Waziri wa fedha: Serikali haitarudi nyuma matumizi ya mashine za EFD

potokaz

JF-Expert Member
Jul 19, 2011
530
486
Leo 22/02/2014 Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya amesema kuwa Serikli haitarudi nyuma kwenye matumizi ya mashine za kielectroniki, EFD. Aliyasema hayo katika mahafali ya chuo cha TRA.

Waziri amesema wafanyaabiasha waache visingizio vinavyotokkana na wao kutokuelewa vizuri juu ya mashine hizo, pia amesisitiza kuwa sisi walaji tunaponunua biadhaa tudai risiti.

WATANZANIA inabidi tuelewe kwamba HATUWEZI kuendelea bila kuwa na mifumo dhabiti ya KODI!

TUJIULIZE,

Hivi kweli mfumo wa kulipishana kodi kwa kukadiriwa kwa kutumia busara na utaalamu wa mkadiriaji wa TRA uko sahihi au umepitwa na wakati?. Nadhani umepitwa na wakati na kuchochea kushamiri kwa vitendo vya rushwa.
Hivi endapo mfanyabiashara ananunua kwa gharama yake na anarejeshewa pesa yake kuipitia malipo yake ya kodi, si ni kama amepewa bure?, mathematically ni sawa na kusema umetoa nne ukapata nne mwisho wa siku unakuwa umetoa sifuri.

Hivi ELIMU ndugu zetu wa TRA si wamejitahidi kuitoa ya kutosha?. Katika baadhi ya mikutano ambayo TRA wamekuwa wakiifanya na wafanyabiashara, mahudhurio ya wafanyabiashara yamekuwa ni hafifu sana kiasi cha kusikitisha, je hapo TRA watalaumiwa hawajatoa elimu ya kutosha?, je lawama hii inawatendea haki TRA?, au wangewafuata kwenye biashara zenu kuwapa elimu huko?

Matengezo ya mashine, je si ilishafahaishwa na TRA kwamza matengenezo ya mashine ni BURE walau kwa mwaka wa kwanza wa matumizi ya mashine?, na baada ya mwaka wa kwanza kupita gharama ya matengezo ya mashine endapo itaharibika italipwa na mfanyabiashara na katika kipindi ambacho mfanyabiashara analipia kodi atarejeshewa kiasi alichotengeneza mashine ile kwani kimsingi mashine hizo ni za TRA.

UONGO UNAOENEZWA, kuna wanaoeneza uongo kuwa mashine hizi zinakata asilimia 18, hiyo siyo kweli. HAZIKATI KIASI CHOCHOTE. Kimsingi ni kuwa badala ya kutumia VITABU sasa tunkwenda kidigitali unabofya na risiti inatoka. Tafuteni majedwali ya KODI kwenye ofisi za TRA. Kwa kuwasaidia tu wanaotaka kujua.

Mfanyabiashara akiuza chini ya shilingi 0 na shilingi milioni 4 hakatwi KODI. Huyu anahitaji kukua kwa kutumia senti zake zote kujikuza kibiashara.

Kati ya shilingi 4Million na 7.5Million kodi ni shilingi 100,000/= kwa mwaka.

Kati ya shilingi 7.5Million na 11.5Million kodi ni shilingi 212,000/= kwa mwaka.

Kati ya shilingi 11.5Million na 16Million kodi ni shilling 364,000/= kwa mwaka.

Kati ya shiling 16Million na 20Million kodi ni shilling 575,000/= kwa mwaka.

Kiasi kinachozidi 20M, hairuhusiwi kukadiriwa ila mfanyabiashara atatakiwa na sheria aandae audited accounts, hapa mfanyabiashara atatozwa kodi kulingana faida aliyoipata, namna hii kitu inavyofanyakazi wasiliana na hii namba ya bure ya TRA 0713800333 au wasiliana na ofisi y TRA iliyo karibu nawe.

Kama tuliweza kuhama ANALOGIA na kuingia DIGITALI tunashindwaje KUHAMA kutoka kwenye kwenye VITABU na kuhamia kwenye EFD machine kwa ajili ya kutolea risiti?

WAFANYABIASHARA TUACHE UJANJA UJANJA, TULIPE KODI!
 
Hakuna mfanyabiashara asiye penda kutumia EFD, ugomvi uko kwenye bei ya kuinunua hiyo EFD kwa bei itakayo ua mtaji wangu. Kama huyo Mkuya ana nia njema na sisi wafanyabishara wa tz. kwa nini anagwaya kushughulika kuondoa ufisadi ulioingizwa kwenye bei za EFD, ambayo kiuhalisia bei yake si sahihi na ni ya kutukomoa wafanyabiashara?
 
Mnalipwa bei gani kwa kushiriki kukandamiza wananchi na kuleta mawazo mfu humu jf?

Mkuu ni kweli unathubutu kusema haya ni mawazo mfu. Nina wasiwasi na uelewa wako na uzalendo wako, tutawezaje kuendelea pasipo kuwa na mifumo thabiti ya kulipa kodi?
Ni uzalendo wa kutaka kuona taifa letu linapiga hatua na kupunguza utegemezi wa mataifa ya nje unaotuletea ukoloni wa kinamna flani hata leo.
 
Hakuna mfanyabiashara asiye penda kutumia EFD, ugomvi uko kwenye bei ya kuinunua hiyo EFD kwa bei itakayo ua mtaji wangu. Kama huyo Mkuya ana nia njema na sisi wafanyabishara wa tz. kwa nini anagwaya kushughulika kuondoa ufisadi ulioingizwa kwenye bei za EFD, ambayo kiuhalisia bei yake si sahihi na ni ya kutukomoa wafanyabiashara?
Mkuu bei ilianza laki 8, sasa bei zimeshuka hadi laki 6 hadi laki 7 kulingana na aina ya mashine. Tatizo sio bei, ni kodi ndio inakwepwa na wafanyabiashara. Halafu wasambazaji/ suppliers wa mashine hizi wanakwambia kuwa uanlipia ndani ya miezi 2 ukifikisha nusu ya gharama wanakuletea mashine hiyo sehemu yako ya biashara na kukufundisha.
 
Hakuna Mfanyabiashara anaependa kulipa Kodi, hiyo ipo Dunia Nzima na ndio maana zinawekwa kila sheria ili kuwadhibiti nao wanatumia kila Fursa ( Tax Evasion na Tax Avoidance kuikwepa) usihadaike na maneno yao.
 
Mkuu bei ilianza laki 8, sasa bei zimeshuka hadi laki 6 hadi laki 7 kulingana na aina ya mashine. Tatizo sio bei, ni kodi ndio inakwepwa na wafanyabiashara. Halafu wasambazaji/ suppliers wa mashine hizi wanakwambia kuwa uanlipia ndani ya miezi 2 ukifikisha nusu ya gharama wanakuletea mashine hiyo sehemu yako ya biashara na kukufundisha.

Mbali ya bei, nilisikia malalamiko mengine ya wafanyabiashara:
1. Wanalalamika kwa nini wauziwe kifaa kinachomsaidia TRA kufanya kazi yake. Kwamba kwa nini wasifungie bure kama Coca anavyogawa friji bure kwa wauzaji wake.
2. Wanalalamika kuwa mashine hizo zimeungwa na server ya TRA. Mtumiaji anapoandika receipt, mashine hai-print hadi server ipokee na iki-confirm ndo receipt inakuwa printed.....kwamba mara nyingi hili limekuwa tatizo la mtandao kuwa down na kumfanya msubiria risti kusubiri kwa pengine zaidi ya nusu saa kwa risti kuprinti. Wanahoji kwa mwendo huo customer care watai-meet vipi.
Hebu mnidadavulie katika angle hii kwani malalamiko mengine ya wafanya biashara naona ni mkakati wa kuendelea kukwepa kulipa kodi. Mwongozo please!
 
Kama hizi mashine baadaye zitakuwa Mali ya TRA baada ya mteja kurudishiwa kwa njia ya kodi, kwanini hivi sasa wasilipe kwa awamu! Kama kodi ya kawaida inaweza kulipwa kwa awamu, kwanini mashine isiwe hivyo!
 
Mbali ya bei, nilisikia malalamiko mengine ya wafanyabiashara:
1. Wanalalamika kwa nini wauziwe kifaa kinachomsaidia TRA kufanya kazi yake. Kwamba kwa nini wasifungie bure kama Coca anavyogawa friji bure kwa wauzaji wake.
2. Wanalalamika kuwa mashine hizo zimeungwa na server ya TRA. Mtumiaji anapoandika receipt, mashine hai-print hadi server ipokee na iki-confirm ndo receipt inakuwa printed.....kwamba mara nyingi hili limekuwa tatizo la mtandao kuwa down na kumfanya msubiria risti kusubiri kwa pengine zaidi ya nusu saa kwa risti kuprinti. Wanahoji kwa mwendo huo customer care watai-meet vipi.
Hebu mnidadavulie katika angle hii kwani malalamiko mengine ya wafanya biashara naona ni mkakati wa kuendelea kukwepa kulipa kodi. Mwongozo please!

Mkuu, nianze na (1) hapo juu, ni kwamba kabla ya kuanza implentation ya hii kitu TA walifanya reseach kidogo kwa nchi nyingine kuona walipitia njia gani, wengi walitumia mfumo huu kwamba mfanyabiashara anunue mshine kisha arejeshewe pesa yake kupitia kodi anayolipa. Unanunua kwanza ili uithamini kama mali yako halafu unarudishiwa hela. Ni kifaa cha TRA ndiyo ndio maana ikiharibika gharaa za matengenezo ni za kodi (TRA)
Hapo (2), Mkuu kuna kitu kinaitwa Z report, hii ndio hutakiwa kutumwa kila siku kabla ya kuanza biashara au kila siku wakati wa kufunga biashara na utumaji wake unatumia mtandao. Hii ni summary ya gharama ya mauzo yaliyofanyika ndani ya 24hrs, wakati inapotumwa TRA ndipo server ya TRA inapowasiliana na mashine. Baada ya kutuma hii risiti zitaendelea kutoka hata kama hakuna mtandao. Swala la kusubiri nusu saa sio kweli.
 
Back
Top Bottom