*Wazo La Leo tarehe 09/03/2013*

*Wazo La Leo tarehe 09/03/2013*

Hapo kwa mimba....mmmm
Kuna watu wanajuhudi hawazipati, ni majaliwa pia aisee
 
WAZO LA LEO; Kumbuka kujenga kwa wakwe ni sawa na kujenga kwenye hifadhi ya barabara...itakula kwako tu!
 
Kuanza Uhusiano Mpya baada ya ule wa zamani kuvunjika: ONYO

Vijana wengi wamejikuta katika mahusiano na hata ndoa na watu wasiowataka wala kuwapenda kwa sababu hawakujipa muda wa kuheal baada ya mahusiano ya mwanzo kuvunjika.

Mara baada tu ya kuvunja mahusiano wanaanzisha mapya na mara nyingine kufunga ndoa kwa haraka wakitaka kujionyesha kwa yule waliyeachana naye kuwa yupo happy wakati kiuhalisia bado hajapona jeraha lake.

Usiingie kwenye mahusiano na mtu mwingine kabla hujapona jeraha la kuvunja mahusiano. Pale utakapopona na kugundua kuwa haupo na mtu sahihi inaweza kuwa too late kurudi nyuma.

Usianzishe mahusiano wala ndoa ili kumuonyesha mtu fulani kuwa umeshamsahau na umepata zaidi yake, itakuja kula kwako…

Jipe muda, Tafakari, Mfahamu mtu kwanza ndipo uanze naye uhusiano....
 
Back
Top Bottom