Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene, tochi za barabarani zimeanza kuwa kero tena

Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
18,174
27,223
Binafsi zamani niliwahi kuwa mhanga mkubwa wa tochi za barabarani kwa kuwa huwa ninasafiri sana(private) Kati ya dar-moro na dar-dodoma.

Kero kubwa hapo zamani ilikuwa unapigwa tochi kichakani na Mtu alafu baadae Kama baada ya km 10 unakutana na trafiki anakusimamisha anakuonyesha picha kwenye simu.

Ikiwa hata haina ushahidi wa kweli Kama ulizidisha hizo speed.
Hili suala liliondoka baada ya aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani kipindi Cha Magufuli kangi lugola kulipinga.

Kangi alikuweza kuliondoa na ikabaki unapigwa tochi eneo la tukio na unasimamishwa hapohapo huku ukionyeshwa kwenye tochi na kibao ambapo ume-overspeed.

Na hata baada ya kangi kuondolewa nakumbuka hili suala simbachawene uliendelea nalo. Ila ghafla Sasa hivi naona limerudi tena kwa Kasi Sana.

Hata hili mpaka tukaseme kwa Mama Samia? Kwa nini ule utaratibu usirudi? Kupigwa tochi mbali huko kichakani alafu baada ya kama km 20 unakutana na trafiki wanakusimamisha na kukuonyesha picha kwenye simu sio sawa maana hakuna hata ushahidi Kama ulizidisha kweli.

Juzi ijumaa niliona ugomvi mkubwa sana, na Mimi pia nilikuwemo kwenye mmoja wa waliosimamishwa kwa ku-overspeed, picha zimepigwa kilomita kadhaa nyuma Ila hazionyeshi Kama tulikuwa eneo ambalo tunapaswa kutembea chini ya speed 50.

Hili suala simbachawene tunakuomba uliangalie na ulitolee tena tamko. Trafiki wameanza kusumbua sana na ugomvi imeanza kuwa mkubwa.

Tunakuomba Simbachawene tunakuomba Sana, sisi wengine kwa mwezi tunasafiri private hata Mara 3 safari ndefu kwenda kwenye shughuli za ujenzi wa taifa.

NB: Picha haihusiani na eneo la tukio, Bali ni mfano wa kibao Cha speed

Screenshot_20210425-114221_1.jpg
 
Kuna mmoja nadhani hawezi kunisahau nilimkatalia katakata akasema twende mahakamani nikamwambia twende akaniitia kikosi cha watu watano na akina dada juu wakasema watanilaza ndani nikawajibu sawa twendeni. Mimi simpi Trafiki documents zangu mfano kibali cha kuendeshea ama leseni ya udereva na kadi ya gari mpaka kuwepo na kosa hasa la msingi. Haya mambo ya kubambikiana kesi kwangu hapana tutaenda mahakamani tu. Na ukiwaambia uende nao mahakamani hawataki maana wanajuana hawana ushahidi. Watanzania tunalile jambo la kusema naogopa kupoteza muda wangu unampa 20 ama 10 ila kumbuka umepoteza rasilimali Fedha.
 
Tii Sheria. Bila shuruti
Utakua husafirigi na gari yako ukapata hii adha wewe. Huyu mkuu yupo sahihi 100%. Mimi juzi naenda arusha..vibao vyote vya 50 nimevitii...halafu nakuja kusimamishwa kwenye mzani pale kabla ya wami kwamba nimepigwa tochi natembea speed 80 kwenye eneo la 50...kitu ambacho najua 100% sio kweli. Bahati nzuri gari kama 5 nyingine zikasimamishwa...wote eti wamepigwa tochi wanatembea speed 80.. mpaka wale matraffic wakaona aibu kwa wizi wa wazi waliokua wanafanya wakatuachia. Yaani kikosi cha traffic inabidi kifumuliwe kabisa kisukwe upya na wale vijana wapya waliotoka mafunzoni ambao bado ni samaki wabichi wanaweza kufundishwa maadili.
 
Pole. Kero hii itapungua usafiri wa treni jkianza. Hutolazimika kusafiri ya gati yako tena hivyo kuepuka usumbufu wa tochi.
Hapa kuna ukweli hasa hata hawa Tarfiki wa Dar huu mradi wa mwendokasi ukitengemaa na kuwa wa uhakika na watu wakaacha kutumia daladala na usafiri binafsi hawa wapuuzi wakatafute kazi. Wanajiona sana miungu wa barabara.
 
Kweli mkuu,Hili mwenyew mwezi ulioishi limenikuta njia ya kwenda Tanga. Yaani nilikuwa makini sana na alama za barabarani lakini cha kushangazi kuna sehemu nilifika nikaambiwa nimezidisha mwendo. Nikaomba kuonyeshwa ni wapi wakawa wakali bila sababu za msingi.Hili nimeliweka kichwani kwangu ni vile tu nilikuwa sitaki kupoteza muda wangu.

Nilivyokuwa narudi ilinibidi niwe makini zaidi, kitu nilikuja kugundua barabara ya kwenda Tanga Alama nyingi za barabarani hazipo. Je mtu kama mimi niliekuwa napita njia ile kwa mara ya kwanza ningeweza vipi kufahamu.
 
Kuna mmoja nadhani hawezi kunisahau nilimkatalia katakata akasema twende mahakamani nikamwambia twende akaniitia kikosi cha watu watano na akina dada juu wakasema watanilaza ndani nikawajibu sawa twendeni. Mimi simpi Trafiki documents zangu mfano kibali cha kuendeshea ama leseni ya udereva na kadi ya gari mpaka kuwepo na kosa hasa la msingi. Haya mambo ya kubambikiana kesi kwangu hapana tutaenda mahakamani tu. Na ukiwaambia uende nao mahakamani hawataki maana wanajuana hawana ushahidi. Watanzania tunalile jambo la kusema naogopa kupoteza muda wangu unampa 20 ama 10 ila kumbuka umepoteza rasilimali Fedha.
Mkuu sasa fikiria uko njiani unawahi dili la kukupa 10M...utaiacha hiyo 10M ili ukapambane mahakamani kukwepa fine ya 30,000? Mimi kawaida huwa nawaambia waniprintie hiyo fine..halafu baadae nikipata muda naendaga makao makuu ya traffic pale karibu na waterfront kuchallenge hiyo fine..uzuri kwenye gari yangu nina kicamera nimefunga kwa mbele kinarecord movement zangu zote si nakuaga na ushahidi
 
Tukipiga kelele kwa umoja wetu hawa wala rushwa trafiki wataacha ujinga. Nasikia tetesi sijui kuna mmoja alishika gari la samaki la mzee wa Pwani wale samaki wakaoza na yeye huyo trafiki wakapoteza. Tukishindwa kusaidiwa na serikali nguvu za giza zitumike kuwaondoa hawa Washenzi wamejiwekea utaratibu wa kuchukua hela kila siku asubuhi kwenye daladala.
 
Utakua husafirigi na gari yako ukapata hii adha wewe. Huyu mkuu yupo sahihi 100%. Mimi juzi naenda arusha..vibao vyote vya 50 nimevitii...halafu nakuja kusimamishwa kwenye mzani pale kabla ya wami kwamba nimepigwa tochi natembea speed 80 kwenye eneo la 50...kitu ambacho najua 100% sio kweli. Bahati nzuri gari kama 5 nyingine zikasimamishwa...wote eti wamepigwa tochi wanatembea speed 80.. mpaka wale matraffic wakaona aibu kwa wizi wa wazi waliokua wanafanya wakatuachia. Yaani kikosi cha traffic inabidi kifumuliwe kabisa kisukwe upya na wale vijana wapya waliotoka mafunzoni ambao bado ni samaki wabichi wanaweza kufundishwa maadili.
Mkuu mwenyew speed ilikuwa 80
 
Mkuu sasa fikiria uko njiani unawahi dili la kukupa 10M...utaiacha hiyo 10M ili ukapambane mahakamani kukwepa fine ya 30,000? Mimi kawaida huwa nawaambia waniprintie hiyo fine..halafu baadae nikipata muda naendaga makao makuu ya traffic pale karibu na waterfront kuchallenge hiyo fine..uzuri kwenye gari yangu nina kicamera nimefunga kwa mbele kinarecord movement zangu zote si nakuaga na ushahidi
Nimekuelewa kama kuna fursa ya kuchallenge kosa. Hii elimu inatakiwa iwe wazi.
 
Kuna mmoja nadhani hawezi kunisahau nilimkatalia katakata akasema twende mahakamani nikamwambia twende akaniitia kikosi cha watu watano na akina dada juu wakasema watanilaza ndani nikawajibu sawa twendeni. Mimi simpi Trafiki documents zangu mfano kibali cha kuendeshea ama leseni ya udereva na kadi ya gari mpaka kuwepo na kosa hasa la msingi. Haya mambo ya kubambikiana kesi kwangu hapana tutaenda mahakamani tu. Na ukiwaambia uende nao mahakamani hawataki maana wanajuana hawana ushahidi. Watanzania tunalile jambo la kusema naogopa kupoteza muda wangu unampa 20 ama 10 ila kumbuka umepoteza rasilimali Fedha.
Wewe nawe njaa tu ukipelekana mahakamani muda unapoteza na hamjui time is money. Tatizo lenu mkikamata vijichenji mnakuwa na viburi na wabishi. Ukimpooza elfu 30 tu hata laki tu utapungukiwa nini? Mnachezechezea vijichenji vyenu hovyo hovyo kununulia mademu iPhone na bia badala muwapige JEKI vijana wetu barabarani. Mnaenda mahakamani mnapoteza muda. Mimi nawapaga hadi million
 
Hii faini ya overspending ya watsapp nilishakataa kulipa mimi aisee.

Yaaani Niko radhi nipoteze muda kupinga hii kitu(Mpare anauza ng'ombe kwa kesi ya njiwa😂😂)

Siku hizi wanabambikia sana. Traffic anatakiwa umuone na akuonyeshe picha kutoka kwenye kamera sio watsapp

Wanachotishiaga ni kukulaza lockup inabidi uwe kiburi tu....kuna siku nilisharudi nao km 20 kwenda kutafuta hilo eneo walipochemsha eti wanaanza kuniomba hela na nishapoteza karibu masaa 3 nikagoma nikawaacha nikasepa
 
Hapa kuna ukweli hasa hata hawa Tarfiki wa Dar huu mradi wa mwendokasi ukitengemaa na kuwa wa uhakika na watu wakaacha kutumia daladala na usafiri binafsi hawa wapuuzi wakatafute kazi. Wanajiona sana miungu wa barabara.
Huo sijui utakuwa ni mwaka gani!!!kwa staili hii bus linakuwa natatizo dogo tu, linatolewa vifaa vizima, vinahamishiwa kwenye gari lingine??ndani ya kipindi cha miaka mitano mabus karibia 60, yamekufa!!!ila waafrika tuna laana!!!hapa labda serikali ache sekta binafsi ndio itoe huduma hizo!!nadhani UDART, kwa sasa ingekuwa mbali,
 
Kweli kabisa. Hii UDART ya sasa hakuna mwenye gari yake private atapaki akapande zile bus zao...labda waboreshe huduma sana...bus ziongezwe ili sisiwe zinajaa vile
 
Back
Top Bottom