Nipe Maji
JF-Expert Member
- Mar 25, 2025
- 335
- 190
Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, ameagiza Miradi yote Mikubwa na ya Kati ya madini ambayo tayari imekwishapewa leseni kuanza utekelezaji wake mara moja ili kuchochea ukuaji wa sekta na kuleta manufaa kwa taifa kwa ujumla na kutimiza azma ya Serikali kutoa leseni hizo.
Mavunde ametoa maagizo hayo leo tarehe 28 Machi, 2025 Jijini Dodoma wakati akizungumza katika Kikao maalum na Chemba ya Migodi Tanzania (TCM) kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Sekta hiyo ili kuboresha uendelezaji na usimamizi wa shughuli za uchimbaji na biashara ya madini kwa manufaa ya sekta na taifa kwa ujumla, ikiwa ni sehemu ya ratiba yake ya kukutana na makundi yote yayojihusisha na mnyororo mzima wa Sekta ya Madini nchini.
Waziri Mavunde amesema Serikali inataka kuhakikisha kuwa Miradi yote ya Uchimbaji Madini iliyopangwa kuanza inaanza mara moja bila kucheleweshwa, na kuwa Serikali kwa upande wake imejitahidi kurahisisha taratibu kwa wawekezaji na sasa ni wakati wa Sekta binafsi kuchukua hatua kwa upande wao.
“Serikali imefanya kazi yake, tumeondoa vikwazo vingi na kurahisisha utaratibu. Sasa ni jukumu la wawekezaji kuhakikisha kuwa miradi inaanza kutekelezwa mara moja” amesema Waziri Mavunde.