Wazo Mitume Na Manabii Hamieni Vijijini Sasa

Wazo Mitume Na Manabii Hamieni Vijijini Sasa

Wakawafanye wawe na utayari sasa utayari utatoka wapi kama manabii hawaendi, kwani wakati wamissionary wanalera ukristo sisi tuliwaambia tupo tayari.
Soma historia ya umissionary utajua injili ilikuwa ni gia tu ya kuingilia Afrika,hawa watu walikuwa na makusudi mengine. Baadae hawa ndio walikuja kututawala(wakoloni),hadi leo wanatuibia rasilimali zetu na yote kwa yote hata wao walianzia mijini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo watumishi wa sasa kama huyu gspain wameshafanya injili ni kazi rasmi ya kujiingizia kipato. Kama sikosei Yesu alikuwa seremala na wengi wa wanafunzi wake walikuwa wavuvi.
Ha haaa,mimi sio mtumishi wa madhabahuni mkuu,kwa kuongezea tu Mathayo alikuwa mtoza ushuru(TRA kwa leo),Yohana alikuwa mfanyibiashara na alikuwa na pesa kweli kweli,Yuda alikuwa Muhasibu nk nk,tafuta vitabu vinaitwa the lost bibles utajua maisha ya Yesu na Mitume wake nje ya injili mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimefikiria jinsi wananchi wanaoishi vijijini wanavyoishi katika style ambayo bado maeneo Mengi kuna uamini mkubwa Wa Nguvu za giza na baadhi kuabudu mizimu
Je si ni wakati muafaka sasa mitume na manabii waliojazana mijini kuweka kusudio LA kuhama kabisa mijini mikoa yote na kwenda kuweka makazi ya kudumu huko kuokoa roho za wanavijiji wengi wanaosumbuliwa na mapepo,imani za kishirikina,mauaji ya albino,ulozi wa mashamba na mazao
Kwa maana mijini tumeshashika neno na tumewaelewa tatizo wenzetu wa vijijini kwa kweli wanakosa kabisa huduma ya kiroho
Sie wa mijini haina shida tutaendelea tu kuwa follow katika insta na tweeter pia YouTube
Hili ni wazo tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakazia.

Vijiini kuna mambo ya ajabu ajabu yanayorudisha nyuma maendeleo. Hawa ndugu zetu wajielekeze huko pia.
Kuna maeneo hata kujenga nyumba nzuri wanaogopa kurogwa
 
Hawa manabii na Mitume ni biashara tosha, biashara inakuwa nzuri kama utatafuta sehemu yenye idadi kubwa ya watu, mwingiliano.


Uende kijijini ibada 1 hata laki ufikishi kwenye sadaka wakati mjini laki inatolewa na Muumini 1. Wakipatikana waumini 10 tayari Una Milioni kwa nini usifanye ibada Mjini utengeneze Pesa za kutosha kwa ajili yako na vizazi vijavyo.
20190109_101941.jpg
hizi atahesabu ngapi hadi afikie millioni
 
Yesu alikuja kwaajili ya watu kama hao
Nimeeleza tayari kuwa hata Yesu alihama kutoka Nazareti alipokulia na kwenda Kapernaum mji wa kibiashara ulio ufukweni ambapo ndipo huduma yake ilishamiri huko. Unapelekaje injili kwa mtu ambaye moyo wake upo kwa mganga wa kienyeji mkuu? Akienda kwa mganga anapeleka ng'ombe akija kanisani (ambapo Mungu anajidhihirisha kwa matendo km uponyaji nk) analeta sadaka jero. Mtumishi wa watu hadi kiatu kinaenda upande kwa kuchakaa,kisha afunge na kuwaombea watu hao hao wasiomtolea Mungu wake?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom