Waziri wa Ardhi na watu wako isaidieni Kwala dry port na vijiji vyake

utukufu mwanjisi

JF-Expert Member
Aug 19, 2017
2,830
2,417
Majuzi nilibahatika kutembelea Kwala kule ilipotengenezwa bandari kavu na kukuta baadhi ya shughuli ndogo ndogo zikiendelea.

Sasa kwa sababu nimekuwa ni mtu wa kupenda kujua vitu na kufanya research ndogo ndogo, nikagundua kitu kidogo ambacho kinatakiwa kufanyiwa kazi mapema ni sekta ya ardhi.

Ni hivi kule mji unaenda kuwa mkubwa sana na unaweza kuja kukusanya watumishi wengi sana wa sekta mbalimbali, vilevile ni mji ambao itakuja kuwa na vitu vingi vya kijamii na utakuwa unawaleta wageni wengi sana.

Sasa mji unahitajika upangwe kuanzia sasa kwa nguvu zote, kuanzia Morogoro Road mpaka kwenye vijiji vyote vinavyoizunguka kwala kuepusha kuja kuharibu mji kama ilivyotokea Goba maana leo huwezi tofautisha goba na Mwananyamala au Tandale tu sababu ya uzembe wa watumishi wa wakati ule.

Kapimeni zile sehemu ziwekeeni strategy nzuri za hapo baadae ili tuwe na sehem ya bandari ya kuvutia hata kwa wageni watakaokuja kufuata mzigo yao na huduma zingine.

Asante.
 
Wazo zuri, kufanya mipango mapema ni vizuri zaidi, hasa serikali za mitaa ambao ndo wapo SITE, wajitahidi kupangana vizuri na kuitaarifu serikali kuu juu ya mahitaji ON THE GROUND.
 
wazo zuri, kufanya mipango mapema ni vizuri zaidi.... hasa serikali za mitaa ambao ndo wapo SITE, wajitahidi kupangana vizuri na kuitaarifu serikali kuu juu ya mahitaji ON THE GROUND........
Serikali za mitaa zisipopelekewa wataalamu toka serikali kuu wataharibu tu maana ikipelekwa hela watauza hovyo bila upimaji
 
Back
Top Bottom