Waziri wa Afya, Dkt. Gwajima aagiza tathmini kufanyika katika miradi ya Sekta ya Afya

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na watoto, Dk Doroth Gwajima ameagiza Wakala wa Majengo Nchini (TBA) kushirikiana na Ofi si za waganga wakuu wa mikoa kufanya tathmini ya miradi yote kwenye sekta ya afya na kumpelekea taarifa ili kudhibiti ubadhirifu wa fedha za miradi.

Dk Gwajima alisema hayo alipotembelea hospitali mpya ya rufaa ya Mkoa wa Geita wakati akiwa ziarani mkoani hapa kukagua maendeleo ya huduma za afya pamoja na ujenzi wa miradi mbalimbali kwenye sekta ya afya.

Alisema kwa tathimini fupi aliyoifanya tangu ateuliwe kuwa waziri amebaini bado kuna changamoto kwenye usimamizi wa fedha za miradi ya sekta ya afya kutokana na miradi mingi kutumia kiwango kikubwa cha pesa nje ya bajeti iliyopangwa.

Dk Gwajima alitolea mfano Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Geita ambayo rais John Magufuli alitoa takribani Sh bilioni tano lakini hadi sasa mradi haujakamilika kwa asilimia 100 na bado kuna ongezeko la Sh bilioni mbili linahitajika.

“Kuna haja ya kufanya tathmini kwenye kusimamia miradi na kujipanga kushirikisha wataalamu ili fedha zetu tujue zinatumikaje, kama zinaongezeka tujue inaongezeka kiasi gani, siyo tumepanga bajeti halafu kabla mradi haujakamilika kunakuwa na ongezeko la karibia asilimia 50 ya bajeti ya awali.

“Pengine tunawapa majukumu watu ambao hawana weledi, au wanafanya makusudi na kutufanya tushindwe kufikia malengo kila siku, inatakiwa tathimini ifanyike, taarifa iandaliwe na haki itendeke na kama kuna vitu haviko sawa hatu za kisheria zichukuliwe,” alisema.

Pia alitoa mwezi mmoja kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita kuhahakisha ujenzi wa jengo la kuhifadhia watoto waliozaliwa kabla ya muda linakamilika kwa wakati ili kuondoa msongamano wa watoto kulala zaidi ya mmoja kwenye kitanda kimoja.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita, DK Japhert Simeo aliahidi kupokea maagizo ikiwemo kusimamia jengo la kutunza watoto na kufafanua kuwa jengo hilo halikukamilika kwa wakati kutokana na ujenzi kusimama baada ya kukosa Sh milioni tano ambazo tayari wameshaandikia dokezo kwa katibu tawala wa halmashauri ya wilaya.

Mdhibiti Ubora wa Majengo kutoka TBA Mkoa wa Geita, Glory Akyoo alisema ongezeko la gharama za ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita zimetokana na ushauri walioupata kutoka kwa wataalamu wa Wizara ya Afya na kuahidi kufanyia kazi maagizo ya waziri
 
Huyu naye anajifanya "katili" kama boss wake aonekane mbele yake kuwa anafanya kazi! Mwambieni naye atapita kama walivyopita wengie na ukatili wao!
 
Back
Top Bottom