mayenga
JF-Expert Member
- Sep 6, 2009
- 4,118
- 1,973
Kiukweli kwa hali tunayokwenda nayo watu wa usalama wakae sana chonjo.Hali ya Zanzibar kwa mwendo tunaoenda nao tukienda kwa kulazimishana tuko hatarini.Dunia ya sasa ya wasomi haiingii akilini uchaguzi ufutwe na utangazwe mwingine ,na huku mwenye kufuta hana mamlaka ya kufanya hivyo na bado mkahubiri demokrasia.Kama walivyoshauri wanadiplomasia wazoefu ubabe hauwezi kusadia hata kidogo,katika suala la Zanzibar.Tufikie hatua tuone ni muhimu tutumie busara zetu,amani hii tuliyonayo kwa swala la Zanzibar iko mashakani.Hatutakuwa wajinga kama tukijishusha kwa mustakhabari wetu.Mazingira na Jiografia ya Zanzibar,tamaduni na itikadi ya eneo lote la bahari ya hindi si ishara nzuri kwa baadaye kama hakuna muafaka.
Kumbuka ikiwa huu uchaguzi wenye mizengwe ukifanyika,CUF watakuwa ni kama mbogo aliyejeruhiwa.CUF wana wafuasi wenye itikadi,uelewa na maono tofauti na bahati mbaya hata jicho kimataifa linaonekana kuwaunga mkono kwa kiasi kikubwa.Upo uwezekano mkubwa utawala wa Shein kwa miaka mitano ukawa mgumu,upo pia uwezekano Zanzibar ikiwa kituo cha uasi.Suluhisho hapa ni dogo kama chembe ya haladali-MUAFAKA,wenye tija na pengine wenye kushirikisha vyama vyote.Tuache ubabe,majuto ni mjukuu.