Wazoefu naombeni mwongozo

Natafuta Ajira

JF-Expert Member
Mar 25, 2020
505
875
Ni matumaimi yangu wote wazima.

Naombeni kujuzwa kwa kawaida inachukua muda gani kutoka siku ulipeleka barua ya posa ukweni mpaka siku ambayo utatakiwa kurudi kutoa mahari? Kama hakuna muda rasmi basi ile kibishi bishi unaweza ukawapiga kalenda wakwe kwa muda gani?

Huyu binti siku moja tulienda kwao, lengo langu lilikua kusalimia tu maana mama yake alimsisitiza sana niende akanione, kumbe walikusanyana uko, katika kupigwa pigwa maswali nikaulizwa suala la kuleta barua ya posa, nikalizima tu kwa kusema nitaleta ila sikutaja siku rasmi.

Sasa wakwe wanasema nipeleke posa, mama mkwe hana noma hata siwasiliani naye, akiongea tu na mwanae anasema msalimie mwenzako. Ila kuna uyo mama mdogo wa huyu binti ndiyo kashikilia bango ilo suala. Haipiti wiki bila kuniuliza tangu mwezi wa 4 nampiga siasa tu. Sasa nataka kumpeleka mdingi mmoja hivi akawazuge zuge watulie kidogo. Sasa kwenye sakata la kutoa mahari ndo kizaazaa, mtaa mgumu.

Kiukweli sina nia ya kumchezea huyu binti, kinachonikwamisha kumuoa ni vile tu bado life halijakaa kwenye mstari. Nataka nimchukue mdigi mmoja mtu mzima apeleke barua ya posa ukweni watulie kidogo.

Sasa je, kwa kawaida inachukua muda gani kutoka kutoa posa mpaka kupeleka mahari?
 

Killa Cam

JF-Expert Member
Jun 12, 2022
376
905
Kijana Muhuni anataka kumbeleka mtu mzima muhuni mwenziwe, kufanya mambo ya kibongo movie. Salamabichi mnatuharibia credit vijana
 

Hoaxer

Senior Member
Sep 7, 2022
106
252
Dogo chamuhimu barua tu. Wakwe zako hawana shida na mahari yako wao wewe uondoke na huo mzigo.
 

Jossephat

Member
Sep 18, 2022
5
2
Kwamimi navyojua mkuu ni kwamba barua huwa haizidishi miezi 3.kwamaana hiyo we mtume huyo mjumbe akawaambie2 mambo ya mali mungu atafungua njia amini hivyo2
 

kingkimwe

JF-Expert Member
Feb 12, 2015
835
761
Et kusalimia kwa sisi wanyamwez ni kosa kubwa sana hilo ungekula fiine kubwa sana
 
Aug 9, 2022
16
38
Ahhh mie naona afadhali uwachane ukweli tu kuwa hujakaa poa but unania njema na Binti Yao kwahyo wasubiri ujipange kilife kwanza then utakuja rasmi hizo mbelile mbelile naona hazina ishu
 

Evelyn Salt

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
57,404
86,770
Sasa nataka kumpeleka mdingi mmoja hivi akawazuge zuge watulie kidogo. Sasa kwenye sakata la kutoa mahari ndo kizaazaa, mtaa mgumu.
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂

Block ukoo wote au badili namba za simu, nimecheka.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

2 Reactions
Reply
Top Bottom