Yaani nilitegemea kuwa wewe ni mwanamke mwenye busara sana na ndio maana nikajieleza haswa kumbe walewale tu! Kuwa supported na goverment is not the reason why some people are independent in europe, trust me, ni mentality yako tu ndio itakayoamua.
Baadhi ya wanawake wa kitanzania ni waoga kupita kiasi when it comes to face challenges. Nimetoa mfano wa ndugu yangu ili upate picha kamili ya wanawake wanavyoteseka na si kwamba ninao mfano huo tu, ninayo mingi na mingine mpaka inatisha jinsi baadhi ya wanaume walivyo, mwanaume anaweza kumpiga mke wake sana kiasi kwamba mke akipata upenyo akakimbia nje anamkimbiza na PANGA mpaka barabarani watu wote wakishangaa na bila aibu anaendelea kumpiga, mbele ya watoto wake binafsi, majirani, n.k mpaka watu baki wanamwokoa huyo mwanamke and sadly, after all that humiliation still huyo mwanamke anaendelea kukaa na huyo mwanaume na nilipomuuliza kwa nini asitafute maisha yake mengine alisema hivyohivyo, "sasa jamii itanielewaje"? Sasa ni uvumilivu gani unataka huyo mwanamke awe nao hapo?
Baadhi ya wanawake wa kitanzania mnaolewa ili muonekane na nyie mmeolewa mbele ya jamii na maisha yenu yote mnaishi kwa sababu ya jamii na sio yenu binafsi, na ndio maana wengi wenu mnaoverlook tabia za baadhi ya waume mlionao kabla hawajawaoa kwa kudhani kuwa wakishaoa watabadilika, matokeo yake mambo kama hayo yakianza kuwatokea mnashindwa kutoka na kubakia kusingizia dini, dini! Ina maana mume wako atakudhalilisha kwa kukupiga kila siku tena mbele za watu na kutembea nje na wanawake, tena wengi wao wakiwa ni marafiki zako then uendelee kuvumilia kisa dini zinakataa divorce? Are you that crazy? Ni wanawake wangapi tunawaona mahospitali wakiwa wameunguzwa na moto, kukatwakatwa viungo na waume zao because they were forgiving them all the time mpaka yanawakuta makubwa zaidi? Aisee we ni kiboko, yaani kama ni kweli unasupport hao wanawake waendelee kunyanyasika ndani ya ndoa zao basi wewe ni mwanamke wa kwanza limbukeni kuliko malimbukeni wote niliowahi kukutana nao.