WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk. Aballah Kigoda awajia juu wanaodai viwanda vimekufa

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,302
2,000
WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk. Aballah Kigoda, amewajia juu watu wanaodai viwanda nchini vimekufa, jambo ambalo si kweli. Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana, wakati akizindua rasmi Ripoti ya Hali ya Ushindani wa Sekta ya Viwanda Nchini (2012).

Alisema wapo watu wanaoeneza uzushi kwa wananchi kuwa viwanda vimekufa bila kuwa na uhakika na jambo wanalolizungumza.

“Hili ni jambo ambalo kwa kweli linanikera, kwa sababu wao wanadhani viwanda vyote vimekufa, wakati si kweli, Tanzania inavyo viwanda zaidi ya 700, kwa upande wa Mkoa wa Dar es Salaam pekee kuna viwanda 432, kati ya viwanda vyote hivyo ni viwanda 15 pekee ambavyo tunaweza kusema vimekufa.

“Jukumu la kuendeleza na kuboresha mazingira ya viwanda nchini siyo la Serikali pekee, ni jukumu letu sote kushirikiana katika kuhakikisha sekta ya viwanda inakua.

“Lakini sasa kuna changamoto kubwa ambayo tunaona bado inawakwaza wananchi, kwanza ni suala la mitaji, pili ni suala la mafunzo.

“Hata hivyo, kwa kuwa sasa tunaandaa sera madhubuti kwa ajili ya kukuza sekta ya viwanda nchini, tuna uhakika sekta hii itakua na kuchangia pato la Taifa kutoka asilimia 9.7 za sasa hadi kufikia asilimia 14 ifikapo 2025,” alisema Dk Kigoda.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO), Emanuel Kalenzi, alisema kwa ujumla katika nchi za Afrika bado hazijaweza kufanikisha maendeleo ya sekta ya viwanda, ukilinganisha na nchi nyingine za Ulaya na Amerika.

“Mchango wa viwanda kwa nchi za bara la Afrika ni asilimia 10 pekee, wakati nchi za mabara mengine ni kuanzia asilimia 40 na kuendelea,” alisema Kalenzi.

Kuhusu ripoti hiyo, Mwanafunzi wa Masuala ya Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Felicia Massakcy, alisema mchango wa sekta ya viwanda katika sekta ya ajira ni asilimia tano pekee.

“Hali hii inatokana na serikali kutoweka kipaumbele katika sekta ya viwanda, tunapaswa kufahamu kuwa viwanda ndiyo sekta muhimu ambayo inaweza kukuza uchumi wa nchi kwa kasi iwapo kutakuwa na mikakati endelevu yenye tija,” alisema Felicia.

Wakati Mkurugenzi Viwanda kutoka Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Alley Mwakibolwa, alisema kukabiliana na matatizo yaliyobainishwa katika ripoti hiyo wamejipanga kuharakisha matumizi ya nishati mbadala.

“Hivi sasa kuna miradi ya makaa ya mawe na uchimbaji wa chuma ya Liganga na Mchuchuma, hii ni miradi ambayo tumejipanga kuhakikisha hadi kufikia mwaka kesho baadhi ya miradi inaanza kutekelezwa,” alisema Mwakibolwa.
 
Kirode

JF-Expert Member
Mar 25, 2011
3,569
0
Bado vinafanya kazi ni kweli g.tire inazalisha matairi kule arusha ya kutosha .........hyena.
 
Chibenambebe

Senior Member
Mar 27, 2012
148
170
Hawa watu kila kitu propaganda. Tunamwomba atutajie viwanda vinavyomilikiwa na serikali ambavyo lengo lake lilikuwa ni kuinua maisha ya walalahoi kwa sasa viko vingapi?
 
Brightman Jr

JF-Expert Member
Mar 22, 2009
1,227
1,195
Mahooookaaaaaaaaaaaaaa...........! We mama we mbavu zangu....! Kumbe viwanda vipo? Mbona sasa mashati, vitenge, viatu nk vinaingizwa toka nje jamani, na kwanini mazao yetu kama pamba nk yaende nje..?lo!
 
JERUSALEMU

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
2,880
2,000
Hana jipya! tanzania kila kitu ni siasa tu.angalia msomi wa uchumi kama yeye bado anatuambia ndio kwanza wanaandaa sera madhubuti za viwanda miaka hamsini baada ya uhuru.haiwezekani jukumu la kujenga, kuendeleza na kukuza viwanda liwe ni la kila mtanzania ndio maana kuna mgawanyo wa kazi! kuna wakulima,walimu, askari,wafanyakazi, n.k.Ni jukumu lake yeye na wizara yake kuhamasisha wafanya biashara wawekeze kwenye sekta ya viwanda na yeye awawekee mazingira mazuri ya kujenga na kuendeleza viwanda. akishindwa kazi aachie ngazi wenye uwezo waingie. haweze kuendelea kubishanna na ukweli. VIWANDA VIMEKUFA!!!!!
 
swrc

JF-Expert Member
Jun 17, 2012
442
0
mtu mpumbavu ni mpumbavu tu hata kama ama esoma namna gani, hivi anamdanganya nani wakati kila kitu kiko wazi
 
Savannah

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
239
0
Serikali na viongozi dhaifu. Akilizao zililala tangu enzi ile ya zidumu fijra za...
 
SHERRIF ARPAIO

JF-Expert Member
Aug 25, 2010
9,428
2,000
Hata Tanzania Fertilizers na Steel Rolling Mills pale Tanga bado vipo hai na vinaendelea na uzalishaji
 
  • Thanks
Reactions: MTK

FJM

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
8,083
1,225
Huyu Kidoga anaanza kulewa uwaziri! Viwanda vilivyokufa vilikuwa na impact moja kwa moja na mtanzania wa kawaida. Tanganyika packers - wafugaji; kiwanda cha maziwa Arusha - wafugaji, viwanda vya nguo - wakulima wa pamba, Tanzania Ferlizers Company - mbolea kwa wakulima (sasa hivi tunaapata mbolea aina ya NPK toka Norway).

Unless tuwe na viwanda vinvyoendana na shughuli za watazania walio wengi kama vile vilivyokufa tutakuwa tunapoteza muda. Mfugaji anauza maziwa Arusha yanapelekwa Kenya na kurudi yakiwa kwenye pakiti! Nyama ni hivyo hivyo, zao la ngozi mtindo huo huo.

Inasikitisha kama Waziri wa viwanda haoni tatizo liko wapi?
 
  • Thanks
Reactions: MTK

2c2

Member
Nov 5, 2009
98
0
CCM imewatuma kukanusha kila jambo la ukweli!hata reli haijafa
kweli hii ndo kasi zaidi ya kudanganya na kuwafanya watanzania kuendelea kuwa mapunguani kwa kuamini uongo, kama mchumi na akiwa na wataalamu waliobobea chini yake anasimama kuwadanganya watanzania kwamba viwanda vipo akitaja idadi kwa kukisia, uku wakati wanaendelea kutuambia vipo wanatuambia havijachangia soko la ajira kwa walao asilimia 5 wala havina mchango kwenye ukuaji wa uchumi napata mashaka sana na viwanda vya aina gani anazungumzia huyu Mh.
 
Kanundu

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
891
0
WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk. Aballah Kigoda, amewajia juu watu wanaodai viwanda nchini vimekufa, jambo ambalo si kweli. Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana, wakati akizindua rasmi Ripoti ya Hali ya Ushindani wa Sekta ya Viwanda Nchini (2012).

Alisema wapo watu wanaoeneza uzushi kwa wananchi kuwa viwanda vimekufa bila kuwa na uhakika na jambo wanalolizungumza.

“Hili ni jambo ambalo kwa kweli linanikera, kwa sababu wao wanadhani viwanda vyote vimekufa, wakati si kweli, Tanzania inavyo viwanda zaidi ya 700, kwa upande wa Mkoa wa Dar es Salaam pekee kuna viwanda 432, kati ya viwanda vyote hivyo ni viwanda 15 pekee ambavyo tunaweza kusema vimekufa.

“Jukumu la kuendeleza na kuboresha mazingira ya viwanda nchini siyo la Serikali pekee, ni jukumu letu sote kushirikiana katika kuhakikisha sekta ya viwanda inakua.

“Lakini sasa kuna changamoto kubwa ambayo tunaona bado inawakwaza wananchi, kwanza ni suala la mitaji, pili ni suala la mafunzo.

“Hata hivyo, kwa kuwa sasa tunaandaa sera madhubuti kwa ajili ya kukuza sekta ya viwanda nchini, tuna uhakika sekta hii itakua na kuchangia pato la Taifa kutoka asilimia 9.7 za sasa hadi kufikia asilimia 14 ifikapo 2025,” alisema Dk Kigoda.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO), Emanuel Kalenzi, alisema kwa ujumla katika nchi za Afrika bado hazijaweza kufanikisha maendeleo ya sekta ya viwanda, ukilinganisha na nchi nyingine za Ulaya na Amerika.

“Mchango wa viwanda kwa nchi za bara la Afrika ni asilimia 10 pekee, wakati nchi za mabara mengine ni kuanzia asilimia 40 na kuendelea,” alisema Kalenzi.

Kuhusu ripoti hiyo, Mwanafunzi wa Masuala ya Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Felicia Massakcy, alisema mchango wa sekta ya viwanda katika sekta ya ajira ni asilimia tano pekee.

“Hali hii inatokana na serikali kutoweka kipaumbele katika sekta ya viwanda, tunapaswa kufahamu kuwa viwanda ndiyo sekta muhimu ambayo inaweza kukuza uchumi wa nchi kwa kasi iwapo kutakuwa na mikakati endelevu yenye tija,” alisema Felicia.

Wakati Mkurugenzi Viwanda kutoka Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Alley Mwakibolwa, alisema kukabiliana na matatizo yaliyobainishwa katika ripoti hiyo wamejipanga kuharakisha matumizi ya nishati mbadala.

“Hivi sasa kuna miradi ya makaa ya mawe na uchimbaji wa chuma ya Liganga na Mchuchuma, hii ni miradi ambayo tumejipanga kuhakikisha hadi kufikia mwaka kesho baadhi ya miradi inaanza kutekelezwa,” alisema Mwakibolwa.
Bange mbaya jamani. Haka kajamaa kameuza viwanda vyetu vyote, halafu kanakuja kuropoa hovyo bila aibu!!!!! Hivi hapa Tanga anapotoka, anaona Kiwanda cha chuma kinafanya kazi? Kiwanda cha Mbolea kinafanya kazi? Tanga Sisal Spining kinafanya kazi? Somaia (CIC) kinafanya kazi? Kiran Soap kinafanya kazi? TANGOLD Korogwe kinafanya kazi? Amboni Plastic Kinafanya kazi? Tanga Blanket kinafanya kazi? Bandari tanga inafanya kazi? Tanga Timber Sales kinafanya kazi? Mkumbara Tembo Chip Board kinafanya kazi??? Hivi ni kwa uchache tu hapa Tanga. Au ndiyo hiyo kazi waliyotumwa na Vasco Da Gama ya kutuonyesha maendeleo yaliyo fanywa na CCM, ambayo kwa upofu wetu hatujayaona?
 
kanga

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
1,020

Nasema uopo juu zaidi ya Newton.Sasa mvuta sigara huyo Kigoda akiambatana na Jangili wake Kinana atasemaje?
 
DOUGLAS SALLU

JF-Expert Member
Nov 13, 2009
22,994
2,000
Ni kweli kabisa hata kile kiwanda cha baiskeli za Swala pale Mwenge kimeshamiri sana na sasa kina tengeneza bajaji, tehe tehe tehe
 
Ringo Edmund

JF-Expert Member
May 10, 2010
4,886
0
hivi kiwanda kufanya kazi au kufa kinahitaji ramli kujua?
bora
tanganyika packers
general tyre
tancut almas
zuzu tyles
kilitex
dodoma wines
tanganyika foods ltd
morogoro canvers
tanzania bag ltd
kilimanjaro machine tools
nk
nk
nk
nk...........
vyote hivi vinafanya kazi kwa akili ya kistuli.
 
  • Thanks
Reactions: MTK

MTK

JF-Expert Member
Apr 19, 2012
8,255
2,000
Hii ndio shida ya ku-recycle dead woods kwenye serikali; Kigoda ana maana hivyo 15 sio viwanda!?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom