Waziri wa Maji: Mradi umekamilika, tatizo la maji Dar limekwisha rasmi

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,968


Waziri wa maji Gaston Mwenge amesema tatizo la maji kwa jiji la Dar linakuwa ni historia baada ya mitambo ya upanuzi wa mitambo ya maji ya Ruvu juu na Ruvu chini kukamilika kwa asilimia mia.

Amesema sasa wanazalisha lita milioni 200 kwa siku kutoka lita milioni 80 kwa siku zilizokuwa zinazalishwa mwanzo.
 

Waziri wa maji Gaston Mwenge amesema tatizo la maji kwa jiji la Dar linakuwa ni historia baada ya mitambo ya upanuzi wa mitambo ya maji ya Ruvu juu na Ruvu chini kukamilika kwa asilimia mia
Amesema sasa wanazalisha lita milioni 200 kwa siku kutoka lita milioni 80 kwa siku zilizokuwa zinazalishwa mwanzo

Mbona Mbagala hakuna maji? Tell me Gaston!
 
Hiyo ni kauli ya kitakwimu yaani kisiasa zaidi ya uhalisia kwa kweli..maana neno historia limetumikaga sana kuweka historia zaidi. Kila kitu kitakuwa historia na kinabakia hivyo hivyo kama historia..ngoja tuone time will tell
 
Hiyo ni kauli ya kitakwimu yaani kisiasa zaidi ya uhalisia kwa kweli..maana neno historia limetumikaga sana kuweka historia zaidi. Kila kitu kitakuwa historia na kinabakia hivyo hivyo kama historia..ngoja tuone time will tell
Kwa hiyo huamini kama mtambo huo umekamilika kwa asilimia 100 au?
 
Mwenge kweli huyo,huku Goba hakuna Maji,sijui anaongelea Dar ipi,tuache siasa kwenye watu kuoga,watu tunaoga kwa vipimo
 
Heko lwenge naona king'ongo na bonyokwa mambo yao super!.sasa maswala ya migari kuuza maji kwishinei!
 
Kwa Dar inayokuwa kwa kasi, sidhani kama mitambo ya ruvu itatoshereza mahitaji ya maji ya jiji zima. Miundominu yenyewe ya usambazaji bado mpaka waje waikamilishe so leo
 
Huyu waziri ni mzigo,wakati wizara ikiwa chini ya Mbarawa aliwa amrisha DAWASCO wawe wamesajili wateja million moja ndani ya miezi kumi na miwili toka chini ya laki mbili wa sasa,tena kwa mkopo
Tangu aje huyu waziri juhudi zote zilizo anza zimekoma jiji zima linapasuka mabomba kwa kukosa wateja huku bei ya lita ishirini shs 500 kwa maskini na wanyonge
 
We mtoa mada huwa unaleta habari zenye tija sana, hongera. User name yako ila ngumu kuiandika ninge ku mention. Ila waziri awe mkweli kwani hayo maji ni kwa wale wenye mifumo ya dawasa au wote!? Sasa sisi huku Chanika hayo maji yatafika kwa blututhi
 
Nakumbuka simbachawene mwaka jana alisema tatizo LA umeme limekwisha kutokana na kukamilika kwa mitambo ya umeme kule kinyerezi baada ya hapo ndo ulitokea mgao afadhal ya mwanzo ni swala LA muda tu
 
Back
Top Bottom