Waziri wa Ulinzi, Dkt. Stergomena amuwakilisha Rais Samia Siku ya Afrika Uganda

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
TUZO RAIS.jpeg

Mhe.Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) akipokea tuzo aliyozawadiwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na Pan African Women Organization (PAWO) kwa kutambua mchango wake katika Uongozi na maendeleo ya jamii tangu aingie madarakani mwezi March 2021.​


Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan kwenye Maadhimisho ya 49 ya Siku ya Afrika (Africa Liberation Day) yaliyofanyika tarehe 25 Mei, 2025 Jijini Kampala Uganda.

Akiongea katika Maadhimisho hayo kwa niaba ya Rais, Waziri Tax aliwashukuru Afrika Pan African Women Organization (PAWO) kwa Mwaliko walioutoa kwa Rais Samia pamoja na kutambua mchango wake wa maendeleo na ustawi wa jamii. Aidha, amesema Rais alipenda kuwa sehemu ya maadhimisho hayo lakini kutokana na majukumu mengine ya kitaifa na kimataifa yanayomkabili, ameshindwa kuhudhuria ndiyo maana amemtuma yeye amwakilishe.

Ameongeza kwa Kusema kuwa tangu Rais Samia aingie madarakani mwaka 2021 anakuwa Rais wa Kwanza Mwanamke kuwahi kuiongoza Tanzania na amekuwa mstari wa mbele katika kuleta maendeleo na ustawi wa jamii kwa wananchi wake na hasa wanawake na vijana. Kwa kufanya hivyo amekuwa ni mfano wa kuigwa na wasichana mashuleni, vijana wa kike, vijana na jamii kwa ujumla ambao nao wanatamani wawe viongozi wa kesho.

Ameongeza kwa kusema kuwa tunaposherekea siku ya Afrika, ambayo ni siku muhimu sana kwani imetoa fursa ya kipekee kwa kuwaunganisha pamoja kama waafrika.

Amepongeza pia, mchango mkubwa wa wanawake kutoka maeneo na mataifa mbalimbali walioshiriki katika mapambano ya kulikomboa Bara la Afrika.

Katika maadhimisho hayo Waziri amepokea tuzo aliyozawadiwa Samia Suluhu Hassan na Pan African Women Organization (PAWO) kwa kutambua mchango wake katika uongozi na maendeleo ya jamii tangu aingie madarakani mwezi Machi 2021. Aidha, Mhe. Stergomena amepokea tuzo ya Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere kama muasisi wa Umoja wa Afrika.

Akisisitiza matumizi ya Kiswahili, Waziri amesema: “Ni furaha pia kuwa tunatumia Lugha ya Kiswahili iliyotumika kutuunganisha wakati wa kupigania uhuru. Tuendelee kukienzi, kukidumisha, na kukikuza”.

Katika maadhimisho hayo, Dkt. Stergomena aliambatana na Balozi anayeiwakilisha Tanzania nchi Uganda, Balozi Dkt. Azizi Mlima na Emma Nyerere kutoka Pan Africanism Women Organization – Tanzania.
 
Back
Top Bottom