Waziri wa Biashara na Viwanda, Godfey Mwambe apiga marufuku taasisi zilizo chini ya Wizara yake kufunga biashara za watu kwa kisingizio chochote

Baada ya miezi 3 litakuja kutolewa tamko kama hili hili tena.

Sisi kazi yetu ni kutoa pongezi tu.

Hakuna kitakachobadilika, haya matamko hayajaanza leo.
 
Tangazo la Waziri limekuja wakati muafaka na nilikuwa nafikiri kuna haja maamuzi kama haya yahamie TAMISEMI ili halmashauri za miji,manispaa na jiji zijifunze kuwa KUBOMOA ENEO LA BIASHARA ya mtu kwa sababu yoyote ile hata kama amevunja sheria inaleta athari zifuatazo
1.Kukosa au kupunguza ajira kwa watanzania baada ya kubomoa biashara aliyoanzisha
2.Kuongeza uhalifu katika jamii baada ya kukosa kazi halali aliyoanzisha
3.Kuongeza umasikini katika jamii hasa baada ya mhusika kukosa pesa ya kurudisha
4.Kuongeza magonjwa mfano ugonjwa wa moyo na shinikizo la damu kutokana na kuwaza baishara iliyoanguka
5.Kuikosesha kodi halali Serikali kwa biashara husika baada ya kusimama kwa biashara yake
Mambo haya maafisa wa Halmahsuri walitakiwa kuyatazama kwa jicho pana badala ya kukimbilia kubomoa biashara husika wakati kulikuwa kuna uwezekano wa
1.Kukaa na kujadiliana nini kifanyike nini ili kutatua tatizo wakati biashara inaendelea
 
Hizi ni siasa tu kama zilivyo zingine. Wao walifikiri baada ya kupora uchaguzi wangelalia vitanda vyenye maua ya waridi sasa wanajikuta kitanda kimejaa miba.

Kila uchao bei za vitu inapanda na mfumuko unapanda mbele ya macho ya serikali na hawana cha kufanya na kisingizio pia hawana maanake wapinzani waliyokuwa wakiwatumia kama "Scapegoat" hawapo.
 

Kichekesho unakuta ameandika huna leseni funga !!!! si waonane na mhusika tu waongee kuwa baada ya miezi miwili tutapita tena uwe umeshatafuta leseni wanampa na tarehe ya kuja na kumtia moyo kuwa hatutapita kukuliza tena hata ukiona tunakuja usifunge usidhani tunakuja kwako.Tunakupa miezi miwili utaratibu wa keseni ni huu hata ikibidi watembee na fomu kabisa wampe wamwelekeze kujaza na viambatanishi vinavyotakiwa .Kama anavyo vyote ajaze hapo hapo wampe na control number alipe hapo hapo kama anazo kwa mobile money au akaunti kama akimaliza vyote kujaza waondoke na fomu zake wamwambie tutakuletea leseni hapahapa dukani endelea na biashara yako Hiyo ndio friendly approach inatakiwa

Lakini jitu linakwambia funga huna leseni hata ukiliambia nipe fomu basi ya kuomba leseni nijaze sasa hivi halina hata fomu limekaa kigaidi gaidi tu na mirangi ya kuandika funga na mikufuli!!! huna TIN ohh huna kibali ohhh hujalipa kodi ohhh leseni huna nk funga!!!!

Mtu leseni hana advice him or her give him or her time without asking him or her to close business
[/QUOTE]
Na biashara hizi zinaanzishwa kwa kusukumwa na changamoto za kimaisha, hazianzishwi na mitaji rasimi. hivyo haitakiwi asumbuliwe bali aelekezwe namna ya kurasimisha biashara yake
 
Kiwanda au biashara kufungwa kwasababu ambazo zinajadilika maana yake, mamlaka inayosimamia imeshindwa kazi.
uko sahihi asilimia 100 mimi nimekutana na wawekezaji wanajua wakija na Mitaji wakienda Tanzania Investment centre wamemaliza kila kitu to their shock wanakutana na mamlaka zingine zinapiga yowe funga sijui kibali chetu huna nk na wanachotaka afunge tu hawataki majadiliano

Kifupi wizara zote zifanye kazi kama timu moja sio ohhh ya biashara iba yae ya mazingira ina yake ya fedha ina yake sijui utumishi ina yake mtu mfano kaomba leseni ya biashara au kiwanda aelezwe kila kitu at any point awe kapitia popote

Sio anapewa leseni mfano ya bendi halafu anaajiri watoto kuimba under 18 wasio na ajira waliomalizadarasa la saba halafu ustawi wa jamii wanakuja kufunga bendi kuwa hutakiwi kuajiri watoto under 18!!! Sio fair .Wanatakuwa wafanye majadiliano taratibu sababu mwenye bendi ajui chochote akipewa leseni anajua kamaliza kufunga ni uonevu
 
Political Bongo Movie..Series 5 episode9.
Kila waziri kwa miaka 6 iliyopita ametoa tamko hilo hilo!
Hili halina uspesheli wowote! Watafunga na hawatawajibishwa kwa kufunga.
Serikali ni makaratasi, atoe tangazo rasmi, atoe waraka! Siyo kubwabwaja jukwaani.

Everyday is Saturday...............................
 
Waziri Ndugulile pia atoe tamko hilo. Taasisi yoyote iliyo chini ya Wizara yake ikiwamo TCRA isifunge biashara za watu kwa sababuyoyote ile.
Wanakera, mfanyabiashara kapanga wanakuja na rangi kuchafua ukuta.maandishi makubwaaa

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Matamko ya majukwaani, kwenye televisheni na redio hayatasaidia!! Hao wanaofunga wanafanya hivo kwa sababu SHERIA zinawarusu na ndio waliopewa MAMLAKA hayo!!

Bila kubadilishwa kwa sheria na mamlaka mambo haya yataendelea kutokea!!

Tubadilishe sheria na taratibu zetu za miaka ya 70 ili kuendana na hali ya sasa!! Mahitaji ndio husababisha kuletwa masuluhisho!! Je mahitaji ya sasa yanaendana na sheria na taratibu zilizopo????!!!
 
Ila U-turn uliyopiga kwenye uzi huu nina mashaka kama ni wewe kweli au kuna jambo limetokea..!!! Maana sijakuzoea kuandika uhalisia bali mara nyingi upenzi wa chama
 
Kwani yalipokuwa hayafungwi, hakukuwa na hizo sheria unazozitaja!? Binafsi naona ni mkumbo tu wa zamu hii... kila mmoja anaimba sauti aliyopangiwa kuimba... kama ya kwanza, Haha... ya pili sawa, ya tatu twende, ya nne, ndiyo yenyewe... DAUTI SAFI SAUTI KUBWA... Philip's, ndiyo yenyewe....!!!!!
 
Tatizo sielewi kama ni ushamba au kitu utamaduni, maana watumishi wa serikali wa idara zote, wanapoenda kukagua au kutembelea shughuli yoyote ya mtu, hawaendi kama walezi wa raia, wanaenda kama vile polisi wanavamia nyumba ya jambazi. Wanapenda kuonyesha mamlaka na nguvu waliyonayo kwa muhusika.
 
Tatizo la mawaziri na watendaji wa serikali huwa mnabadilika kama kinyonga. Huyu Mwambe school mate wangu alikuwa aliharibu sana pale TIC na alikuwa ana misimamo mibovu na anajua alivyokuwa akiumiza wawekezaji, leo anatuambia kuwa watu wasiumizwe. Jamani basi muwe na msimamo moja. Kwanini mnabadilika kama vinyonga?
 
Uko sahihi hawaendi kirafiki wanaenda kipolisi
 
Uko sahihi hawaendi kirafiki wanaenda kipolisi
Tuacheni tu tumeshazoea kuumia, muda ukifika atakuja kiongozi anayejali watu wake tutarudi kwenye hali ya kawaida. Tumemwachia Mungu, Wafanyabiashara tunaishi kama wahalifu tukitarajia ipo siku haya yatakwisha. Utawala huu siyo Taxpayer friendly, kwa hiyo acha tuzugezuge muda upite.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…