Waziri wa Mambo ya Ndani anatakiwa kujiuzulu mara moja

Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
3,114
2,000
Nimemsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani, Mh. Mwigulu Nchemba, akitoa taarifa ya Serikali kuhusiana na "waraka" wa Serikali kujibu Waraka wa Maaskofu wa KKKT. Waziri ametumia kikao hicho na Waandishi wa Habari kujaribu kujisafisha yeye mwenyewe binafsi na pili kuisafisha Serikali juu ya kadhia hii.

Mwigulu anatuambia kwamba kwenye mitandao kuna taarifa nyingi za kugushi, kwa kutumia mbinu za kitekinolojia. sasa cha kushangaza ni kwamba hiki kinachoongelewa hapa wala hakihusiki na hawa wataalamu wa kugushi. Maana ingekuwa hivyo, ya nini kumsimamisha kazi huyo jamaa aliyesaini? "Waraka" wa serikali ni matokeo ya vikao kati ya KKKT na Wizara, na ukiangalia jibu la KKKT wanakubali kwamba wamekaa na serikali, na kwamba kulikuwa pia na mwakilishi wa Askofu Mkuu, Mkuu wa KKKT. na wameeleza mambo mengi ambayo wameyatekeleza ili kukidhi mahitaji ya Serikali. sasa inakuwaje huu "waraka" wa serikali ukawa feki? Ki mantiki, Waziri anajaribu kujikinga na jani la mwembe ili kujihifadhi utupu wake mbele ya jamii, jambo ambalo haliwezekani.

Mwigulu pia anawashambulia watu ambao "wanashabikia vitu vinavyoweza kuleta migawanyiko katika jamii yetu" kwamba "mambo ambayo yanaweza kuleta mgawanyiko katika jamii yetu" wanayashabikia na kutafuta "kiki ya kisiasa".
Hapa naamini anawalenga UKAWA ambao waliitisha mkutano wa waandishi wa habari na kuwataka Maaskofu wasijibu "waraka" wa serikali, ili "tuone serikali itafanya nini". Kauli hii ya Mwigulu inalenga "kupunguza" "ushindi" ambao UKAWA wameupata katika sekeseke hili. Maana serikali ya CCM imecheza faulo. Refa kaamuru upigwe mpira wa adhabu. Golikipa wa CCM akatoka nje ya goli. UKAWA hawakufanya ajizi wakatikisa nyavu za Serikali ya CCM. sasa upande wa CCM wanasema kwamba timu ya UKAWA wanatafuta "ushindi" wa bure kwa sababu wao walisusa!!!

Haya ni makosa ya wazi kabisa ya serikali katika uwajibikaji. na nafasi ilitolewa bungeni kwa Waziri mkuu kujibu swali la Mbatia. lakini serikali ikashindwa kuitumia na wakajiegemeza kwenye rungu la naibu spika. Hiki ni kipindi ambacho imeonekana wazi kabisa kwamba rungu la naibu spika ambaye ameletwa maalum kulinda maslahi ya serikali, kuna wakati linakuwa halina maana kabisa, na kwa kweli naibu spika hakuwapiga wapinzani, bali wapinzani wamekwepa na rungu limeipata Serikali yenyewe. Upinzani wametekeleza wajibu wao wa kikatiba ili kuweka mambo sawa, kuleta " a sense of commonsense in all this nonsense", kuleta utulivu katika bahari ya machafuko iliyosababishwa na serikali ya CCM, kuleta matumaini katika taharuki iliyosababishwa na serikali ya CCM.

Mwigulu mbali ya kugusia kwa kifupi tu kwamba amemsimamisha kazi "Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Usajili wa Jumuiya za Kidini na Vyama vya Kijamii, Merlin Komba, kupisha uchunguzi wa barua iliyoandikwa kwa maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania." anatumia muda mwingi kuwalaumu "wanaotafuta kiki za kisiasa". inavyoonekana serikali "iko vizuri" na tatizo liko kwa "wanaoshabikia vitu vinavyoweza kuleta migawanyiko katika jamii yetu" Pia anawapongeza waandishi wa habari kwa "kumpigia simu mara kwa mara kuulizia ukweli wa jambo hili" lakini ukisoma Magazeti hakuna mahali serikali imefafanua sekeseke hili. Hata kule bungeni serikali imeingia mitini. siyo waziri wa Mambo ya ndani, siyo naibu, siyo waziri mkuu, waliokuwa tayari kuongelea hili. sasa leo waziri anapoibuka na kuanza kutoa mashambulizi kwa "watu wanaotafuta kiki za kisiasa" sidhani kama kuna watakaomuelewa.

Ni dhahiri kwamba Serikali imejikanganya yenyewe. Imeruhusu bomu hilo kulipuka, na ikakaa kimya bila kufafanua lolote. baada ya kuona taharuki kubwa ya jamii, na UKAWA walipolivalia njuga, na inawezekana kuna mtu alimnong'oneza Mkuu wa kaya, ndiyo waziri anaibuk.

Hapo sana sana waziri wa mambo ya ndani ajiuzulu tu. Kumsimamisha Mkurugenzi wa kitengo ambaye amefanya kazi yake kwa niaba ya Wizara, ni kutoa kafara ambayo haina mashiko. kafara stahiki hapo ni Waziri Mwenyewe, kufuata mfano wa Ali Hassan Mwinyi, ambaye aliwahi kujiuzulu nafasi hiyo hiyo kipindi kile miaka ya 70 yalipotokea mauaji katika mikoa ya Shinyanga na Mwanza.
 
treborx

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
4,634
2,000
Hakuna sababu yoyote ya Waziri kujiuzulu. Kwa nini ajiuzulu? Hata ningekuwa mimi siwezi kujiuzulu ng'o. Kwa nini nijiuzulu au niwajibike katika mfumo ambao hakuna mtu anayewajibika wala kujali hata kama amekosea, na hata mtu huyo akienda kugombea bado huchaguliwa kwa kura nyingi na wapiga kura? You guys must be joking. Kwenye mfumo ambao watu hawajui maana ya kuwajibika, huwezi kumwambia mtu mmoja kuwajibika. Mwigulu chapa kazi mzee. Huu ni upepo. Utapita tu kama yalivyopita mengine mengi.
 
Wo shi niubi

JF-Expert Member
Aug 14, 2015
961
1,000
Kwa maneno mafupi waziri wa mambo ya ndani JIPU, unawezaje kumfukuza mtu kwa barua batili? si angesema tu hiyo ni barua batili haihusiani na serikali na tutawatafuta wote wanaosambaza barua batili, lakini ukisema ni barua batili halafu unamfukuza msajili maana yake ile barua sio batili tena, hiyo ni 100% imetoka katika wizara yake, niliwahi sema hapa katika mawaziri wasiojitambua mwiguru yumo,tulianza na kibiti wananchi walipopiga kelele ndo kwa mbali akachukua hatua, tukaja na watu wasiojulikana, tukaja polisi kupiga raia na kuua, leo kaja na kituko cha maaskofu,maelezo yake yote yanakinzana, mara technologia watu wanaweza wakarekebisha heading, nimeona nyaraka mbalimbali, barua ni batili, sasa hapo tuelewe kipi, barua imetoka serikali au haijatoka serikali? kama imetoka serikali nani kahusika kwa misingi ipi? ameitisha press conference baada ya kumaliza tatizo kwa umakini na ufanisi anaongeza tatizo huyu mtu hafai,kama anataka afanye kazi kwa ufasaha zaidi basi ni lazima awe karibu sana na wizara yake pia na wafanyakazi wake ,naona kama yuko mbali sana na wizara yake hiyvo ni rahisi kuingizwa chaka.
 
Jmc06

JF-Expert Member
May 11, 2016
1,801
2,000
Sijui mnatumiaga akili gani kutoa haya mawazo?,ajiuzuru sababu ya huu upuuzi wa waraka?,ingekuwa wewe ungejiuzuru?,tangu juzi nawaambia hizi siasa zinawaletea ujinga.Mnakomalia kila mnacholetewa bila kutumia akili, hii ishu ndo inaishia hivyo jumatatu tunaanza na series nyingine mkijakushtuka 2020 Hanna Sera yoyote zaidi ya kudandia kila linaloletwa.Sisapoti upinzani ila mngekomalia hata katiba Mpya tu mwanzo mwisho mngeonekana MNA hoja ya msingi.Ila kudandia kila linalojitokeza mtapoteza 90% ya viti bungeni 2020. Mtaani Maisha yanasonga fresh watu wanajiandaa na weekend.
 
Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
3,114
2,000
Hakuna sababu yoyote ya Waziri kujiuzulu. Kwa nini ajiuzulu? Hata ningekuwa mimi siwezi kujiuzulu ng'o. Kwa nini nijiuzulu au niwajibike katika mfumo ambao hakuna mtu anayewajibika wala kujali hata kama amekosea, na hata mtu huyo akienda kugombea bado huchaguliwa kwa kura nyingi na wapiga kura? You guys must be joking. Kwenye mfumo ambao watu hawajui maana ya kuwajibika, huwezi kumwambia mtu mmoja kuwajibika. Mwigulu chapa kazi mzee. Huu ni upepo. Utapita tu kama yalivyopita mengine mengi.
Nimekusoma vizuri mkuu. Ila tatizo la mkakati kama huo, ni wa muda mfupi, siyo wa muda mrefu. haya mambo huwa yanafumukaga, na watu wakiangalia wataona kwamba kuna mtu aliangalia mbele na kufanya kitu kwa "Maslahi ya Taifa". Mzee Mwinyi alijiuzulu lakini baadaye akaja kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huo ni mfano mmojawapo wa jinsi ya kucheza vizuri karata zako. Mwigulu bado kijana, bado anaweza kuchanga karata zake kuangalia mbele.

Ila kwa upande mwingine pengine uko sahihi, kwa sababu Mwigulu mwenyewe ana maskendo kibao. kama yale ya kuwaita CHADEMA magaidi, na hapa katikati kuna mengi yametokea kama watu kupotea, kutekwa, mauaji ya kibiti, yote yapo chini ya wizara yake. kwa hiyo inawezekana kwamba tayari keshachafuka sana anaona bora aendelee kula nguruwe aliyenona, na kama ni noma na iwe noma.
 
Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
3,114
2,000
Sijui mnatumiaga akili gani kutoa haya mawazo?,ajiuzuru sababu ya huu upuuzi wa waraka?,ingekuwa wewe ungejiuzuru?,tangu juzi nawaambia hizi siasa zinawaletea ujinga.Mnakomalia kila mnacholetewa bila kutumia akili, hii ishu ndo inaishia hivyo jumatatu tunaanza na series nyingine mkijakushtuka 2020 Hanna Sera yoyote zaidi ya kudandia kila linaloletwa.Sisapoti upinzani ila mngekomalia hata katiba Mpya tu mwanzo mwisho mngeonekana MNA hoja ya msingi.Ila kudandia kila linalojitokeza mtapoteza 90% ya viti bungeni 2020. Mtaani Maisha yanasonga fresh watu wanajiandaa na weekend.
Mkuu, hasira za mkizi furaha ya mvuvi. naona mchezo wa siasa hujaujua vizuri. Kosa moja goli moja. hakuna msahamaha hapa. hata kama hatajiuzulu, damage imetokea tayari.

Kumbuka kwamba upinzani wamekuwa wakiongeza kura zao consistently tokea uchaguzi mkuu wa 2010. Hii inatokana na kazi nzuri ya kuitwanga ngumi serikali ya CCM kila inapofanya faulo, na pia kuonesha njia mbadala. Kujieneza vijijini. Kitu ambacho kinawakwamisha upinzani ni kimoja tu: DOLA, au ukipenda, MAGOLI YA MKONO. Na ukiangalia hesabu za JPM katika chaguzi ndogo zilizopita, ni kuhakikisha mawakala wa upinzani hawaingii mapema ili watu wafanye vitu vyao. Maana yake pamoja na mbwembwe zote, JPM haamini kabisa kwamba anaweza kupenya katika sanduku la kura katika uchaguzi ulio huru na wa haki. Na kwa hali hii ya uchumi, kwa siasa hizi za kuwekeza kwenye mambo ya muda mrefu na kuwaacha hoi watu wako, ubabe huu wa kuwaumiza wafanyakazi, ambao wanawakilisha ndugu na jamaa wengi tu, kuwaumiza wavuvi katika operesheni za kikatili na zisizo na maana, kuwaumiza wafanyabiashara, wajasiriamali, bomoabomoa zisizo na akili wala huruma, sioni mahali JPM anaweza kupenya katika uchaguzi bila kutumia uporaji wa kura.

Wapinzani waendelee kuiponda serikali ambayo yenyewe pia inajiponda kila ipatapo nafasi, ili ifikie hatua hata hao wanaoagizwa kupora kura waone aibu na wananchi wafike mahali wadai watu wao walioshinda kihalali.
 
Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
3,114
2,000
Merlin Komba deserves commendation rather than condemnation.
Uko sahihi Mkuu. lakini naamini wamemhakikishia mambo yake yako salama, watampangia kazi nyingine na hata promosheni atapewa.
 
Jmc06

JF-Expert Member
May 11, 2016
1,801
2,000
Mkuu, hasira za mkizi furaha ya mvuvi. naona mchezo wa siasa hujaujua vizuri. Kosa moja goli moja. hakuna msahamaha hapa. hata kama hatajiuzulu, damage imetokea tayari.

Kumbuka kwamba upinzani wamekuwa wakiongeza kura zao consistently tokea uchaguzi mkuu wa 2010. Hii inatokana na kazi nzuri ya kuitwanga ngumi serikali ya CCM kila inapofanya faulo, na pia kuonesha njia mbadala. Kujieneza vijijini. Kitu ambacho kinawakwamisha upinzani ni kimoja tu: DOLA, au ukipenda, MAGOLI YA MKONO. Na ukiangalia hesabu za JPM katika chaguzi ndogo zilizopita, ni kuhakikisha mawakala wa upinzani hawaingii mapema ili watu wafanye vitu vyao. Maana yake pamoja na mbwembwe zote, JPM haamini kabisa kwamba anaweza kupenya katika sanduku la kura katika uchaguzi ulio huru na wa haki. Na kwa hali hii ya uchumi, kwa siasa hizi za kuwekeza kwenye mambo ya muda mrefu na kuwaacha hoi watu wako, ubabe huu wa kuwaumiza wafanyakazi, ambao wanawakilisha ndugu na jamaa wengi tu, kuwaumiza wavuvi katika operesheni za kikatili na zisizo na maana, kuwaumiza wafanyabiashara, wajasiriamali, bomoabomoa zisizo na akili wala huruma, sioni mahali JPM anaweza kupenya katika uchaguzi bila kutumia uporaji wa kura.

Wapinzani waendelee kuiponda serikali ambayo yenyewe pia inajiponda kila ipatapo nafasi, ili ifikie hatua hata hao wanaoagizwa kupora kura waone aibu na wananchi wafike mahali wadai watu wao walioshinda kihalali.
We huwajui watanzania vizuri endelea kuota, nyie mmekalia kuhesabu weakness za serikali, na wananchi wanahesabu mazuri ya serikali moyoni bila kelele Kama nyie tuone 2020 nani zaidi.Endelea kujifariji utafurahi mwenyewe 2020.
 
Masiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
6,997
2,000
Wamelikoroga ngoja walinywe sasa. Ati "Wewe Askofu". Unakaaje na mtu kujadili kitu batili.......
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom