Waziri wa Mazingira na siasa za kuchimba mchanga jimbo la Kawe

Bulesi

Platinum Member
May 14, 2008
14,210
13,724
Hivi karibuni waziri wa mazingira akifuatana na mbunge wa jimbo la Kawe na Viongozi wengine wa wilaya ya Kinondoni walifanya mkutano na wadau kuhusiana na kuchimba mchanga kutoka vyanzo mbalimbali vya mito jimboni humo. Sababu ya kuitiswa mkutano huo ni malalamiko ya wenye magari ya kubeba mchanga yaliyokamatwa na kuzuiwa na polisi kwa siku kadhaa ili hali walisema walikuwa na vibali vya kuchimba na kubeba mchanga.

Mbunge wa jimbo la Kawe aliwalaumu askari polisi kwa kuwakamata wenye magari hayo ingawa walikuwa na vibali. Baada ya majadiliano na hao wadau kama kawaida ya wanasiasa, waziri akaunda tume ambayo ilipewa siku saba kuja na ushauri wa jinsi ya kulitatua suala hilo la uchimbaji mchanga.

Vijana wengi katika jimbo la Kawe wanajihusisha na shuhuri za kuchimba mchanga katika mto Kawe na mto Ndumbwi. Katika uchimbaji wao mchanga huo wanapanua kingo za hiyo mito kiasi kwamba mvua zikinyesha mito hufurika na kuharibu viwanja na nyumba za Watu. Hilo liko wazi sana na waziri hana budi kujionea mwenyewe uharibufu unaofanyika na wajimbaji hawa sehemu ya daraja lijulikanal kama daraja la Malecela hapo Kawe.

Ukifika hapo utaona jinsi uchimbaji huo wa mchanga ulivyopanua kingo za mto kiasi kwamba daraja hilo muda si mrefu litakuja zolewa na maji. Kuruhusu uchimbaji wa mchanga kwenye mito karibu na makazi ya watu inahatarisha mali za watu na madaraja yanayounganisha sehemu mbalimbali.

Katika mkutano huo wachimbaji walijitetea kuwa wao huchimba mchanga ili kuzuia mafuriko kwani wao huchimba katikati ya mito. Utetezi huo hauendani na hali halisi kwani mali na madaraja yako hatarini kwa sababu ya jinsi mito inavyopanuliwa. Waziri hana budi kuweka siasa pembeni juu ya suala hili kwani uchimbaji wa mchanga ni sula la sayansi ya mazingira.

Hapo Kawe Diwani ni mdau mkubwa wa uchimbaji na uharibifu wa mazingira; hao wachimbaji wa mchanga hugawana na viongozi hao wa mtaa mapato ya mauzo ya mchanga wanaochimba. Pia huyo diwani anahusika moja kwa moja na uuzaji wa viwanja sehemu ambayo mto Ndumbwi unaingia baharini na kuharibu mazalia ya samaki kwenye mikoko. Diwani anaishi sehemu hizo hivyo hawezi kusema hajui uharibifu unaoendelea huko.

Waziri hana budi kulinda mazingira kama jukumu lake la kwanza, uchimbaji wowote wa mchanga kwenye mito mijini ni hatari kwa miundombinu na mali za watu. Serikali imetenga sehemu maalum nje ya jiji ya kuchimba mchanga na sio katikati ya jiji. Kuruhusu uchimbaji mchanga mitoni kama njia ya kuzuia mafuriko haina ukweli wowote isipokuwa uharibifu!
 
Suluhisho ili mto usipanuke ni kujenga ujuta wa mawe kando ya mto.

It is easier said than done. Nenda pale daraja la Malecela halafu angalia kwa juu ya daraja mto unakotoka na chini huko mto unako kwenda baharini utaona jinsi uchimbaji wa mchanga ulivyoharibu kingo za mto na kuharibu mali! Hata kujenga ukuta kama unavyoshauri ni mtihani!!

NEMC wana kila sababu ya kumshauri waziri kama walivyofanya huko nyuma , kupiga marufuku uchimbaji wa mchanga mitoni katikati ya miji na pia kupiga marufuku kilimo cha mahindi na mboga kando kando ya mito!!
 
Back
Top Bottom