Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene, tochi za barabarani zimeanza kuwa kero tena

Ninaomba nisaidiwe kujua hapa mjini dsm trafiki kazi yao kubwa ni ipi haswa. Maana naona wamejaa barabarani wakisimamisha haswa gari za mizigo, mara wanashika tochi kuangalia over speeding lakini inapotokea ajali ni mpaka uwatafute ndio wanakuja kwenye ajali au ikitoke foleni ambayo ilitakiwa trafikia afike haraka kuruhusu magari huwa wanapotea.

Elimu inahitajika zaidi kwa umma kujua kazi za askari wetu hawa wa barabarani, haki kwa raia na wajibu wetu kwao maana wengine anakulazimishia kosa na kukimbilia kukuandikia fine. haina mantiki wajazane sehemu moja kusimamisha magari tuu bila ya sababu. Guokoe hizi fedha zikatoe mikopo kwa vijana.
 
Kuna mmoja nadhani hawezi kunisahau nilimkatalia katakata akasema twende mahakamani nikamwambia twende akaniitia kikosi cha watu watano na akina dada juu wakasema watanilaza ndani nikawajibu sawa twendeni. Mimi simpi Trafiki documents zangu mfano kibali cha kuendeshea ama leseni ya udereva na kadi ya gari mpaka kuwepo na kosa hasa la msingi. Haya mambo ya kubambikiana kesi kwangu hapana tutaenda mahakamani tu. Na ukiwaambia uende nao mahakamani hawataki maana wanajuana hawana ushahidi. Watanzania tunalile jambo la kusema naogopa kupoteza muda wangu unampa 20 ama 10 ila kumbuka umepoteza rasilimali Fedha.
Sasa sisi tutakula wapi
 
Swala sio kichakani ,hilo eneo linasomekaje spidi
Tatizo akikaa kichakani hawezi kukusimamisha kukuonesha kosa lako, sijui kama unaelewa?? Akiwa kakaa sehemu sahihi anakupiga picha anakuonesha papo kwa papo kwamba kibao kile pale cha 50Kph umepita na 60 nakuandikia faini kiroho safi unatoa leseni na namba ya simu unachorewa ukafie mbele

Sasa ile ya picha wanakupiga sehemu yoyote uko na spidi 80 unakuja kuoneshwa picha tu ya gari lako na spidi yake hakuna ushahidi kama kuna speed limit. Huo ndo ujanja wao.....nadhani kama ww ni dereva itakua ushakutana na huu usumbufu ambao Mabendera Lugola aliupiga marufuku ila sasa umerudi naona kama mwezi mzima sasa wameanza kutumia vipicha vya watsapp tena
 
Basi kama hata eneo LA spidi binafsi wanapiga ,eneo LA spid ya serikali inakuaje .umesomeka
 
Unapigwa hata Kama sio eneo la speed 50
Changamoto ,ningekua waziri ningewasha gari langu binafsi harafu nielekee Dodoma au nitoke Dodoma Moro..piga pama lakufa MTU na penzi pakiti ya sigara kila nikisimamisha naiwasha sport yangu .10000 nawapa tunamalizana nyuma ya gari yangu napakia Joseph awe anapiga picha.
 
Utakua husafirigi na gari yako ukapata hii adha wewe. Huyu mkuu yupo sahihi 100%. Mimi juzi naenda arusha..vibao vyote vya 50 nimevitii...halafu nakuja kusimamishwa kwenye mzani pale kabla ya wami kwamba nimepigwa tochi natembea speed 80 kwenye eneo la 50...kitu ambacho najua 100% sio kweli. Bahati nzuri gari kama 5 nyingine zikasimamishwa...wote eti wamepigwa tochi wanatembea speed 80.. mpaka wale matraffic wakaona aibu kwa wizi wa wazi waliokua wanafanya wakatuachia. Yaani kikosi cha traffic inabidi kifumuliwe kabisa kisukwe upya na wale vijana wapya waliotoka mafunzoni ambao bado ni samaki wabichi wanaweza kufundishwa maadili.
Hilo eneo kati ya wami mpaka mpakani mwa Pwani na Tanga(Manga nafikiri)....hata ufuate sheria ya vibao vyote lazima wakuonyeshe picha kwamba umezidi.....kuna ujanja wanatumia bado sijaung'amua ...naendelea kuchunguza!
 
Huyo demu nitakayemuonga labda uwe wewe. Upo tayari nikuonge. Wapi umeshaambiwa kuna uhalali wa kumpa trafiki pesa? Kaomba kazi na mshahara anapewa.
Ila kila baya lenye mwanzo lazima lina mwisho, na wale matrafki wapenda rushwa, ambao sio wote, wana wakati mfupi sana kazini, uroho wao ndio mwisho wa kazi zao nzuri kwa taifa...
 
Hayo yalikuwa yameisha, na kwa hili ninampongeza Sana kangi lugola.
Ila Sasa hivi wameanza tena kwa Kasi kubwa sana
mkuu safiri usiku mimi huwa naondoka dsm saa 3 usiku kabla hapajakucha niko dodoma huwa natenga kama 10k tu kwaajili ya kuwapa hela ya kahawa elfu mbili mbili checkpoint ya kibaha, dumila na kule mbelembele....ila macho yawe bomba vinginevyo tutakuokota mtaroni..
 
mkuu safiri usiku mimi huwa naondoka dsm saa 3 usiku kabla hapajakucha niko dodoma huwa natenga kama 10k tu kwaajili ya kuwapa hela ya kahawa elfu mbili mbili checkpoint ya kibaha, dumila na kule mbelembele....ila macho yawe bomba vinginevyo tutakuokota mtaroni..
Shida ya usiku sio wote tunao uzoefu wa kuendesha usiku jumlisha na yale mataa ya malori hukawii kuingia mtaroni
 
Tatizo hawa traffic police wamehalalisha kazi yao kuwa ndio namna ya kupata hela ya ziada yaani kamradi ka pembeni. Hapa Arusha atakusimamisha akukague tyre,fire extinguishers, triangle brake lights na plate numbers light anakuta vyote sawa hapo sasa ooh naombahela ya kula pumbavu zao
 
Back
Top Bottom