Wazungu huwa hawaitii chakula wageni?

Wazungu huwa hawaitii chakula wageni?

Na unabahati ungekuja kwangu ningekupa glasi ya maji ukimaliza nakupa tule tu vijiti twa kuchokonolea meno.
 
Za mchana wakunduguzangu! Tukiwa tumetoka ofisini(kazi nusu siku jumamosi), rafiki yangu akaniambia twende kwao kwa chakula cha mchana. Kufika kwao nikakuta mke wake kama hajaridhika kualikwa kwangu. Baada ya kumaliza kula nikasema, "nashukuru kwa chakula shemeji yangu". Akasema, "asante kwa kula hatuna cha kukulipa". Jamani muwe mnaangalie kauli za kuongea sio mnaongea tu mnapokaribisha wageni. Nilivyomwambia rafiki yangu akasema kuwa mke wake hajawahi kuzungumza hivyo na akasema eti nipotezee ila nimekwazika sana. Poleni nanyi pia.
Habari zenu!
Niliagizwa na mkubwa wangu wa kazi nipeleke hati fulani aipitie mzungu nyumbani kwake. Nikakaribishwa vizuri na mfanya kazi wake hadi sebuleni nikakuta anakula. Akaonesha ishara ya kunikaribisha kukaa kwenye sofa. Pia akanipa ishara ya kutokuongea. Nikakaa kimya. Alivyomaliza ndo akatekeleza shida yangu. Yaani hadi amemaliza kula hakukaribisha chakula kama tufanyavyo sisi waafrika. Hawa wenzetu hawana utaratibu wa kuongea wakati wa kula na hawakaribishi?

Mkuu inaonekana unaendekeza sana kula.
Chakula kwako ni big deal eeh!!
 
huwa hawaharibu bajeti yao kama ni sahani nne hakuna ya ziada ndo maana hawakukukaribisha

nice and like very smart mbongo sijui anamatatizo gani

kwani we mleta thread ulikuwa hujui utakula wapi tena home kwetu bora huyo mzungu.Fata ulichoendea s.Tupid
 
Wewe ulifikiri nyumbani kwa mzungu ni hotel au mgahawa ? Kwa taarifa yako wenzio wanapika kwa kiasi sio kama ninyi wanyamwezi mnavyopika makande ya kula siku tatu.
 
Alipigia simu na bosi kuwa nitampelekea kwake mkuu Kiranja.

The name is Kiranga.

Simu hazijajibu swali. Kwa nini habari za ofisini zije nyumbani?

Ukianza kuleta ya nyumbani ofisini ndiyo unakutana na mambo tofauti.

Kwa sababu ushaanza kuambatanisha vitu tofauti, vya nyumbani na ofisini.
 
Last edited by a moderator:
nice and like very smart mbongo sijui anamatatizo gani

kwani we mleta thread ulikuwa hujui utakula wapi tena home kwetu bora huyo mzungu.Fata ulichoendea s.Tupid

Wengi tukisema tunakuja kwa mtu hata hujui wakoje unajiaminisha utakula... nilishawahi karibishwa na rafiki yangu we use to take beer maeneo fulani akaniambia anatamani nijue kwake siku zinavyokaribia akaniambia plz dont forget to take your own drinks.. kwa wakati Ule nilichukia sana yani mi najua mwaliko ndo nikajitundike mpaka nilale anazengua ila niligundua bajet ni jambo muhimu sana kwao.
 
Inawezekana ilikuwa hakuna kingine na hakutaka kukukaribisha kinafika...I mean ukae ule ukiondoka asikitike.
 
Wengi tukisema tunakuja kwa mtu hata hujui wakoje unajiaminisha utakula... nilishawahi karibishwa na rafiki yangu we use to take beer maeneo fulani akaniambia anatamani nijue kwake siku zinavyokaribia akaniambia plz dont forget to take your own drinks.. kwa wakati Ule nilichukia sana yani mi najua mwaliko ndo nikajitundike mpaka nilale anazengua ila niligundua bajet ni jambo muhimu sana kwao.

umaskini na ujinga wa watanzania huzidi kudumaza fikra ,nchi yangu inapotea naona
 
Kumbe. Hata mie huwa nachanganya kati ya Kiranja na Kiranga. Nimejifunza kitu!Ni utafiti mzuri nimeupata hapo.

The name is Kiranga.

Simu hazijajibu swali. Kwa nini habari za ofisini zije nyumbani?

Ukianza kuleta ya nyumbani ofisini ndiyo unakutana na mambo tofauti.

Kwa sababu ushaanza kuambatanisha vitu tofauti, vya nyumbani na ofisini.
 
Last edited by a moderator:
Dogo tukubaliane wewe ulikua si mgeni wa mzungu. wewe ni mesenja tu ulipeleka cheki ikasainiwe wajanja wachukue hela. sasa kweli mesenja anaweza kua mgeni wa mwekezaji halafu at short notice ???!!"
 
Kwa nini habari za ofisini upeleke nyumbani?

2014 !@#$%^&*() Watu wanafanya kazi nyumbani kijana. Mimi nafanya kazi hata nikiwa kwenye Helicopter. Watu tuna ofisi za nyumbani na kule tulipo toa ajira kwenu.

Hakuna kosa kupitia makaratasi ya ofisi nyumbani. Kwa wewe mwajiriwa ndio unashangaa, utashangaa sana hapa duniani.
 
watanzania ukitaka wakutangaze dunia nzima wanyime chakula.... mbona mnapenda kulalamika sana ishu inapohusisha chakula??????? mbona wewe pia uwezo wa kununua unao? waacheni watu waishi maisha kwa mtindo wanaoupenda. kati ya mambo yanayonikwaza kwa watanzania ni ile hali ya kutaka watu waishi kwa mfumo fulani wanaoutaka wao..let people be.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom