Waziri Ummy Mwalimu atoa maagizo mazito kwa Halmashauri 8 zenye hati chafu na zisizoridhisha kwenye ripoti ya CAG

Madam Ummy apitie huu uzi atajifunza mengi. Wahasibu na wakaguzi hawana nguvu kuzuia upigaji, wakionewa huruma baadhi ya mambo wanapewa mgao kiasi. Wale ni makarani wenye nguvu wakuu idara na mkurugenzi.
Na mkurugenzi akikuona muhasibu ni kikwazo anakutoa halmashauri anakupeleka shuleni huko ukawe muhasibu wa sekondari/ shule ya msingi ushike hela za chaki za shule
 
Tunahitaji kuangalia namna nzuri ya kupata viongozi bora, tuna viongozi wengi sana hawakuandaliwa kuwa viongozi bali ni bahati tu na ujanja ujanja tu..

Tunahitaji watu serious kwenye mifumo...sio hizi blah blah, Nyerere aliandaa watu angalau tukawa na descipline kwenye utendaji pamoja na matatizo yote...hizi kazi zinazopatikana kwa connection ni hatari sana kwa ustawi wa Taifa..
Umenena vema kiongozi, teuzi nyingi za Wakurugenzi zinaangalia zaidi kufahamiana
 
Kwa mara ya kwanza Ummy anaibuka kuwa kilaza kwenye uwaziri.
Kaona wasio na nguvu kisiasa ni wahasibu kwahiyo anataka kuwaonea, hajaona DED wala wakuu wa Idara?
Siasa za kiafrika hovyo sana, mtu anajua ukweli lakini hataki kuufata
umemwelewa Ummy vizuri? anazungumzia uzembe wa ukaguzi wa hesabu huo unafanyika na DED?
 
Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ummy Mwalimu ameagiza Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Mamlaka za kinidhamu kuwachukulia hatua wakuu wa vitengo vya ukaguzi wa ndani wa halmashauri 54

Waziri Ummy amesema wakuu hao hawakukagua hesabu za mwisho kabla ya kuziwasilisha kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) ambapo amesema wakaguzi wa ndani kutokagua Hesabu ni ukikwaji wa kanuni za fedha za mamlaka za serikali za mitaa

Katika hatua nyingine ametaka wataalamu wenye CPA walioko kwenye Halmashuri zenye hati mbaya na hati zenye shaka wabainishwe na wafikishwe katika bodi ya wakaguzi (NBAA) ili wachukuliwe hatua stahiki

Ummy Mwalimu ameyazungumza hayo Aprili 9, 2021 jijini Dodoma alipokuwa anazungumza kuhusu ripoti ya CAG kwa Wizara ya Ofisi ya Rais TAMISEMI
Binafsi sikuona kwa nini aliitisha Press Conference,this is trying to create cheap popularity.Ambacho angefanya ni kuitisha mkutano na people who matter kwenye Halimashari akatoa maelekezo.

Furthermore,ufisadi ni mfumo wa Halishauri zetu,so what she is doing ni too cosmetic.Kuwaona wahasibu tu kwamba ndio wenye makosa is wrong.Almost everybody kwenye Halimashauri ni fisadi.

Suluhisho la kudumu ni kuzifuta.Mwalimu Nyerere alipata shida hii hii tunayopata leo na Halimashauri na hatimaye akaamua kuzifuta 1972,only to be instituted again in 1982.As far as I am concerned it was a mistake.

Nashauri tuwe na Mkuu wa Wilaya,District Administrative Secretary/Officer na vitengo mbali mbali,Kilimo nk na mfumo huu uwe moja kwa moja chini ya serikali kuu.Hii itakuwa rahisi ku-monitor,administer na kuwajibisha if necessary.Hii loose connection ya Mkuu wa Wilaya na Halimashauri inamfanya Mkuu wa Wilaya awe na uwezo mdogo sana wa kuwawajibisha, ku-manage na ku-monitor viongozi wa Halimanjauri.Sasa kama Mkuu wa Wilaya ana such a loose connection,je Mkuu wa Mkoa?To me call ya Ummi kuwataka wakuu wa Mikoa kwa mfumo wa sasa kusimamia Halimashari ni wishfull thinking,it is simply impossible.The system is the problem.Halimashauri ndizo kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya Watanzania,so unless tatizo la ufisadi linapatiwa ufumbuzi,maendeleo kwa Watanzania yatakuwa a far fetched dream.
 
Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ummy Mwalimu ameagiza Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Mamlaka za kinidhamu kuwachukulia hatua wakuu wa vitengo vya ukaguzi wa ndani wa halmashauri 54

Waziri Ummy amesema wakuu hao hawakukagua hesabu za mwisho kabla ya kuziwasilisha kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) ambapo amesema wakaguzi wa ndani kutokagua Hesabu ni ukikwaji wa kanuni za fedha za mamlaka za serikali za mitaa

Katika hatua nyingine ametaka wataalamu wenye CPA walioko kwenye Halmashuri zenye hati mbaya na hati zenye shaka wabainishwe na wafikishwe katika bodi ya wakaguzi (NBAA) ili wachukuliwe hatua stahiki

Ummy Mwalimu ameyazungumza hayo Aprili 9, 2021 jijini Dodoma alipokuwa anazungumza kuhusu ripoti ya CAG kwa Wizara ya Ofisi ya Rais TAMISEMI
Na mawakili wa serikali wanaoshindwa kesi kila siku nini hatima yao?
 
umemwelewa Ummy vizuri? anazungumzia uzembe wa ukaguzi wa hesabu huo unafanyika na DED?

Wewe ukimkagua boss wako anayekupa mkate wa kila siku na ambae anaweza kukuvurugia maisha yako ndani ya dakika 1 tu unaweza kutoa report ya aina gani khs yeye?
 
Huyu naye ...bado yuko kwenye kubwekabweka na kukurupuka kwa enzi za Jiwe!
1618043136662.png
 
Mkaguzi wa ndani anaweza akafanya kazi vzur ila sasa DED anamwambia badirisha hapo.

Atafanya nn sasa.

Wanakuwa na taarifa mbili moja kwa DED ingine anakaa nayo yeye.

Yakitokea ya kutokea ndo ataitoa huko mbele ya safari

Wamekula kiapo hao

umemwelewa Ummy vizuri? anazungumzia uzembe wa ukaguzi wa hesabu huo unafanyika na DED?
Kwa mawazo yako mkaguzi wa ndani akikagua vizuri unafikiri hela zilizopigwa zitarudi?
Kwanza mkaguzi wa ndani anakagua matumizi yaliyofanyika kwahiyo hata kama kuna madudu hawezi kuyasawazisha
 
Kwa mawazo yako mkaguzi wa ndani akikagua vizuri unafikiri hela zilizopigwa zitarudi?
Kwanza mkaguzi wa ndani anakagua matumizi yaliyofanyika kwahiyo hata kama kuna madudu hawezi kuyasawazisha
amekagua?
 
Haya ndio madhara ya kumpa mtu cheo ambacho hana taaluma nacho.

Kazi ya mkaguz wa ndan ama mkaguzi wa nje, yaani akishakuwa tu ni mkaguzi, ieleweke kuwa hana authority au mamlaka yoyote juu ya jambo flani, yeye ni mkaguzi tu.

Kama vile unavyoona CAG hawez kumfukuza kaz mfanyakaz yoyote yule wa umma, ama kama vile ambavyo hawezi kulazimisha shirika flan ama taasisi flani ifanye matumiz flani, ndivyo ambavyo mkaguz wa ndani alivyo.

Ukaguzi sio cheo chenye mamlaka ndan ya Ofisi, yaani kusema kwamba mkaguzi ataniwajibisha au kitu flan hakiwezi kwenda pasipo mkaguzi.

Naona Waziri ameongea kihuni tu, wakurugenz ama bodi inachukua hatua ya kumpa mzabun tenda flan pasipo ushindani, mhasibu anaruhusu fungu litoke kwa amri ya bod au mkurugenzi. Sasa mkaguzi hapo anahusika na nini? Akija mkaguz wa nje yeye ataandika tu tenda flan yalifanyika makosa flani.

Labda shirika flani linaenda kununua madawa ya milion 200, wameenda huko hawajapewa risit au wamekiuka utaratibu, sasa mkaguzi atakagua nini? Mkaguzi kama jinsi anavyoitwa ndivyo anavyotenda, yeye ni mkaguzi tu.

Mfano mmenunua computer 100, je atahakiki 100 zipo? Na documents ni halali? Kabla ya kununua ilifanyika quotation sehemu tofauti? Aliyeauthorize hayo malipo ni mhusika n.k

Sasa mkaguz yeye ni wa kuletewa documents tu ofisin, hana mambo mengi kama tunavyowafkiria.

Tatizo ni mifumo iliyopo katika mashirika na sio mkaguzi.

Ngoja niishie apa
Kama walitakiwa kukagua lakini hawakukagua je?
 
Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ummy Mwalimu ameagiza Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Mamlaka za kinidhamu kuwachukulia hatua wakuu wa vitengo vya ukaguzi wa ndani wa halmashauri 54

Waziri Ummy amesema wakuu hao hawakukagua hesabu za mwisho kabla ya kuziwasilisha kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) ambapo amesema wakaguzi wa ndani kutokagua Hesabu ni ukikwaji wa kanuni za fedha za mamlaka za serikali za mitaa

Katika hatua nyingine ametaka wataalamu wenye CPA walioko kwenye Halmashuri zenye hati mbaya na hati zenye shaka wabainishwe na wafikishwe katika bodi ya wakaguzi (NBAA) ili wachukuliwe hatua stahiki

Ummy Mwalimu ameyazungumza hayo Aprili 9, 2021 jijini Dodoma alipokuwa anazungumza kuhusu ripoti ya CAG kwa Wizara ya Ofisi ya Rais TAMISEMI

View attachment 1748251
View attachment 1748252
View attachment 1748253
View attachment 1748254
View attachment 1748255
View attachment 1748256
View attachment 1748257
Huu ni upotoshaji taarifa sahihi ni hii;
‘Wataalamu wa Fedha wenye CPA(T) wanaotakiwa kufikishwa kwenye Bodi ya Wahasibu(NBAA) ili wachukuliwe hatua stahiki kwa mujibu wa Taaluma zao ni wale ambao Halmashauri zao zimepata Hati Mbaya na Hati zenye Shaka na wao kama wataalamu walisaini taarifa ya hesabu za mwisho kuthibitisha kwamba taarifa hizo ni sahihi na hazina makosa ilihali Ukaguzi wa CAG umebainisha kuwa taarifa hizo hazikufuata viwango wa Kimataifa vya uandaaji wa Hesabu za Mwisho’.
 
Back
Top Bottom