Waziri wa Nishati na Madini

si kila king'aacho ni dhahabu, ni taasisi gani aliyo wahi kuiongoza kwa mafanikio kitaifa au kimataifa? ni kosa kubwa sana kutoa credit kwa mtu just kwa kuangalia CV yake tuu, CV za kubumba na zilizochakachuliwa zipo vile vile

Kwa comment hii inaonyesha humjui kabisa profesa huyu! Angalia tu tuzo zake za kitaifa na kimataifa nadhani atleast utapata mwanga wa jibu la swali lako
 

Huyu nae atakuwa kama Benno ndulu gavana wa benki kuu ambae alijengewa nyumba na swimming pool ya bilioni moja na watu walisema ana cv ya kimataifa lakini yumeona hayo madudu chini ya utawala wake.
Balali nae alitolewa hukohuko usa na cv kubwa mwisho akatu-EPA na kusepa
 

Hii inaonyesha dhahiri kuwa tatizo linaweza kuwa sio kiongozi mmoja mmoja bali system nzima.

Hivyo basi, ila mambo yaende kama tunavyotegemea, ni vizuri kuioverhaul system nzima. Mafisadi dagaa pia washughulikiwe kwani hawa po wengi na wanakula pesa zetu zaidi ya viwavi washambuliavyo mashamba.
 
Hilo ndio suala la msingi kwa nchi hii na watu wake tuelewe hilo,kwani kwa sasa system ndio hiyo unaiona imejaa kulindana mfano tulitakiwa tuambiwe na rais ni hatua gani inafuatia baada ya kuwafukuza hawa mawaziri kama watafikishwa mahakamani au la!
Halafu tunaambiwa mkuchika amehamishwa Tamisemi wakati madudu yake huko ndo balaa la kupukutisha fedha za mlipa kodi kila siku,je alistahili kuwa kwenye baraza tena
 
Kwani performance ya Professor Kapuya ilikuwaje katika wizara zote alizoongoza mpaka mwisho akaingia kwenye dili ya kufisadi UDA???
 
"Education purpose is to replace an empty mind with an open one" mkuu tutambue kuwa kila wizara ni muhimu katika mustakabali wa maendeleo ya Taifa letu ila ni ukweli ulio wazi kuwa wizara zinatofautiana kwa umuhimu wake. Wizara ya fedha ndo roho katika harakati zote za kupigania maendeleo kwani ndiyo inayo husika na allocations za fedha katika serikali yoyote duniani.Sina tatizo na uteuzi wa wateule wa mkuu wa KAYA lakini kuna umuhimu wa kutambua kitu kimoja nacho ni uteuzi wa Bi. Saada Mkuya Salum aliyeteuliwa na Rais kuwa mbunge masaa machache kabla ya kuteuliwa tena kuwa Naibu Waziri wa Fedha. Inaonyesha ni jinsi gani tunavyo ichukulia wizara hii (VODA FASTA) na kwa hili naomba niwasilishe hoja kuwa mkuu hukufanya maamuzi sahii kulingana na wakati na alivyo uchukulia uteuzi huu. PLEASE LETS BE SERIOUS KAMA TUNATAKA KULIKOMBOA TAIFA HILI KUTOKA KWENYE MKWAMO HUU WA KIUCHUMI NA UFINYU WA MAONO.Alitakiwa kuwa na maono ya mbele zaidi ya kauli mbiu(Ari zaidi, Kasi zaidi, Nguvu zaidi) na mambo ya usawa wa jinsia
 
Without saying much, please refer the difference between Intelligence quotient (IQ) and Emotional Intelligence (EI), they said at home call it Kuerevuka KIAKILI Vs kueleimika KIUTU! You can have akili mingi sana the IQ thing ....lakni .... Unarudi nyumbani wa kwanza, unakula chakula cha watoto unalala wa kwanza ... Doest it disqualify your IQ and its CV? But where is your UTU!!

In a big picture? Chakula cha watoto inaweza kumaanisha Mirahaba ya Mali ya asili Ya TAIFA!! doest it disqualify your IQ No but, huoni hapo ni UTU katika uongozi wako is Kaputi!!

ON A Serious NOTE ... Watch out, Never ever mix up the two!!!
 
He has good cv, mimi nafikiri watanzania tumuombee afanye kazi maana ni kwa maslahi yetu wote.



Huyu prof Presentation zake juu ya sayansi technologia na innovation zimekuwa zikinikoga sana, na ana ideas nyingi mno juu ya nishati, Lakini BUDGET INATAKIWA NA NI KUBWA cha maana wazungu wataipata maana hatawakubalia kirahisi, migodi mipya itabidi itoe pato kubwa na akubaliwe kuwekeza katika nishati. Pia atumie kuombwa ushauri katika sayansi na technologia. Anyway imeprove tena kuwa ukiwa msomi uaweza kuchaguliwa kutokana na usomi wako wa kimataifa NA SI KUJIPENDEKEZA NA KUDHALILISHA TAALUMA KAMA DR BANA, HIVI JK ALIMSAHAU DR BANA NINADHANI ALIPASWA KUMUAZNSHI WIZARA YA PROPAGANDA ILI AMUTOE UDSM.
 
No way out. Hatuwezi kutegemea mtu mmoja kama huyo Muhongo kuleta mabadiriko.We can not make changes if we are not for changes.
 
Kwenye siasa hakuna cha man of honor.

namuombea mazuri asitekwe na mafisadi na hili alilionyesha alipokuwa Stamico:makaa ya mawe akiyasimamia TZ inauaga umasikini achilia mbali gas tuliyonayo
 

Kaka Siasa haina BA, MA wala PHD usimwogope mtu kwa ajili ya qualifications zake... Je, atweza kufanya kazi ndani ya Chama ambacho rushwa ni ORDER OF THE DAY na Serikali ambayo ipo corrupt na demarcation lines za Mihilili mitatu ya dola ni compromized? Lets wait and see... Magembe ana PHD, Kawambwa ana PHD, Mbarawa ana PHD wamefanya nini hata kuacha LEGACY... afadhali hata ya Kanumba aliigusa mioyo ya watu ... kama una bisha angalia NYOMI ya watu katika MSIBA wake!!
 
An academician turned politician...

Tusitegemee chochote toka kwa huyu mwanataaluma katka siasa za mikiki mikiki za kibongo!!

Wait and see!!
 
Ukiishi na wezi sio lazima na wewe uwe mwizi.
Ni maamuzi yako ndo yatakufanya either you join them or do away with them
Akili kumkichwa


But you are likely to be suspected!!
 

Mkuu ni kweli jamaa ni kichwa kizuri sana. Nimewahi kuhudhuria presentation yake kwenye mkutano mmoja it was supa. Kinachotakiwa ni kwamba aachwe afanyekazi zake kwa uhuru na awe ngangari kama alivyo Magufuli bila kuangalia sura ya mtu. Tatizo huwa ni pale rais anapokuwa mwizi kwa kuwatumia mawaziri wake. Nakumbuka imewahi kuripotiwa kuwa JK ni rafiki wa karibu sana na jamaa moja aitwaye "Sinclair" ambaye ni fisadi mkuu wa madini yetu. Huyu jama aliipata ile ripoti ya kamati ya madini hata kabla haijafika Bungeni na tuliona mapendekezo ya kamati hiyo hayakufanyiwa kazi. Kumbuka pia Kikwete aipoingia madarakani alitamka kuwa hatutasaini tena mkataba wa kinyonyaji wa kuchimba madini, lakini haukupita muda mrefu Karamagi akaenda kusaini mkataba "gizani" wa Buzwagi huko London na hakufanywa kitu. Hii inaonyesha kuwa huenda Kikwete anahusika kufisadi madini yetu. Kikwete pia amewahi kutamka kuwa hamfahamu mmiliki wa DOWANS kitu ambacho si kweli na hii pia inaonyesha kuwa kwenye nishati huenda nako pia ana sehemu katika ufidasi huo. Kwahiyo Huyu Prof. ana kazi kubwa mbele yake.
 
Hata Waingereza walikuwa na matumaini kama hawa kwa Godorn Brown ,maana jamaa alikuwa kichwa kwny mambo ya uchumi na alifanya vema wizara ya fedha, lakini alipokuwa PM mambo hayakwenda kama walivyotarajia so tumpe muda tuone
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…