R.B
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 6,296
- 2,573
WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk. Aballah Kigoda, amewajia juu watu wanaodai viwanda nchini vimekufa, jambo ambalo si kweli. Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana, wakati akizindua rasmi Ripoti ya Hali ya Ushindani wa Sekta ya Viwanda Nchini (2012).
Alisema wapo watu wanaoeneza uzushi kwa wananchi kuwa viwanda vimekufa bila kuwa na uhakika na jambo wanalolizungumza.
Hili ni jambo ambalo kwa kweli linanikera, kwa sababu wao wanadhani viwanda vyote vimekufa, wakati si kweli, Tanzania inavyo viwanda zaidi ya 700, kwa upande wa Mkoa wa Dar es Salaam pekee kuna viwanda 432, kati ya viwanda vyote hivyo ni viwanda 15 pekee ambavyo tunaweza kusema vimekufa.
Jukumu la kuendeleza na kuboresha mazingira ya viwanda nchini siyo la Serikali pekee, ni jukumu letu sote kushirikiana katika kuhakikisha sekta ya viwanda inakua.
Lakini sasa kuna changamoto kubwa ambayo tunaona bado inawakwaza wananchi, kwanza ni suala la mitaji, pili ni suala la mafunzo.
Hata hivyo, kwa kuwa sasa tunaandaa sera madhubuti kwa ajili ya kukuza sekta ya viwanda nchini, tuna uhakika sekta hii itakua na kuchangia pato la Taifa kutoka asilimia 9.7 za sasa hadi kufikia asilimia 14 ifikapo 2025, alisema Dk Kigoda.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO), Emanuel Kalenzi, alisema kwa ujumla katika nchi za Afrika bado hazijaweza kufanikisha maendeleo ya sekta ya viwanda, ukilinganisha na nchi nyingine za Ulaya na Amerika.
Mchango wa viwanda kwa nchi za bara la Afrika ni asilimia 10 pekee, wakati nchi za mabara mengine ni kuanzia asilimia 40 na kuendelea, alisema Kalenzi.
Kuhusu ripoti hiyo, Mwanafunzi wa Masuala ya Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Felicia Massakcy, alisema mchango wa sekta ya viwanda katika sekta ya ajira ni asilimia tano pekee.
Hali hii inatokana na serikali kutoweka kipaumbele katika sekta ya viwanda, tunapaswa kufahamu kuwa viwanda ndiyo sekta muhimu ambayo inaweza kukuza uchumi wa nchi kwa kasi iwapo kutakuwa na mikakati endelevu yenye tija, alisema Felicia.
Wakati Mkurugenzi Viwanda kutoka Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Alley Mwakibolwa, alisema kukabiliana na matatizo yaliyobainishwa katika ripoti hiyo wamejipanga kuharakisha matumizi ya nishati mbadala.
Hivi sasa kuna miradi ya makaa ya mawe na uchimbaji wa chuma ya Liganga na Mchuchuma, hii ni miradi ambayo tumejipanga kuhakikisha hadi kufikia mwaka kesho baadhi ya miradi inaanza kutekelezwa, alisema Mwakibolwa.