Wazungu huwa hawaitii chakula wageni?

Wazungu huwa hawaitii chakula wageni?

Crispin Nyoni

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
413
Reaction score
90
Habari zenu!
Niliagizwa na mkubwa wangu wa kazi nipeleke hati fulani aipitie mzungu nyumbani kwake. Nikakaribishwa vizuri na mfanya kazi wake hadi sebuleni nikakuta anakula. Akaonesha ishara ya kunikaribisha kukaa kwenye sofa. Pia akanipa ishara ya kutokuongea. Nikakaa kimya. Alivyomaliza ndo akatekeleza shida yangu. Yaani hadi amemaliza kula hakukaribisha chakula kama tufanyavyo sisi waafrika. Hawa wenzetu hawana utaratibu wa kuongea wakati wa kula na hawakaribishi?
 
Ndivyo walivyo ni afadhali ungekuwa unatarajiwa ugeni wako kidogo ungepona mbali na hapo pole sana
 
Juzi baada ya kutoka kanisani, shemejio alikutolea kauli ambayo ilikutatiza kuhusu chakula na leo tena mzungu hajakukaribisha chakula. Una hatari sana mkuu.
 
Ni mroho uyo mzungu...alitakiwa kukupa gilasi ya maji...Mimi nina rafiki yangu wa Kiyahudi..nikimkuta anakula mara nyingi ananipa matunda,keki maji au ananifanya kehawa...
 
Ulimpa taarifa utaenda kula mchana kwake?
Ile ilikuwa bajeti yake mkuu na kama ulikuwa na ubao kama nakuona ulivyoteseka
 
Huo mfumo ukiuleta kwako itakuwa safi sana,jaribu mkuu na ulete mrejesho....
 
Habari zenu!
Niliagizwa na mkubwa wangu wa kazi nipeleke hati fulani aipitie mzungu nyumbani kwake. Nikakaribishwa vizuri na mfanya kazi wake hadi sebuleni nikakuta anakula. Akaonesha ishara ya kunikaribisha kukaa kwenye sofa. Pia akanipa ishara ya kutokuongea. Nikakaa kimya. Alivyomaliza ndo akatekeleza shida yangu. Yaani hadi amemaliza kula hakukaribisha chakula kama tufanyavyo sisi waafrika. Hawa wenzetu hawana utaratibu wa kuongea wakati wa kula na hawakaribishi?

kuwa na akili unapofungua thread
1.mzungu anaheshimu chakula na mda wa chakula yani ni saa ya kula tu.
2.mzungu anaratiba yake
3.mzungu anabudget
4.akukaribishe kuna share yako
5.kilichokupeleka ni kula?
6.heshimu nyumba na sheria zao

rudi shule
 
sign-do-not-disturb.jpg
clip-art-eating-959297.jpg
 
kwi kwi kwi ulitaka atoe sentensi kama ya yule shemejio ungemwambia live mzungu nataka kuonja lol
 
Mmmh !! mzungu njaa huyo ! hata kusema karibu ya uongo hakusema ..khaa, uchoyo na ubahili umewajaa...!! Kwani chakula ndo mali? Hapo angelipaliwa au kusakamwa sii angeliomba msaada ? hata wakupiga kofi mgongo?!! Hopless wadhungu na wanao wapendelea !!
 
Ni mroho uyo mzungu...alitakiwa kukupa gilasi ya maji...Mimi nina rafiki yangu wa Kiyahudi..nikimkuta anakula mara nyingi ananipa matunda,keki maji au ananifanya kehawa...
Mmmh !! mzungu njaa huyo ! hata kusema karibu ya uongo hakusema ..khaa, uchoyo na ubahili umewajaa...!! Kwani chakula ndo mali? Hapo angelipaliwa au kusakamwa sii angeliomba msaada ? hata wakupiga kofi mgongo?!! Hopless wadhungu na wanao wapendelea !!
 
Nyoni# kweli wewe na visa vya misosi ni balaa juzi shemeji yako baada kula akaueleza kauli tata na hii tena mzungu hajakukaribisha kweli unalo
 
Juzi baada ya kutoka kanisani, shemejio alikutolea kauli ambayo ilikutatiza kuhusu chakula na leo tena mzungu hajakukaribisha chakula. Una hatari sana mkuu.



Hiyo ndo jf usiichukulie serious wengine hawana kazi so hiki ni sehemu ya maisha yao.....
 
Habari zenu!
Niliagizwa na mkubwa wangu wa kazi nipeleke hati fulani aipitie mzungu nyumbani kwake. Nikakaribishwa vizuri na mfanya kazi wake hadi sebuleni nikakuta anakula. Akaonesha ishara ya kunikaribisha kukaa kwenye sofa. Pia akanipa ishara ya kutokuongea. Nikakaa kimya. Alivyomaliza ndo akatekeleza shida yangu. Yaani hadi amemaliza kula hakukaribisha chakula kama tufanyavyo sisi waafrika. Hawa wenzetu hawana utaratibu wa kuongea wakati wa kula na hawakaribishi?

Huyo alikuwa Mbwenu sio mzunu pure..... mzungu pure angekuuliza ''what are you doing here'' do you want to east something?', ok you may have a seat.... let me finish my lunch,,,,,, au angesema if dont minde let me finish my lunch.... narudia tena hakua mzungu alikua Mbwenu bojo
 
huwa hawaharibu bajeti yao kama ni sahani nne hakuna ya ziada ndo maana hawakukukaribisha
 
Kwa nini habari za ofisini upeleke nyumbani?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom