Mindi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2008
- 3,523
- 4,991
Nimemsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani, Mh. Mwigulu Nchemba, akitoa taarifa ya Serikali kuhusiana na "waraka" wa Serikali kujibu Waraka wa Maaskofu wa KKKT. Waziri ametumia kikao hicho na Waandishi wa Habari kujaribu kujisafisha yeye mwenyewe binafsi na pili kuisafisha Serikali juu ya kadhia hii.
Mwigulu anatuambia kwamba kwenye mitandao kuna taarifa nyingi za kugushi, kwa kutumia mbinu za kitekinolojia. sasa cha kushangaza ni kwamba hiki kinachoongelewa hapa wala hakihusiki na hawa wataalamu wa kugushi. Maana ingekuwa hivyo, ya nini kumsimamisha kazi huyo jamaa aliyesaini? "Waraka" wa serikali ni matokeo ya vikao kati ya KKKT na Wizara, na ukiangalia jibu la KKKT wanakubali kwamba wamekaa na serikali, na kwamba kulikuwa pia na mwakilishi wa Askofu Mkuu, Mkuu wa KKKT. na wameeleza mambo mengi ambayo wameyatekeleza ili kukidhi mahitaji ya Serikali. sasa inakuwaje huu "waraka" wa serikali ukawa feki? Ki mantiki, Waziri anajaribu kujikinga na jani la mwembe ili kujihifadhi utupu wake mbele ya jamii, jambo ambalo haliwezekani.
Mwigulu pia anawashambulia watu ambao "wanashabikia vitu vinavyoweza kuleta migawanyiko katika jamii yetu" kwamba "mambo ambayo yanaweza kuleta mgawanyiko katika jamii yetu" wanayashabikia na kutafuta "kiki ya kisiasa".
Hapa naamini anawalenga UKAWA ambao waliitisha mkutano wa waandishi wa habari na kuwataka Maaskofu wasijibu "waraka" wa serikali, ili "tuone serikali itafanya nini". Kauli hii ya Mwigulu inalenga "kupunguza" "ushindi" ambao UKAWA wameupata katika sekeseke hili. Maana serikali ya CCM imecheza faulo. Refa kaamuru upigwe mpira wa adhabu. Golikipa wa CCM akatoka nje ya goli. UKAWA hawakufanya ajizi wakatikisa nyavu za Serikali ya CCM. sasa upande wa CCM wanasema kwamba timu ya UKAWA wanatafuta "ushindi" wa bure kwa sababu wao walisusa!!!
Haya ni makosa ya wazi kabisa ya serikali katika uwajibikaji. na nafasi ilitolewa bungeni kwa Waziri mkuu kujibu swali la Mbatia. lakini serikali ikashindwa kuitumia na wakajiegemeza kwenye rungu la naibu spika. Hiki ni kipindi ambacho imeonekana wazi kabisa kwamba rungu la naibu spika ambaye ameletwa maalum kulinda maslahi ya serikali, kuna wakati linakuwa halina maana kabisa, na kwa kweli naibu spika hakuwapiga wapinzani, bali wapinzani wamekwepa na rungu limeipata Serikali yenyewe. Upinzani wametekeleza wajibu wao wa kikatiba ili kuweka mambo sawa, kuleta " a sense of commonsense in all this nonsense", kuleta utulivu katika bahari ya machafuko iliyosababishwa na serikali ya CCM, kuleta matumaini katika taharuki iliyosababishwa na serikali ya CCM.
Mwigulu mbali ya kugusia kwa kifupi tu kwamba amemsimamisha kazi "Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Usajili wa Jumuiya za Kidini na Vyama vya Kijamii, Merlin Komba, kupisha uchunguzi wa barua iliyoandikwa kwa maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania." anatumia muda mwingi kuwalaumu "wanaotafuta kiki za kisiasa". inavyoonekana serikali "iko vizuri" na tatizo liko kwa "wanaoshabikia vitu vinavyoweza kuleta migawanyiko katika jamii yetu" Pia anawapongeza waandishi wa habari kwa "kumpigia simu mara kwa mara kuulizia ukweli wa jambo hili" lakini ukisoma Magazeti hakuna mahali serikali imefafanua sekeseke hili. Hata kule bungeni serikali imeingia mitini. siyo waziri wa Mambo ya ndani, siyo naibu, siyo waziri mkuu, waliokuwa tayari kuongelea hili. sasa leo waziri anapoibuka na kuanza kutoa mashambulizi kwa "watu wanaotafuta kiki za kisiasa" sidhani kama kuna watakaomuelewa.
Ni dhahiri kwamba Serikali imejikanganya yenyewe. Imeruhusu bomu hilo kulipuka, na ikakaa kimya bila kufafanua lolote. baada ya kuona taharuki kubwa ya jamii, na UKAWA walipolivalia njuga, na inawezekana kuna mtu alimnong'oneza Mkuu wa kaya, ndiyo waziri anaibuk.
Hapo sana sana waziri wa mambo ya ndani ajiuzulu tu. Kumsimamisha Mkurugenzi wa kitengo ambaye amefanya kazi yake kwa niaba ya Wizara, ni kutoa kafara ambayo haina mashiko. kafara stahiki hapo ni Waziri Mwenyewe, kufuata mfano wa Ali Hassan Mwinyi, ambaye aliwahi kujiuzulu nafasi hiyo hiyo kipindi kile miaka ya 70 yalipotokea mauaji katika mikoa ya Shinyanga na Mwanza.