Waziri wa Nishati anafanya nini kikaoni wakati Nchi iko gizani?

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,175
22,697
Nimekuona kwenye Runinga Mheshimiwa Naibu waziri Mkuu, Dotto Biteko ukimwagiza Maharage Chande kutohudhuria kikao Cha kimataifa kinachojadili masuala ya Nishati Ili aende akaungane na watendaji wenzie kutatua changamoto ya umeme.

Kilichonishangaza Mimi Mwananchi mzalendo ni kuwa, umemwacha Waziri wa Nishati kuendelea na kikao ilhali anahitajika kushirikiana na Maharage Chande na team yake kuhakikisha hatukai gizani.

Enzi zile Magu akiwa waziri wa ujenzi, akipata taarifa kuhusu kuharibika Kwa miundombinu ya barabara na kulazimika Kutoka bungeni haraka kwenda site kutatua changamoto Kwa ukaribu, huyu waziri wa Nishati anafanya nini mkutanoni wakati Nchi Iko gizani?

Nasisitiza, ninayemuulizia ni Waziri wa Nishati, yule Naibu waziri mkuu hahusiki hapa.

Karibuni tujadili HOJA,ila wakurupukaji njoni Polepole🙏
 
Back
Top Bottom