pcman
JF-Expert Member
- Oct 9, 2008
- 742
- 186
Wana Jf
Leo nilikua Wizara ya Kilimo na Chakula Idara ya Uhasibu katika mambo ya ambayo nimesikitika ni uzembe na Ufisadi wa waziri huyu akiwa katika serekali ya Awamu ya Nne .
Wazira wasira akiwa waziri Mwaka jana mwezi 4 alitakiwa kwenda mwanza kufungua kikao cha BODI ya Pamba jamaa akakatiwa Tiketi ya Ndege Precision jamaa akalala akapitiliza matokeo yake wizara ikabidi Imkodishie Ndege ndogo wizara ikaamua kumkodishia Single engine small flight akagoma wizara ilikua ilipe Dola 8000 kwa safari hiyo kwa aina hiyo ya Ndege.
Waziri akalazimisha akodishiwe Ndege ndogo yenye Engine mbili kwa Gharama ya Dola 13,000 hii ni fedha za walipa Kodi pia Waiting Charge na Gharama za kurudi. Ambazo kwa ujumla wizara ililipa Jumla ya Dola 19,870.
Tukio la Pili ni Ufisadi wa Ununuzi wa Gari ya wizara. Mwaka Jana (2010) mwezi Juni alinunuliwa Gari VX V8 ambayo ilikuwa haina Friji ndani kwa Gharama ya Milioni 250 akalikataa akataka zuri zaidi lenye madoido akataka la Thamani ya milioni 350 likaletwa mwezi September ambalo alilitumia kwa miezi 2 kabla ya uchaguzi.
Tukio la Tatu ni Kuibeba Kampuni inayoitwa SIMON GROUP kampuni hii ilipewa Miradi yote ya Kusambaza na Kuchukua Vyakula kutoka SGR za serekali bila kutangaza Tenda, Miradi hii Mwaka Jana Peke yake walipewa Miradi Ifuatayo. SONGEA 23.5bn, Iringa 19.2bn, Rukwa 39.5bn lakini pia ikumbukwe kampuni hii ndio iliyopewa kinyemela UDA kwa bei ya KUTUPA, kampuni hii ndio iliyonunua NYUMBA ya Familia ya MARIALE kwa 1bn masaki kampuni hii ilipewa Mradi mkubwa wa kuingiza Matrekta ambayo halmashauri zimelazimishwa kununua Matreka ya aina ya POWER TILER ambayo hayana uwezo wa kufanya kazi na mengi yamekwama. TUJIULIZE SIMON GROUP NANI YUPO NYUMA YA HII KAMPUNI?
Wana JF nimeleta uchafuu huu tuujadili na tuangalie huy wasira ambae anafanya kazi kwa karibu na MKULU.
It make sense.