbe kukiwa na Maulid wanagonga mpunga na chai pamoja. Seif kule ni makamo wa presidia na matamko anayatolea bara.
 
Sina tatizo na hilo amani tuliyonayo sio kwamba TISS ndio walio sababisha ikawepo ni Mungu tu na ashukururiwe kwa hilo ,hizo covert intelligence unazosema ningewaheshimu sana kama Twiga wanapanda ndege ya kijeshi ya Qatar ,makontena hayalipiwi kodi,meli ya pembe za ndovu zinakamatwa nje ya nchi ,kashfa za Richmond, escorow ,kama haya tu yamewashinda ni covert operations zipi za Mosad,CIA,MI6 na wenzake watazuia ???
Una uhakika gani kama yamewashinda?
Ni vizuri kujua majukumu yao, hadi wewe kuyaongelea hayo ina maana taarifa zilitoka sehemu usifikiri ni bahati mbaya.
 
ubishi wa viongozi wetu utatumbukiza kwenye shida tu kama Zimbabwe

Tatizo sisi hatuna tatizo na nchi yoyote ya mzungu kisiasa.Waafrika hawajawahi ingilia siasa za nchi za wazungu.Wala hawajawahi hoji kwa nini malkia wa uingereza au mfalme wa norway kwa nini awe yeye tu asiwe anachaguliwa kidemokrasia kwa sanduku la kura? Lakini wao kiguu na njia kutwa kuingilia siasa za Afrika.Mwenye adabu ni china tu.

Kuhusu Zimbabwe uchumi wake umevurugwa na wazungu.Wazungu walikuwa wameshilia ardhi kubwa yenye rutuba Zimbabwe kwa miaka mingi Kila wazungu wakiambiwa wagawieni mashamba waafrika wakawa wanagoma.Waafrika wanaendelea kuteseka.Mugabe akachukua mashamba yao akawagawia waswahili.Alipowapa waswahili wakawa wanalima mazao yale yale waliyokuwa wakilima wazungu kwa ubora ule ule bila kupunguza kitu.Walipotaka kuuza kwenye masoko ya wazungu,wazungu wakagoma kununua wakasema hatutaki kununua kutoka kwa ngozi nyeusi mumefukuza wazungu wenzetu kuleni mazao yenu wenyewe.Ndio mwanzo wa kuporomoka uchumi wa Zimbabwe.
 
Binafsi nadhani ving'ang'anizi wa madaraka wasio heshimu demokrasia wawekwe kundi moja na magaidi.Hawa wakiachiwa ndio wanutumbukiza nchi kwenye mfarakano na umwagaji damu wa kutisha- shuhudia hali ya Burundi. Such irresponsible leaders should be targeted terrorists.
 
Tatizo sisi hatuna tatizo na nchi yoyote ya mzungu kisiasa.Waafrika hawajawahi ingilia siasa za nchi za wazungu.Wala hawajawahi hoji kwa nini malkia wa uingereza au mfalme wa norway kwa nini awe yeye tu asiwe anachaguliwa kidemokrasia kwa sanduku la kura? Lakini wao kiguu na njia kutwa kuingilia siasa za Afrika.Mwenye adabu ni china tu.

Kuhusu Zimbabwe uchumi wake umevurugwa na wazungu.Wazungu walikuwa wameshilia ardhi kubwa yenye rutuba Zimbabwe kwa miaka mingi Kila wazungu wakiambiwa wagawieni mashamba waafrika wakawa wanagoma.Waafrika wanaendelea kuteseka.Mugabe akachukua mashamba yao akawagawia waswahili.Alipowapa waswahili wakawa wanalima mazao yale yale waliyokuwa wakilima wazungu kwa ubora ule ule bila kupunguza kitu.Walipotaka kuuza kwenye masoko ya wazungu,wazungu wakagoma kununua wakasema hatutaki kununua kutoka kwa ngozi nyeusi mumefukuza wazungu wenzetu kuleni mazao yenu wenyewe.Ndio mwanzo wa kuporomoka uchumi wa Zimbabwe.
Tusitake kufanyana wajinga mkuu ,bajeti ya nchi yetu inategemea nini ??? Swala la Zanzibar hizo nchi wahisani wakiamua kulitumia kama kigezo cha ku impose strict economic sanctions haturudi Zimbabwe ilipo sasa ?? Sawa tuseme tunaachana na sera za mabeberu wa magharibi IMF na WB mbadala wake utakua nini ???
 
Una uhakika gani kama yamewashinda?
Ni vizuri kujua majukumu yao, hadi wewe kuyaongelea hayo ina maana taarifa zilitoka sehemu usifikiri ni bahati mbaya.
Kwani primary goal ya TISS ni nini ?? Ukishanijibu hilo ndio uangalie kama wameshindwa au wamefanikiwa
Halafu usikariri sio kila source ya Taarifa inatoka TISS
 
Amani ipo sana lakini ukiwa na amani ni lazima ujue kuna nchi zingine hazitutakii mazuri, tusijisahau na kila wakati tuwe makini kwa maisha haya ya leo.

Watu wanajisahau unaweza kuingia ofisi za serikali bila hata kuulizwa unaenda wapi, unarandaranda ofisi hadi ofisi.

Kama mnakumbuka yaliyotokea Libya yule kijana aliyeichukuwa bastola ya Gaddafi (golden pistol) mpaka leo bado anayo na ilitengenezwa Belgium na leo hiyo hiyo company bado inasaidia rebels kwa kuwauzia silaha. Think big
1454485000270.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom