Waziri wa Katiba na Sheria: Mahakimu wenye elimu ya astashahada na stashahada kufutwa kazi

Waziri wa Katiba na Sheria Mh.Dkt Harrison Mwakyembe amesema serikali itawafuta kazi Mahakimu wote wa mahakama za mwanzo wenye elimu ya cheti na diploma ya sheria.

“Tunahitaji mahakimu wenye uwezo wa sheria ambao wamehitimu shahada ya kwanza, hivyo serikali inaandaa utaratibu wa kuwafuta kazi mahakimu wote wenye elimu ya cheti na diploma”
Kwani waliajiriwa na nani hao wa astashahada na shahada?
 
Wizara ya katiba na sheria chini ya Waziri mwakyembe imeanza kupunguza wafanyakazi kazi wake imewafukuza kazi waajiriwa 385 walioajiriwa mwezi June 2016 walifanya kazi mwezi mmoja na kusainishwa mikataba yote ya kazi baada ya hapo walisimamishwa kazi kwa kisingizio cha uhakiki wa watumishi hewa baada ya kuishi uhakiki huo hawakurudishwa kazini walipofatilia waliambiwa kuwa wamefukuzwa kazi hayo yalitolewa na tume ya utumishi wa mahakama mpaka sasa wana miezi sita toka wafukuzwe kazi wapo nyumbani pia wizara ya katiba na sheria itawafukuza kazi mahakimu wote ambao wana diploma na cheti ndani ya mwaka huu.

Source. EATV
 
Hii ni kazi kwakweli. Kila sehemu matamko yaongoza taifa, kunamaana gani ya kuwa na kanuni na taratibu. Kwa hizi taratibu sasa hata sheria za nchi hazina kazi tena, haswa haki ya kikatiba ya mwananchi wa kitanzania ipo ukingoni kupotea. Hii hali sio nzuri kwa Tanzania sasa.
 
Unajua hii kauli ya hawa viongozi ya kusema kuwa ''watatoa'' ajira inabidi tuwe tunaitafakari sana .

Maana hili neno linamaana kupunguza wala sio kuongeza sasa kwa sababu ya mahaba niue na chama kipindi wakisema watatoa ajira watu huwa wanashangilia sana bila kujiuliza kutoa ajira kuna maana gani...

Ila wacha tuisome namba kwa sababu tumeipenda wenyewe na tumeichagua wenyewe angalau mimi sikuwapigia kura yangu hawa jamaa.

Sasa hao watu waliofanya kazi kwa kipindi chote hicho na certificate / Diploma zao wataenda wapi wakati hata pesa zao za fao la kujitoa mmezizuia mpaka watakapokuwa wazee .

Viongozi wa nchi hebu kuweni na huruma na wananchi wenu hizi adhabu mnazowapa wakija kulipiza kwenye sanduku la kura mnatuma Chaje aje afute matokeo na virungu wanapigwa.

Haki ya hii nchi itachelewa sana kupatiakana nahisi vituku vyetu ndio vitakavyoweza kuipata.

Hii nchi ni kisiwa cha uvumilivu ila amani hakuna sio siri.
 
"lazima tufanye kila juhudi hawa Watanzania maskini wapate ajira"---Juma Punda Mtumbuaji
 
Hizi taarifa si sahihi. Watu wanaleta habari ili wapewe habari. Chaka la chanzo ni EATV
 
Katika kikao kijacho cha Bunge, Serikali inakusudia kupeleka bungeni na kusoma kwa mara ya kwanza Muswada wa Sheria ya msaada wa Kisheria (The Legal Aid Bill), ambao pamoja na mambo mengine utaruhusu watu wasio na taaluma ya sheria lakini wenye uzoefu na masuala ya kisheria (Paralegals) kutoa msaada wa kisheria, kwa mujibu wa kifungu cha Kifungu 10(1)d(ii) na (iii).

Maana yake ni kwamba ikiwa muswada huu utapita na kuwa sheria, it means wale watu wasio na taaluma ya sheria lakini wanajishughulisha kwa namna moja au nyingine na mambo ya kisheria (mnawaita Bush Lawyers) watatambulika rasmi na watapewa fursa ya kutoa msaada wa kisheria katika baadhi ya masuala ya kijamii.

Nini maoni yako??
 
Kuna watu walidisco enzi zilee na wanaifahamu sheria na wajanja wajanja sijui hawa nao ni bush lawyers?
 
Back
Top Bottom