sodoliki
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 2,593
- 2,016
Kwanza ni dharau kwa KKKT, unawaambia wmejibu barua batili?, lazima walipelekewa original, mnatia aibu na hizo elfu saba mnazolipwaKwa maneno mafupi waziri wa mambo ya ndani JIPU, unawezaje kumfukuza mtu kwa barua batili? si angesema tu hiyo ni barua batili haihusiani na serikali na tutawatafuta wote wanaosambaza barua batili, lakini ukisema ni barua batili halafu unamfukuza msajili maana yake ile barua sio batili tena, hiyo ni 100% imetoka katika wizara yake, niliwahi sema hapa katika mawaziri wasiojitambua mwiguru yumo,tulianza na kibiti wananchi walipopiga kelele ndo kwa mbali akachukua hatua, tukaja na watu wasiojulikana, tukaja polisi kupiga raia na kuua, leo kaja na kituko cha maaskofu,maelezo yake yote yanakinzana, mara technologia watu wanaweza wakarekebisha heading, nimeona nyaraka mbalimbali, barua ni batili, sasa hapo tuelewe kipi, barua imetoka serikali au haijatoka serikali? kama imetoka serikali nani kahusika kwa misingi ipi? ameitisha press conference baada ya kumaliza tatizo kwa umakini na ufanisi anaongeza tatizo huyu mtu hafai,kama anataka afanye kazi kwa ufasaha zaidi basi ni lazima awe karibu sana na wizara yake pia na wafanyakazi wake ,naona kama yuko mbali sana na wizara yake hiyvo ni rahisi kuingizwa chaka.