Waziri wa Mifugo na Uvuvi aivunja Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Maziwa nchini

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameivunja Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Maziwa nchini kutokana na kutoridhishwa na utendaji wa Bodi hiyo

Bodi hiyo imevunjwa kuanzia leo Agosti 22 chini ya kifungu cha sheria ya Bodi ya Maziwa namba 8 ya mwaka 2004 kifungu cha 8 na 9(1)

Bodi ya Maziwa nchini ina majukumu ya Kusimamia, Kuratibu na Kuendeleza tasnia ya maziwa nchini
 
Bodi ya kipumbavu kabisa, wafugaji Mwanza hawana soko la maziwa mpaka wamejiundia kijichama chao na kuanzisha mchakato wa kutengeneza sehemu ya kukusanyia maziwa yao ilhali bodi ya maziwa ipo na wanakula mishahara bure.
 
Mpina yuko sahihi kabisa hawa jamaa walikuwa wanapokea mishahara ya bure, kila product ikiundiwa bodi kuna siku tungesikia kuna bodi ya Mayai.
 
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameivunja Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Maziwa nchini kutokana na kutoridhishwa na utendaji wa Bodi hiyo
Bodi hiyo imevunjwa kuanzia leo Agosti 22 chini ya kifungu cha sheria ya Bodi ya Maziwa namba 8 ya mwaka 2004 kifungu cha 8 na 9(1)
Bodi ya Maziwa nchini ina majukumu ya Kusimamia, Kuratibu na Kuendeleza tasnia ya maziwa nchini
Bodi mbili za nini, bodi inayoisimamia bodi! Bodi moja inayosimamia viwanda vya maziwa inatosha, kuwa na bodi inayosimamia bodi ni kwamba bodi inayosimamia kiwanda haiaminiki kiutendaji hivyo na yenyewe inaundiwa bodi.
 
Ningepewa wasaa wa kuishauri serikali kwenye inshu ya maziwa ningesema tu
Mosi, serikali ilipaswa kutengeneza vyama vya Ushirika vya maziwa maana yake kungekuwa na soko la uhakika
Mbili, watoto watanzania below 5 yrs wangekuwa wanapewa maziwa bure kwenye public schools.
Faida,
Hii ingepelekea kuongeza ufugaji wa tija na ingepunguza tatizo la ajira kabisa
Pia, tungeandaa kizazi cha watoto wenye Afya ya kiakili ambao watalitumikia taifa ili kwa siku za usoni.
Maziwa ni dhahabu iliyo kwenye majani. Tunaejua hilo tunaona kuna fursa tunaichezea
Asante
 
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameivunja Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Maziwa nchini kutokana na kutoridhishwa na utendaji wa Bodi hiyo

Bodi hiyo imevunjwa kuanzia leo Agosti 22 chini ya kifungu cha sheria ya Bodi ya Maziwa namba 8 ya mwaka 2004 kifungu cha 8 na 9(1)

Bodi ya Maziwa nchini ina majukumu ya Kusimamia, Kuratibu na Kuendeleza tasnia ya maziwa nchini
WATANZANIA TUMEKUWA TUNACHEZA SANA NA THEORY ZA KUONGOZA MIFUMO YA NCHI IKIWA NI PAMOJA NA KUONGOZA SEKTA MBALIMBALI NA KUJIPA MAISHA MAGUMU BILA SABABU ZA MASINGI JAMBO LA KUJIULIZA NINI MAANA YA SEKTA BINAFSI KATIKA UANDAAJI WA SERIKALI YA VIWANDA?

PRIVATE SECTOR NI MAAMUZI YA KUONGOZA TAASISI AU PRIVATE SECTOR NI FEDHA (MISHAHARA) ZA KUONGOZA TAASISI?

MFANO
TPDC
STAMICO
MRI
TANROAD

HAKIKA HAKUNA ANAYEINGILIA MAAMUZI YA STAMICO, TANROAD N.K IKIWA NI KULIPA FIDIA? KUELIMISHA JAMII>>>> N.K

KILA LA KHERI KATIKA MAPAMBANO YA MITAJI ISIYO FIKIWA KWA KIZINGIZIO CHA PRIVATE SECTOR...

KWA MUJIBU WA RAISI MWANAMKE LIBERIA UJAMAA ULIOELIMIKA NDIO UMESHINDA.... TUTAWAJIBU TU

HALMASHAURI YA KICHWA (AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKWAKO/MBAYUWAYU)
 
Ningepewa wasaa wa kuishauri serikali kwenye inshu ya maziwa ningesema tu
Mosi, serikali ilipaswa kutengeneza vyama vya Ushirika vya maziwa maana yake kungekuwa na soko la uhakika
Mbili, watoto watanzania below 5 yrs wangekuwa wanapewa maziwa bure kwenye public schools.
Faida,
Hii ingepelekea kuongeza ufugaji wa tija na ingepunguza tatizo la ajira kabisa
Pia, tungeandaa kizazi cha watoto wenye Afya ya kiakili ambao watalitumikia taifa ili kwa siku za usoni.
Maziwa ni dhahabu iliyo kwenye majani. Tunaejua hilo tunaona kuna fursa tunaichezea
Asante
Wangeenda mkoani Kilimanjaro wakajifunza. Kuna kipindi nilienda kule wilaya ya Hai, wako juu sana. Vyama vya Ushirika kwenye maziwa na ufugaji wa ngombe wa Maziwa wako mbali sana.
Shida ninayoiona nchi hii, kila kiongozi anayekuja ana bifu zake na mipango yake kuona waliopita hawakufanya chochote. Aibu kubwa!!
 
Hii wangelifanyia kazi pia lingepunguza ufugaji holela na ungebaki ufugaji wa tija ambao pia ni rafiki kwa mazingira na kuongeza ajira kwa wahitimu wetu.

Mfano, Sisi Tanzania ingawa tunasifika kwa kuwa na ng'ombe wengi kulinganisha na nchi yoyote huku kusini kwetu kwa jangwa la Sahara lakini hatuongozi kwenye uzalishaji wa bidhaa ya aina yoyote ya mifugo yaani maziwa wala ngozi wala nyama wala kwato au pembe.

Hii ni sababu ufugaji wetu hauna tija kuachilia mbali changamoto za magonjwa na ombwe la kisera na utashi wa kawaida kabisa wa serikali zetu kuwekaza kwenye ufugaji.
 
Mpina yuko sahihi kabisa hawa jamaa walikuwa wanapokea mishahara ya bure, kila product ikiundiwa bodi kuna siku tungesikia kuna bodi ya Mayai.

Bodi ya Sungura yaani ni mwendo wa bodi kwa kwenda mbele.
 
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameivunja Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Maziwa nchini kutokana na kutoridhishwa na utendaji wa Bodi hiyo

Bodi ya Maziwa nchini ina majukumu ya Kusimamia, Kuratibu na Kuendeleza tasnia ya maziwa nchini
Bodi ya maziwa yepi, yale aliyoyasema Raisi Samia au ya kunywea chai? Maana usikute kuna Bodi imeundwa wanawake wasipoteze maziwa yao kwa mazoezi na kukosa wanaume wa kuwaoa!

Sikubali Bodi ya kusimamia maziwa ya my wife wangu I say!
 
Back
Top Bottom