TUJITEGEMEE
Platinum Member
- Nov 6, 2010
- 27,551
- 28,538
Juzi Alhamisi nilifanikiwa kufuatilia kikao cha bunge kutwa nzima. Lakini jambo nililoligundua ni kuwa kumbe tunaweza kutumia faida ya teknolojia kuokoa rasilmali mtu ambayo nadhani inaweza kufanya kazi nyingine ya kuliendeleza taifa badala ya hii anayoifanya kwa sasa.
Wakati bunge likiendelea kulikuwa na wakati bunge linakaa kama kamati na wakati mwingine linakaa kama kikao(spika akiwa active). katika mabadiliko hayo ya bunge kukaa kama kamati na baadaye kama kikao kulikuwa na askari alikuwa anakuja kuweka fimbo mezani na baadaye anarudi kuiingiza kabatini mbele karibu na meza kuu.
Binafsi nimegundua kuwa askari huyu anaweza kufanya kazi nyingine ya kulijenga taifa endapo ninyi wataalam wa teknolojia mkibuni mfumo wa kujiendesha wenyewe(automated system) kufanya kazi hiyo ya kutoa na kuingiza fimbo hiyo ya bunge kabatini.
Nadhani watu wa Programing, Computer Logic contols, na wengine katika fani ya sayansi na uhandisi mwaweza kuandaa proposal nzuri sana ambayo itahusisha pamoja na wazo langu lakini pia na uboreshaji mwingine mnaoweza kuufanya katika jengo la Bunge letu na kuipeleka kwa katibu wa Bunge amabaye atawapa mwelekeo wa namna ya kupewa kazi hiyo.
NAWASILISHA